Ushauri wa bure kwa viongozi wetu

Ushauri wa bure kwa viongozi wetu

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
621
Reaction score
1,284
Nadhani kuna haja kubwa kwa Mama kutafuta namna na mazingira kwa kadri itakavyowezekana ili aombe radhi kwa kauli tata aliyoitoa kupinga kauli za Mabalozi, Maaskofu(TEC), Vyombo na Taasisi mbalimbali za kimataifa, Wanasiasa, watu binafsi waliolaani utekaji, utesaji na mauaji ya watu Nchini.

Mimi naamini, ukishakosana na makundi hayo yote na kuwaambia wameota mikia ni kuwakosea kabisa heshima yao. For the sake of peace, nadhani angetafuta forum yoyote ile ili kuomba radhi.

Lakini kuomba radhi tu hakutoshi, la pekee ni kukomesha tatizo lenyewe la utekaji, utesaji na mauaji.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom