Ushauri wa kitaalamu kwa wanaohitaji kulima kibiashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa kitaalamu kwa wanaohitaji kulima kibiashara

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by JBAM, Feb 16, 2012.

 1. J

  JBAM Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima kwenu wanajamvi.
  Tanzania tumekuwa na sera nyingi za kuendeleza kilimo cha mtanzania (mkulima mdogo mdogo) kwa miaka hamsini sasa. lakini pamoja na sera nyingi na zenye mvuto masikioni tumeshindwa kufikia lengo kama nchi. Moja ya changamoto kubwa ambayo imekuwa ikisahaulika ni wataalamu wenye uwezo wa kumshauri mkulima kwa wakati sahihi juu ya zao gani aoteshe wapi, aoteshe vipi, lini, udhibiti wa magonjwa na wadudu waharibifu, uhifadhi wa udongo kwa kilimo endelevu na matumizi sahihi ya mbolea. hii imekuwa ni changamoto kwa muda mrefu sasa kwa wakulima wa Tanzania ukilinganisha na baadhi nchi za jirani zilizofanikiwa kuboresha kilimo.

  Kwa kutambua changa moto hii tumeanzisha consulting firm ambayo kwa sasa ina ofisi zake mjini Morogoro na Moshi ambapo unaweza kupata ushauri sahihi wa kitaalam kuhusiana na kilimo cha mazao yote yanayostawi katika ukanda wa kitropiki (tropical crops) popote ulipo katika Tanzania. Pia tunatoa huduma ya upimaji udogo ili kutambua mahitaji ya rutuba katika udongo, tunauza mbegu mbali mbali zenye ubora na madawa ya kudhibiti wadudu na magonjwa.

  kwa wale wafanyabiashara na wafanyakazi wa sekta nyinginezo (zisizo za kilimo) ambao wangependa kulima kibiashara nafasi ndio hii.

  Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuni PM au kutumia simu namba 0653649152.
   
 2. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante kwa taarifa mkuu. Labda hii inaweza kuwa njia nyingine ya kumkomboa mtanzania anaelima.
  Nafikiri ni vema ukaweka na bei zenu yaani consultancy fee itakua njema zaidi

  Thanks
   
 3. J

  JBAM Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru mkuu kwa mchango wako. napenda kukuhakikishia kuwa bei zetu ni za kizalendo kabisa kwa ajili ya wakulima wadogo na wajasiriamali wa sekta ya kilimo. gharama hutofautiana kutegemeana na shamba lilipo (mkoa ulipo). tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia namba hiyo. huduma zetu ni za haraka hakuna ucheleweshaji
   
 4. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kama mmejipanga vizuri na mmeangalia wapi tulipokosea ktkt hiyo miaka 50 ya uhuru basi tunawatakia kila la kheri...

  Hofu yangu ni kuwa kwa sera hizi mbovu za kilimo tulizonazo sijui kama malengo yenu yatatimia. Mkulima mdogo ana matatizo mengi sana ambayo utatuzi wake ni wa kisera. Hata mkiniuzia mbegu leo, nitaendaje kulima kwenye shamba langu lile lile ambalo halipapimwa na siwezi kulitumia kama dhamana ili nipate mkopo wa kuliendeshea? Je mvua ikikatiba baada ya mwezi mmoja kuna insurance yoyote ya kumlipa huyu mkulima kwa nguvu na gharama alizotumia? Anyway, karibuni sana.
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  MKUU HONGERA SANA KWA HILI NA HILI LITAWAKOMBOA SANA WAKULIMA WA TANZANIA, MAKE KILIMO CHA KISASA NI MUHIMU SANA KATIKA KUFNIKISHA KILIMO KWANZA.

  ILA MKUU KUNA MAHALI MIMI NITATOFAUTIANA NA WEWE KIDODO, ILA NI KATIKA KUJENGA NA SI KUBOMOA MKUU,

  1. Mkuu Ni kweli wakulima wengi wamekuwa hawafuati njia za kisasa katika kulima,hilo silipingi, ila mkuu kilimo cha Tanzania kina kabiliwa na changamoto moja kubwa sana nayo ni MASOKO

  - Mkuu MASOKO ndo tatizo kubwa kwa wakulima wa Tanzania na kuna wakulima wanajitahidi sana kulima kitalaamu lakini hawajui wapi pa kuuza, ni mefanya kazi na NGOs moja inaitwa Faida Market Linkage company, hii ilikuwa na jukumu la kufanya Market Linkage kati ya wakulima na wanunuzi so ilikuwa ni kama Daraja kati ya watu hao wawili,

  Mkuu mfano mzurri ni wakulima wa Machungwa kule Tanga, machungwa yanaozea kwenye miti kipindi cha msimu na hawana pa kuyapeleka na wanalazimika kuuza kwa hasara

  Kule Kilimanjaro wakulima wamefikia hatua ya kung'oa kahawa waoteshe mazao mengine kisa ni Masoko

  Kule kusini mikoa ya Luvuma wakulima huvuna mahindi ya kufa mtu lakini hawana pa kuyauza na inafikia mahali wanaamua kuuza kwa hasara, mkuu hiyo ni mifna michache,

  Wakulima wanaweza lima kisasa kabisa but kama hakuna masoko ya uhakika ni kazi bure mkuu na hii ndo tatizo linalo wavunja moyo wakulima wa Tanzania wengi hukata tamaa ya kulima kwa sababu ya masoko ya mazao,

  Mkuu kikubwa cha kwanza kinacho takiwa kufanyika ni kutafuta masoko ya uhakika ya wakulima then ukija na mpango huu utafankiwa sana, na kilimo cha biashara ni kitendo cha mkulima kufanya kilimo sawa sawa na biashara nyingine yoyote ile

  Kilimo cha biashara inatakiwa mkulima Aingie shambani huku akijua anaamuuzia nani hayo mazao yake, na si mkulima alime then asubiri walanguzi waje na mafuso mashambani, Kilimo cha kisasa bila kuangalia masoko ni kazi bure mkuu, na kilio cha wakulima wa Tanzania ni masoko ya mazao yao,
  Cheki mfano wa kilimo cha Pamba, kwa sasa kinakufa kwa sababu ya msoko, kilimo cha tumbaku kinakufa wa sababu ya masoko

  SO MKUU KAMA MNAWEZA JARIBU KUFANYA NA MARKET LINKAGE HII IKIENDA PAMOJA NA HIYO KAZI NYINGINE ITAKUWA VIZURI SANA,
   
 6. l

  lumbagengata Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari Mkuu ,tunashukuru kwa wazo lako na jitihada hizo. Hebu nijuze ,unayo mbegu ya Mpunga aina gani na ina sifa gani? na bei zikoje ? nijuze hiyo ili tuone kama tutaweza fanya na huduma muhimu,natamani ungekuwa consultant wangu ktk shughuli hizi za kilimo. Kwa utalamu wako Kitunguu maji kinatoka gunia ngapi zenye ujazo gani wa katika ekari moja? na mbegu unayo lkn, ?
   
 7. i

  iMind JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,908
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  The idea is good. Tunaposema wasomi kujiajiri tunamaanisha vitu kama hivi. Traditionaly huduma hizi zimekua zikitolewa na serikali kupitia kwa maafisa ugani, ambao wako wachache, hawana vitendea kazi n.k. Kwa kua kilimo ni biashara we can no longer rely on them.
  Msijikite tu kwa wakulima wadogo, lakini pia angalieni jinsi gani mnaweza kufanya kazi na wakulima wakubwa. Kwa mfano they can outsource baadhi ya kazi kwenu.

  Pia angalieni how you can help kwenye suala la masoko. Pia NGO na serikali can contract you kufanya kazi fulani fulani kuhusu kilimo. Mnatakiwa pia mjenge mtandao mzuri na taasisi za utafiti za mazao mbalimbali, they can contract you to do some extionsion services.
  There are millions ideas, however kwenye ujasiliamali katika biashara ya ushari mnahitaji kuwa competent, mdelive siyo longolongo. Nawatakia kila la kheri
   
Loading...