Ushauri wa Bure Kwa Wanaume wote

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,468
1,329
Heshima yenu nyote wapambanaji wenzangu.Matumaini yangu mmeamka na mnaendelea vizuri na majukumu ya kila siku. Tuje moja kwa moja kwenye mada.

Ipo hivi ukitaka kufa masikini kama unafamilia tayari kwepa kuhudumia familia yako au jifanye majukumu yako huyajui na umwachie mkeo ndio atunze familia.

Kuna uhusiano mkubwa sana baina ya fikra za mwanaume katika kuhudumia familia yake na mafanikio yake.

Sijui mnanielewa ndugu zangu wa kiumeni?

Kuhudumia familia kunaleta baraka kwa mwanaume, huamsha ari na shauku, humpa nguvu, humuongezea ubunifu na bidii.

Kila anapoamka asubuhi akijua kuwa watoto wanatakiwa wale, wavae, wasome, wafanikiwe, mke inatakiwa avae, apendeze, ale na kila kitu kiwe sawa kutokana na kipato chake inatosha sana kumfanya aweke juhudi na apambane kuhakikisha hilo linafikiwa na kwa kufanya hivyo inamfungulia mlango wa mafanikio kadiri umri unavyozidi kwenda mbele.

Ila sasa hapo inabidi mwanamke( mke) nae ahakikisha haui hii hamasa ya mume, anatakiwa kumtia moyo na kumuamini kwa vitendo.

Usijaribu kabisa kupuuza juhudi zake wala uwekezaji wake kwako hata kama ni mdogo kiasi gani usijaribu kupuuza nguvu zake usijaribu kuona afanyacho hakina thamani.

Kukuhudumia wewe na watoto wako ni upendo mkuu na mara nyingine mimi husema wanaume wanapo amua kuchagua mke wa kuoa sio kwa ajili ya ngono ni kwa sababu wanahitaji faraja na mtu wa kushea nao maisha.

Good Morning dear Friends
 
Good morning to you too dear friend.

Mzani wako umeelemea upande mmoja. Sikuhizi haki sawa. Weka tuweke! 🙌🏽

Being Goalkeeper ni mambo za kizamani hizo.
 
Hudumia familia Ila usiache kujiweka akiba yako binafsi na kujiurahisha mwenyewe mwanaume unaweza kujitoa Kwa wanao mkeo siku life likichenji wale uliojitoa kwawo ndyo wakakupa stress zaidi ukaachwa na wanao wakasema kuwa kipindi Una pesa ulikuwa huwajalii sababu ulikuwa uwatoi out wakati uliwasomesha shule nzuri chakula cha uwakika home mavazi na sehemu nzuri ya kulala Ila bado watakuona hukufanya lolote juu Yao Baba beba majukumu yako Ila jijali sna tena sna
 
Good morning to you too dear friend.

Mzani wako umeelemea upande mmoja. Sikuhizi haki sawa. Weka tuweke! 🙌🏽

Being Goalkeeper ni mambo za kizamani hizo.
Mwanaume kusubiri pesa ya mke wako mwisho wa mwezi mpige mahesabu ni UMAMA.

Ndiyo maana heshima inapungua now days pesa yake ni yake na yako ni yenu wote .

Hammer that inside your psyche.
 
N ushaur mzr lkn usjisahau, jiwekee akiba. Mara nying wababa wakizeeka huteseka zaid yetu wamama.

Me nitachukuliwa na watoto wakanitunze, ww utaachwa pekee ukiteseka(naongea maana nimeishuhudia mara nying kwny jamii niliyopo). Sjui n kwann lkn mara nying wanaume huishia kuzeeka wenyewe, mwsho kujifia wakiwa wamejichokea. Watt hutazama wamama tu bila kujal baba nae n mzazi.

Ili kuepuka hilo yapasa kujiwekea akiba itakayokuja kukutunza uzeeni, maana huwa inatia huzuni mnoo kuona wababa wakizeeka pekee huku wakikosa msaada wakat walismama ipasavyo kulea hao watoto.
 
Back
Top Bottom