Jehovah Shamah
Member
- Aug 29, 2016
- 18
- 10
Ujumbe wangu kwa Wazazi, juu ya watoto na familia zenu.
Ktk maisha kuna mambo makuu matatu hasa hasa mzazi wa kiume (Baba) anapaswa kuyafahamu:
1. Awe baba anaefikika (accesible)
2. Anaepatikana (Available)
3. Anachukulika (Adaptable)
Kuna wazazi hata watoto wao hawawafikiii, haongei na watoto, hagusiki, hapatikani, hachukuliki wala haigiki.
Anatoka usiku anarudi usiku. Watoto hawamjui, au wamemsahau. Wanamuona kwenye luninga tu.
Sikiliza....Mungu tu anapatikana, wewe kwanini umekuwa adimu hata watoto wameanza kukusahau?
Pamoja na shughuli nyingi lakini tenga muda na familia yako, kagua madaftari ya watoto, rudi mapema nyumbani, kaa, sikiliza. Tenga muda na familia yako. Hata kama wewe ni mtu mkubwa hupatikani, lakini ikumbuke familia yako. Baada ya cheo hicho na heshima hiyo utarudi nyumbani.
Hujaoa au kuolewa na ofisi. Kila kitu lazima kiwe na utaratibu. Kuna muda wa kazini na muda wa nyumbani.
Utaua ndoa yako, na utapoteza upendo wa watoto kwako. Ukifa watatamani wapige mawe kaburi lako.
Tumeshuhudia matatizo mengi ya ndoa siku hizi, mengi yanasababishwa na break down ya mawasiliano, kuchelewa kurudi nyumbani ama kutokurudi kabisa.
Usiri kwa wana ndoa ni hatari. Kwanini husemi kwa mwenzako kiasi cha pesa ulichopata? Mbona ni mwili mmoja, lakini mna akaunti kila mtu yake?
Ujunbe wangu wa leo ni kwamba:
Unbalanced truth always leads to unbalnced living!
Nawatakia siku njema.
Mchungaji Michael Nhonya
DODOMA