Ushauri wa Kibiblia kwa Rais wangu JPM

Slas Nature

Member
Oct 18, 2013
36
72
Assaalam alaykum.! / Tumsifu Yesu Kristu.! / Bwana Yesu asifiwe.!

Awali ya yote ninamshukuru Mungu kwa nafasi hii ya uzima mpaka sasa, lakini pia ninamshukuru kwa kupata nafasi hii ya kutoa kile kidogo ambacho kipo moyoni mwangu kwa Rais wangu Jonh Pombe Magufuli. Ni maombi yangu unaposoma waraka huu mfupi uusome kwa jicho la kimungu na la kujenga zaidi.

Si jambo la kupinga kwamba Rais wetu ana nia njema ya kuijenga Tanzania mpya yenye amani na maisha mema kwa wananchi wote na amekua akionyesha hisia zake waziwazi mbele ya watanzania wote lakini pia amedhihirisha hilo kupitia matukio kadhaa ambayo amekua akiyasimamia akiwa na lengo la kumsaidia mtanzania wa hali ya chini.

Pamoja na hayo zipo changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikionekana dhahiri katika utendaji wa Rais wetu hasa katika suala zima la matamko au maamuzi ambayo anayafanya, na sababu mojawapo inawezekana kabisa wanaomzunguka hawatoi taarifa sahihi juu ya jambo fulani, si rahisi sana kwa Rais kujua kila linaloendelea nchini kwa wakati mmoja hivyo anategemea watendaji wake wampe taarifa sahihi ili afanye maamuzi sahihi yenye matokeo mema..

hebu tuangalie mstari huu...

Mithali 29:12
"Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu"

Umeuona huu mstari? Huyu ni Mungu anatuambia kuwa mwenye kutawala yeyote (mathalani Raisi) akisikiliza uongo (yaani taarifa isiyo sahihi) basi watumishi wake wote watakuwa waovu maana yake watatenda yasiyopendeza kwa Mungu na wananchi pia, mtu mwovu ni yule asiyetenda yanayompendeza Mungu na wanadamu wenzake.. na watumishi wakiwa waovu nini kitatokea?

Mstari huu unatupa jibu.. hebu tuusome

Mithali 29:16
"Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka;.."

Hii ni hatari sana maana watumishi waovu wanapoongezeka ndivyo na maasi yanavyoongezeka, hivyo baada ya muda tunaweza kuwa na jamii yenye kuasi iliyojaa waovu kila mahali, lakini kosa lilianzia wapi? ni kwa mtawala kusikiliza taarifa zisizo sahihi.. Sasa madhara makubwa ya maasi au maovu kuongezeka ni Mungu kuacha kutusikiliza na kutusaidia... hebu tulitazame hili katika kitabu cha Isaya

Isaya 59:1-2
"Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia; lakini MAOVU yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia"

Umeona hapo? Mungu anatuambia kwa sababu ya maovu yetu ataacha kutusikiliza, hivyo Pamoja na Raisi wetu kutaka tumuombee lakini kama asipokuwa makini na maamuzi na anachoambiwa basi itakuwa kazi bure maana maombi yetu hayatapokelewa.

Hivyo basi ushauri wangu kwako Mhe Raisi ni kuwa makini na unachoambiwa, tunajua saivi viongozi wengi wameshakujua jinsi ulivyo, hivyo wengine wanalazimika kukupa taarifa zisizo sahihi ili usiwatumbue na wengine wanatoa taarifa zisiko sahihi kwako ili uwaone watenda kazi wazuri na uwapandishe vyeo,, hivyo ni vyema ukawa mwangalifu sana katika kila unachoambiwa. Lakini pia uwe na washauri wazuri ili taifa letu lisianguke maana mithali inatuambia...

Mithali 11:14
"Pasipo mashauri taifa huanguka; bali kwa wingi wa washauri huja wokovu."


Mwisho, nitoe Rai kwa baadhi yetu ambao tumeacha kuwa na utii kwa serikali yetu kwa sababu ya changamoto kadha wa kadha au kutotimiziwa wanayotaka wao. Maandiko yanatuambia katika kitabu cha Warumi.

Warumi 13:1-3
"Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake."


Niwatakakie siku njema, Mungu awabariki nyote.
 
Hii ni tangu tupate uhuru . ..ndiyo maana anajitahidi kubadilisha mfumo maana nchi ilikuwa imeoza na tulikuwa tunaiuza kwa wageni . ...tumshukuru MAULANA MOLA WETU RHABUKA kwa kutushushia mkombozi wa taifa letu . .mtukufu rais wetu JPJM . ..asante MWENYE ENZI MUNGU kwa upendo wako kwa nchi yetu Tanzania milele . ..ubarikiwe
 
Back
Top Bottom