Ushauri wa haraka kuokoa biashara yangu

Mkuu usivunjike moyo jitahidi wewe na familia yako kujikita katika maombi ya nguvu mambo yatakaa sawa tu.

-Ndumilakuwili-
 
Jichunguze namna unavohudumia wateja wako, punguza ile lugha ya ukakasi kwa wateja wanaokukera, kumbuka wanakukera wewe hawaikeri biashara yako,


lazima ukubali hasara Fulani ili upate faida badae,
 
jichunguze kauli zako.....unaweza fikiri unaongeza vzr kumbe unatoa kaul chafu na majibu ya kuudhi kwa wateja..... usiwe mwepesi wa kukasirika na kukunja sura kila saa!

wateja wengi wa maduka ya kawaida ya chakula na bidhaa muhimu za nyumbani ni wanawake.... kwenye hili kundi kuna house girls, ambao kama tujuavyo hawa wadada hupewa majukumu ya kuhemea vitu madukan magengeni sokoni n.k, pia wapo wamama na kina dada ambao kwa namna moja nao wanahusika sana kununua bidhaa muhimu kama mchele unga sukari n.k !
makundi niliyotaja hapo ndio wateja wakubwa wa dukani, sasa napata mashaka pengine hawaridhiki na huduma unazotoa kulingana na sababu nlizotaja hapo mwanzo mfano kauli n.k na hii ni kasumba ama jadi, wanawake kwa wanawake hampendani , kulingana na hzo sababu wanashindwa kuja dukani kwako wanakupita na kwenda pengine.... !

pole jichunguze vyema uangalie unapokosea.... kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda nikuulize mwanzo ulikua unauza bei gan maana umesea tu ya sasa kwamba buku mpka buku kumi. Pia inategemea una mwombaje mungu maana tunakosa ving tunavyoomba kwa kukosea kwetu kuomba,huwez kumwomba mungu biashara yako ishamiri ni uongo tuliorithishwa,sababu unaweza kua unachanganya sala na maombi we ukajuona upo sahihi kumbe unakosea. Ngoja nikufundishe njia ya kua karibu na mungu na mungu akusikie mapema

SHUKURU KWA KILA JAMBO,HATA LIWE GUMU KIASI GANI,MUNGU ANATAKA TUMTUKUZE TU,MAANA ANAJUA MHITAJI LAKO,WE SHUKURU KWA KILA HALI,HATA KAMA HUPATI HATA MIA MWAMBIE MUNGU NAKUSHUKURU KWA HALI HII NAKUACHIA BIASHARA YANGU MIKONONI MWAKO,UWE MWANGALIZI WANGU KUANZIA SASA NA HATA MILELE.

THEN WAKATI WA KUOMBA JARIBU SANA KUOMBEA WENGINE,OMBEA WATOTO WAKO NA WAWENZAKO,OMBEA VIONGOZ WAKO WA KIROHO NA KISERIKALI,OMBEA WAGONJWA,OMBEA WAJANE,OMBEA MAYATIMA,OMBEA WASIOMWAMIN MUNGU,OMBEA YYTE YULE CHINI YA JUA MAANA IMEANDIKWA YEYOTE AJITOLEAE KWA AJILI YA WENGINE NITAMBARIKI,SO UKISHPATA BARAKA ZA MUNGU NDIO UTAJIRI HASWA UNAPOKUJA,HAKUNA UTAJIRI BILA BARAKA ZA MUNGU,LABDA KM UNAMTUMIA SHETAN JAPO NAE ATAKUPA ILA ATAKUUMIZA.

UNAPOSEMA MUNGUNAOMBA BIASHARA YANGU IKUE,NIPATE HELA,NIPATE NYUMBA,NIPATE MTOTO,NIPATE KAZI JE MMESAHAU SHETANI NDIE ATAKUITIKIA MAANA VYA ULIMWENGU HUU VINGI ANAVIMILIKI SHETANI?

Baadae
 
Habari wana jamvi, matumain yangu hamjambo.
Ngoja niende moja kwa moja, n hv nlijichanga nkapata mtaji nkafungua duka la bidhaa mchanganyiko mkoa wa Pwani sasa mwanzon wiki ya kwanza biashara haikua nzuri ila cku zlvyozd kwenda ikachangamka mauzo yakawa yanapanda mpk laki,

sasa kuna cku wakat nataka kufunga ilkua cku ya j3 nkaona juu kabsa ya geti ambapo n parefu kwelii kufkia mpk uweke kiti kirefu sn nkaona pana soks pair moja za mtoto zmebanwa na kibanio nkashangaa sn zmefkaje kule ikabd nmuite mume wng akasema n watoto watakua wameweka mmh nkamwambia poa,

sasa bwana toka siku ile mauzo yamepungua sn naweza fungua asbh mteja wa kwanza akaja sa nane nalala naamka nalala naamka hakuna mteja, najitahid sn kukemea hii ila cjajua iman yng n haba au vp.
Kwan naweza kuuza ht elfu moja tu kwa cku, inaniuma sn.
Nikiuza sn elfu 10 navunjika moyo, naomben ushauri na mm iman za waganga siziamn kweli.

Nafanya maombi lkn wap mara tu nnavyofungua.
Naomben ushauri ila kwenye huu mtaa yapo maduka km 6 hv km langu.
Nawaza nfunge tu kwan kod yng haijaisha na kwenye hii biashara nna miez mi5 tu.

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
Funga kula siku saba, ukiombea biashara yako kwa maombi ya nguvu wakati huo usiache kufungua.... Itakuwa vzr like never before. Mrejesho muhimu.....
 
Biashara ndivyo zilivyo..sasa kama unasema mtaani hapo kuna maduka 6 kama lako unategemea nini? Tafuta mahali pengine au badilisha aina ya biashara!

Hapo hamna uchawi, ni demand tu ndogo hivyo mnagawana wateja! Mi ilinikuta nikafungua biashara sehemu ambayo kuna biashara 2 kama yangu, kuna siku nilikuwa naletewa mauzo elf 3 na nimewekeza zaidi ya 8m imagine, ilibidi nifunge niconcentrate kwenye biashara ya mwanzo!!

Hivyo basi location ndo kitu cha msingi kuliko vingine vyote, pia namna unavyointerract na wateja, huwezi jua wanakuonaje!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikimbie hiyo ni changamoto ikabili,labda ndio eneo lako la riziki yako ya daima ukienda kwingine huenda mambo yasiwe sawa endea tu kuomba kwa Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku tulifungua ofisi asubuhi tukakuta paka ndani amekufa.

Geti letu ni yale yanayoshushwa kufunga na kupandishwa kufungua, ni kama coil yaani.
Mimi na mwenzangu tukaambiana hivi "Ujue hili geti tunalivuta vibaya hadi hapa mbele pameinuka ndiyo maana paka kaweza kuingia"

Siku nyingine tumefunga ofisi mwenzangu kuna kitu akawa amesahau tukarudi kukichukua.
Tumefungua geti tu akatoka paka mule ndani mbio.

Na bado tukang'ang'ana na nadharia yetu ile ile.
Baada ya hapo nini kiliendelea.? Kulikuwa na madhara kama ya mleta uzi? Au hapana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana jamvi, matumain yangu hamjambo.
Ngoja niende moja kwa moja, n hv nlijichanga nkapata mtaji nkafungua duka la bidhaa mchanganyiko mkoa wa Pwani sasa mwanzon wiki ya kwanza biashara haikua nzuri ila cku zlvyozd kwenda ikachangamka mauzo yakawa yanapanda mpk laki,

sasa kuna cku wakat nataka kufunga ilkua cku ya j3 nkaona juu kabsa ya geti ambapo n parefu kwelii kufkia mpk uweke kiti kirefu sn nkaona pana soks pair moja za mtoto zmebanwa na kibanio nkashangaa sn zmefkaje kule ikabd nmuite mume wng akasema n watoto watakua wameweka mmh nkamwambia poa,

sasa bwana toka siku ile mauzo yamepungua sn naweza fungua asbh mteja wa kwanza akaja sa nane nalala naamka nalala naamka hakuna mteja, najitahid sn kukemea hii ila cjajua iman yng n haba au vp.
Kwan naweza kuuza ht elfu moja tu kwa cku, inaniuma sn.
Nikiuza sn elfu 10 navunjika moyo, naomben ushauri na mm iman za waganga siziamn kweli.

Nafanya maombi lkn wap mara tu nnavyofungua.
Naomben ushauri ila kwenye huu mtaa yapo maduka km 6 hv km langu.
Nawaza nfunge tu kwan kod yng haijaisha na kwenye hii biashara nna miez mi5 tu.

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
The same to me!! What a Coincidence!!! Mimi nami biashara imepiga u turn mpaka nachanganyikiwa. Hapa Dar kufanya biashara ya duka bila Akili mbili huifanyi nimegundua. Wataalamu ni wengi. Unasubiri mteje mpaka Unachanganyikiwa
 
Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarawajiayo,ni bayana ya mambo yasio onekana (Ebrania 11:1)
..kama unaomba huku unamashaka ni ngumu kupokea ndg...pia hata maombi ya ulegevu huwa majibu ni magumu...nakushauri funga pia tazama WRM tv kuongeza imani yk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikate tamaa anza urafika na wenye maduka kama lako watakupa maarifa. Najua wivu upo lakini zungmza nao taratiiibu (life is a game play it)

Sent using Jamii Forums mobile app
bahati mbaya ni kwamba wafanyabiashara wa kitanzania kwa 99% hawapendi kushare na wengine kuhusu biashara zao hasa kama atagundua anaetaka ushauri kwake ni mtu anayefanya au anayetaka kufanya biashara kama yake.
 
SULUHISHO LA HARAKA: Hama hapo haraka iwezekanavyo,washaweka vyao hata aje mtu mwingine itakuwa hivyohivyo mwishowe anafunga.
 
HOFU imekutawala tu hakuna kingine.

Biashara huwa ina faida na hasara, kiangazi na masika,sasa usifurahie tu unapokutana na kipindi kimoja badala yake furahia unapokutana na vipindi vyote hasa cha faida..

Na inapotokea umepata matatizo katika biashara yako tafuta chanzo chake ni nini? Na sio kulalamika na ukipata chanzo chake anza kukabiliana nacho mapema ili kisije kukuletea madhara makubwa.

Binafsi nimekuelewa vizuri sana mkuu, ila nimejaribu kufuatilia kiundani zaidi nimegundua kwamba wewe sasa hivi unaendeshwa na HOFU na pia unahisi kuna imani za kishirikina ambazo wafanyabiashara jirani zako wamekufanyia,tena chanzo kikuu cha yote ni ile Sox uliyoikuta dukani kwako.

Na mimi binafsi NALIPINGA KABISA hakuna mchezo wowote uliochezewa,kwanza naomba jiulize maswali haya

1)Thamani uliokuwa unaitoa kipindi cha nyuma na sasa vinaendana?

2)Je baada ya kuona unapata wateja wengi uliendelea kuongeza thamani au ulibweteka?

3)Je huduma unayoitoa hapo katika biashara yako inapanda kila Siku au inaenda inashuka?

4)Je Unakauli gani kwa wateja wako Nzuri au mbaya?

5)Na Je bidhaa zako na huduma zako ni bora au zinashuka Siku hadi siku?

Tafadhari naomba jiulize maswali hayo na kama uko tofauti,basis jirekebishe na naimani wateja watarudi tu,

Weka bidhaa bora zaidi na toa huduma bora zaidi na utapata wateja wengi zaidi.

Nikutakie Siku njema..

Kocha Deus

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom