Ushauri wa kununua miti Iringa Kilolo Idete

mtuwatofauti

Member
Jan 21, 2017
25
8
Naomba ushauri wanaJF,

Natarajia kununua miti mia mbili yenye umri wa miaka minne kwa bei ya sh 760,000/=. Biashara itafanyika kwa kutuma pesa kwa M-pesa mimi ntaenda kuiona Mwezi wa sita. Kwa sasa kuna mtu huko atakayefanya makubaliano ya awali.

Vipi imekaaje hiyo?
 
Usifanye hivyo nenda mwenyewe ukakabidhiane serikali za mitaa watu siku hizi siyo waaminifu hata kidogo, jana kuna mtu alimtumia mtu hela amletee ng'ombe yule mtu kanunua ng'ombe kaleta dar kauza huku wanawasiliana vizuri badaye kazima cm kupiga huko kijijini anaambiwa huyu mtu kahama juzi tu na familia yake ndo kufuatilia mawasiliano yake kuja kumpata dalali alikuwa anamtafutia nyumba ya kuishi, sasa kama unataka kudhurumiwa tuma hela
 
Naomba ushauri wanaJF,

Natarajia kununua miti mia mbili yenye umri wa miaka minne kwa bei ya sh 760,000/=. Biashara itafanyika kwa kutuma pesa kwa M-pesa mimi ntaenda kuiona Mwezi wa sita. Kwa sasa kuna mtu huko atakayefanya makubaliano ya awali.

Vipi imekaaje hiyo?
ndugu yangu utaingingizwa chaka ni bora uende mwenyewe huko ukakabidhiwe mbele ya mashahidi au mwenyekiti wa serikali za mitaa kama inawezekana ukituma hela itakula kwako ndugu yangu utatapeliwa usijue la kufanya siku hizi hakuna kumwamini mtu ni bora upange safari uende mwenyewe
 
Mkuu hela ilivyo ngumu unaleta masihara! Uaminifu ilikuwa zaman! For now its a lot of money! Ukizubaa utakuja kulalamika jf!
 
Nenda uione miti, hesabu idadi, wafahamu majirani wanaopakana na shamba, andikishaneni serikali ya kitongoji /kijiji, shiriki taratibu za kupambana na moto unapotokea.
 
umenikumbusha sfari yangu ya kwnda Kijiji cha Itonya nilikua napiga kambi hapo Idete.
Nenda kwanza ukapaone, palivyo mbali kutoka kilolo ukidhulumiwa hata kufuatilia utakata tamaa,
Kuna bus moja tu inaenda huko kutoka Iringa, kuna guest house 2 tu last time nimeenda room ilikua Tsh.2500 na unaoga nje kwny bafu ilizongushiwa miti.
 
Hahaaaa mie umenikumbusha nilifanya safari ya kufika Uluti...
Wakati wa kwenda nilipanda gari la padri siku ya kurudi nilihenya kipindi hicho gari zaishia Dabaga nilitembea kutoka Uluti hadi Dabaga nikichapwa na mvua...

Zila sifa za kufanya utalii na uchunguzi kwenye vijiji vya Tanzania ziliniiisha...

Ila Idete nilipata msosi wa maana wali kwa Samaki mkubwa bei rahisi...

Pale kwenye bonde la mto Lukosi palikuwa na shule ya sekondari ikijengwa nadhani itakuwa imeshatoa wahitimu kadhaa...

Kwa mtoa mada hiyo pesa huenda ni ndogo kwako lakini ukitapeliwa ndipo utajua ukubwa wake..
 
Nenda uione miti, hesabu idadi, wafahamu majirani wanaopakana na shamba, andikishaneni serikali ya kitongoji /kijiji, shiriki taratibu za kupambana na moto unapotokea.
Dah asee juzi nimetoka ludewa nimekuta mashamba yaliyoungua hadi nikajisikia chozi kunishuka. Pia kuna hii njia ya songea,mbea kabla hujafika lilondo kuna mengine moto umepita ajabu dah!
 
umenikumbusha sfari yangu ya kwnda Kijiji cha Itonya nilikua napiga kambi hapo Idete.
Nenda kwanza ukapaone, palivyo mbali kutoka kilolo ukidhulumiwa hata kufuatilia utakata tamaa,
Kuna bus moja tu inaenda huko kutoka Iringa, kuna guest house 2 tu last time nimeenda room ilikua Tsh.2500 na unaoga nje kwny bafu ilizongushiwa miti.
Mi nlikuwa njombe juzi mkuu dah wilaya ya ludewa huko kuna kijiji kinaitwa mavanga duh mbali kupindukia kutoka tuu njombe to mavanga nauli 10000
Kuna mwekezaji mmoja yuko katikati ya madaba na mavanga
Anamiliki shamba kumbwa la Ndolela estate analima soya na mahindi ila kuna mashaka ya huyo mwekezaji kuvuna dhahabu pale wakubwa inabidi wwangalie kwa macho ya karibu maana maeneo mengi kule ni madini tupu.
 
Ukiona mtu unataka kumtumia hela alafu haweki msisitizo wa kama anaogopa kufanya maamuzi kwa niaba yako yaani kuonyesha kwamba anakuhitaji wewe mwenyewe uwepo (shituka!!!) unless kama uliwahi kufanya deal nae several time na anajua vitu unavyopenda. In this case, nenda eneo la tukio mwenyewe
 
Back
Top Bottom