Ushauri wa maisha kwa vijana

Ushauri wa maisha kwa vijana

Ujinga mtupu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2017
Posts
887
Reaction score
2,020
Habari vijana wenzangu,

Naombeni niongee na nyie vijana wenzangu kwa haya machache kuhusiana na maisha ya sasa.

Jambo la kwanza naombeni tumpe sana Mungu nafasi katika maisha yetu ikiwa tunayahitaji sana mafanikio,,tusiache kumwamini tu Mungu hata kama nafsi zetu zimebeba majuto sana,maana kumwamini Mungu kunaleta roho ya kujiamini na ujasiri wa kuendelea na utafutaji wa siku zote.

Jambo pili, usiyasubiri maisha ila ishi kwa wakati uliopo. Leo hii kijana tangu mwaka 2015 anakaa kusubiri ajira za mama Samia ilhali maisha inabidi yaendelee hivyo kama unamwamini Mungu basi fanya shughuli yoyote yenye kukuingizia senti yoyote mkononi kuhusu ajira na mambo mengine yatakukuta mbele ya safari.

Jambo la tatu, jitahidi kuwekeza katika kumiliki asset, hapa nazungumza baada ya kuweka akiba au kupata hela yoyote kubwa tuachane na bata kidogo kuna viwanja vipo vizuri tu vya million 1,2 kuna mapori yanauzwa hata heka laki 3. Nunua gari, jenga nyumba, fungua biashara anza hata na mtaji wa mali kauli, kesho yako inakuja kuwa kubwa kuliko mwanzo ulionao.

Jambo la nne, lazima tutengeneze circle yenye kutupa manufaa, katika kuzunguka kwako kubali kuwa chinj ila tamani siku moja kuwa juu wala usijisikie vibaya pale unapoona wale uliosoma nao au kuwaacha shuleni wana maisha ambayo wewe unadhani hauna.

Jitengenezee circle yako, save namba ya kila mmoja unayekutana nae hata kama unaona hauwezi kuwasiliana nao lakini kuna muda itakusaidia. Jitengenezee ukaribu na watu ambao unaona watakufaa kwa wakati mwingine, mfano unajitolea kwenye taasisi fulani na umepata bahati ya kuwa karibu na wakubwa kadhaa jaribu kuwa nao karibu, watakusaidia tu kwa wakati mwingine.

NITAMALIZA KWA WAKATI MWINGINE.
 
Sawa nitaanza na kununua gari
Unadhani gari halina umuhimu mkuu.

Nikwambie mtafute mfanyabiashara yoyote kariakoo au mtu anayefanya biashara za delivery au mtu wa catering waulize hili swali gari na kiwanja kipi cha muhimu uone watakujibuje
 
si ndio maana mimi nimesema nitaanza na ndinga au hujaelewa hapo
 
Habari vijana wenzangu,

Naombeni niongee na nyie vijana wenzangu kwa haya machache kuhusiana na maisha ya sasa.

Jambo la kwanza naombeni tumpe sana Mungu nafasi katika maisha yetu ikiwa tunayahitaji sana mafanikio,,tusiache kumwamini tu Mungu hata kama nafsi zetu zimebeba majuto sana,maana kumwamini Mungu kunaleta roho ya kujiamini na ujasiri wa kuendelea na utafutaji wa siku zote.

Jambo pili, usiyasubiri maisha ila ishi kwa wakati uliopo. Leo hii kijana tangu mwaka 2015 anakaa kusubiri ajira za mama Samia ilhali maisha inabidi yaendelee hivyo kama unamwamini Mungu basi fanya shughuli yoyote yenye kukuingizia senti yoyote mkononi kuhusu ajira na mambo mengine yatakukuta mbele ya safari.

Jambo la tatu, jitahidi kuwekeza katika kumiliki asset, hapa nazungumza baada ya kuweka akiba au kupata hela yoyote kubwa tuachane na bata kidogo kuna viwanja vipo vizuri tu vya million 1,2 kuna mapori yanauzwa hata heka laki 3. Nunua gari, jenga nyumba, fungua biashara anza hata na mtaji wa mali kauli, kesho yako inakuja kuwa kubwa kuliko mwanzo ulionao.

Jambo la nne, lazima tutengeneze circle yenye kutupa manufaa, katika kuzunguka kwako kubali kuwa chinj ila tamani siku moja kuwa juu wala usijisikie vibaya pale unapoona wale uliosoma nao au kuwaacha shuleni wana maisha ambayo wewe unadhani hauna.

Jitengenezee circle yako, save namba ya kila mmoja unayekutana nae hata kama unaona hauwezi kuwasiliana nao lakini kuna muda itakusaidia. Jitengenezee ukaribu na watu ambao unaona watakufaa kwa wakati mwingine, mfano unajitolea kwenye taasisi fulani na umepata bahati ya kuwa karibu na wakubwa kadhaa jaribu kuwa nao karibu, watakusaidia tu kwa wakati mwingine.

NITAMALIZA KWA WAKATI MWINGINE.
Tatizo ss vijana wa siku hizi tumewekeza kwenye ngono na mambo yasiyo na faida katika maisha yetu.

Si ajabu kukuta kijana anatumia zaidi ya asilimia 70 ya kipato chake anacho kipata kwa mwezi tena kwa mateso kuhonga ili kumfurahisha demu wake.
 
Back
Top Bottom