ha ha ha ha ha ha! C.T.U, sijui ulikuwa una maanisha nini hapo kwenye bold!Uko wapi?? Kama uko mjini tafuta sehemu yenye ofisi nyingi then fungua stationary..target kuwauzia watu wa maofisini kwa jumla na reja reja anza kujipendekeza kwa watu wa ofisini kama wewe ni mwanamke itakuwa rahisi kwako kupata connection
....Nikopeshe shilingi Milioni Moja na baada ya Mwezi ninakurudishia Milioni Moja na Laki Tatu. ukifanya hivyo kwa watu wa Nne tu unakuwa kila mwezi una Shilingi Milioni Moja na Laki Mbili ya Matumizi yako bila Kugusa Mtaji Wako Wakati Ukiendelea Kutafakari cha Kufanya. NiPm kama Upo tayari.
Jaribu u agent wa mpesa,tigopesa, airtel money etc! Naamnini haihitaji mtaji mkubwa sana kuanzisha na hivyo itakufanya uwe na pesa ya kutosha kuzungusha! Say utatumia kama 5m kwa ajili ya miundo mbinu (hasa kukodi au kupata sehemu ya kufanyia biashara) na kubakiwa na 20m kwa ajili ya kuizungusha na 5m inabaki kama ya dharura.
Kuna soko kubwa la mashudu ya alizeti na pamba huko Kenya. Kuna wakenya wanakuja kila siku Singida, Tabora, na Shinyanga kutafuta mashudu wao wenyewe sasa kama unaweza kupeleka hata mpaka Namanga wawe wananunua kwako. Fanya utafiti uone kama itakufaa hii biashara.
Nina lori (semi linaweza beba hadi tani 30) kama utahitaji usafiri au kushirikiana kama utachagua biashara yeyote itakayohitaji usafirishaji.
Kila la kheri
Wa Tanzania Bana, Utatujua tu,
Kwa kifupi ni kwamba Wewe Mleta mada Ulikuwa na Makosa, Uliwezaje kwenda Kukopa kabla ya Kujua unacho enda kukifanya? Au unachora watu Humu?
Mkuu kama Uko Dar wewe Tafuta watalamu wa Maswala ya Biashara wakushauli ni nini cha Kufanya na hizo pesa, Ila cha Muhimu ni Bora ukaenda na ,Mawazo yako kama matatu wakusaidie kuchambua ili ibakie Moja, Na ni bora ukae chini utengeneze wazo lako mwenyewe kulingana na mazingira ya sehemu ulipo,
Na ni lazima liwe wazo la Biashara Endelevu ya Miaka na miaka na si Biashara za Musimu mara leo Unanunua Mahindi, mara kesho uko kwenye Mafuta, kesho kutwa kwenye Nguo, So kaaa chini wewe mwenyewe na Umiza kichwa na utapata wazo Bora kabisa, NA WAZO BORA LA BIASHARA NI UNALO ANZISHA WEWE MWENYEWE
Mkuu mlata mada hajakosea kitu ila nafikiri hujamwelewa vizuri. Amemaliza kusoma na bro ameahidi kumpa 30m afanye biashara, kwahiyo kijana amekimbilia JF kuomba msaada. Kama una mawazao mazuri ya biashara mshauri, huwezi jua kesho anaweza kuwa mwajiri mzuri akaajiri na wadogo zako, wewe si unaona ajira zilivyo ngumu ziku hizi? Tunatakiwa tupeane support na siyo kukatishana tamaa na hasa kwa wajasiriamali.
Bobo kuna thread nyingi humu ndani ambazo zilikuwa na mawzo mazuri ya ujasiriamali, nakushauri search uzipitia zitakusaidia.