Kwa mara ya kwanza naijitokeza kwenu familia ya JF kuomba kuifahamu vizuri course ya public relation hii inakuaje na inafaida gani na unaweza fanya kazinkama zipi?
hakuna kozi ambayo ni mbaya isipokuwa tu ubaya wa kozi unatokana na wewe kutoajirika. public relations ni kozi mahsusi kwa masuala ya mahusiano ambapo ukiwa serikalini utaitwa information officer ( afisa habari ) na ukiwa katika private sector utaitwa public relations manager / officer ( afisa uhusiano ) ila kazi zao ni zile zile na zinafanana isipokuwa ukiwa serikalini utasota mno kutoka kwani pesa za serikalini zinapita katika mlolongo mrefu huku kukiwa na figisu figisu nyingi na kuna kubaniana sana na kutoka kwako ni labda ungojee shughuli za wizara au saba saba kilwa road na semina ambazo hata hivyo siku hizi hazipo nyingi lakini ukiwa katika kampuni binafsi lazima utatoka mno na haraka kimaisha kwani huko fursa ni nyingi mno na hata mishahara yake ni mizuri na privileges zingine na ni kuzuri. mfano ulio hai tu ili uelewe ninachokisema hebu muangalie afisa habari au msemaji wa serikali ndugu arthur mwambene halafu mfananishe na afisa uhusiano wa vodacom kelvin twisa utapata jawabu ya nilichokisema hapo juu.
siku hizi hiyo kozi imebadilika na mahala pengine inajulikana kama corporate relation management na muhusika anaitwa corporate relation manager ila suala hili utalisoma zaidi ukifika ngazi za master's degree kwani mara nyingi status hii utaipata kama ukiwa na shahada ya uzamili lakini kwa shahada ya kwanza utabaki na status ile ile ya information officer au public relation officer.
kuhusu faida gani sijakuelewa ila kama unaulizia mshahara ufafanuzi nimeshakupa hapo juu ila kama ni faida ya kikazi kubwa zaidi ni kutengeneza tu mahusiano mazuri na wadau wako wakuu ambao ni watu, vyombo vyote vya habari na ofisi yako kupitia service mnayoitoa.
kazi zake ni zile zile tu :
- public relations manager
- information officer
- corporate manager / corporate relation manager
- communication manager
- head of corporate management
- communication coordinator
- communication program manager
nadhani nitakuwa nimejaribu kukupa ufahamu japo kidogo na naomba niwaachie na wengine. nakutakia kila la kheri katika kutimiza lengo lako.
Asante sana kaka nimepata mwanga now na kuelewa maana yake coz nilikuwa sina ufahamu huo