USHAURI WA BURE:Serikali iwe makini na mkataba wa ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI WA BURE:Serikali iwe makini na mkataba wa ATCL

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,589
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  Serikali iwe makini na mkataba wa ATCL


  HATUA za kunusuru uhai wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) zinaendelea kushika kasi, huku serikali ikiwa imeshampata mwekezaji wa kutoka China ambaye tayari ameshakubaliwa.

  Serikali imefanya hivyo ili kurejesha heshima ya kampuni hiyo inayopeperusha bendera ya taifa letu katika medani za usafiri wa kimatiafa ambayo sasa imeshuka baada ya huduma zake kufa.


  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, mpango huo unaosimamiwa na ofisi ya rais kwa ufanisi, tayari mwekezaji huyo amenunua ndege mbili.


  Kwanza tunapongeza juhudi za serikali za kufufua shirika letu la ndege. Hata hivyo, tunaitahadharisha kuwa iwe makini kwa kuhakikisha kuwa inaingia mkataba na mwekezaji mwenye sifa zinazostahili, ili yasitokee tunayoshuhudia kwa kampuni ya TRL ambayo mwekezaji wake amebainika kuwa ni mbabaishaji.


  ATCL haina tofauti na TRL kwa kuwa inaliunganisha taifa hilo na jumuiya ya kimataifa na kuchangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa biashara ya utalii na masoko ya kimataifa pamoja na ustawi wa taifa kwa ujumla.


  Yanayotokea TRL yanadhihirisha jinsi serikali ilivyokosa umakini katika kuchagua mzabuni sahihi, hivyo tunaomba isiwe hivyo kwa ATCL.
   
Loading...