Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,823
- 27,695
1. Hapakuwa na umuhimu wowote kukamata Tundu Lissu na hizi forced disappearances za kina mdude, soka na wengine, hata Lisu angeongea namna gani, angechoka, hata chadema ingeenda kwenye uchaguzi na wewe, nakuhakikishia wasingeshida, ccm bado ilikuwa na watu wengi, ungeshida uchaguzi bila yote haya, though kuna majimbo kadhaa wangeshinda, jambo ambalo ni zuri kwa uongozi ili wakukosoe bungeni.
2. Safari zako zoote ulizokula kodi zetu kwenda kurekebisha uhusiano na wazungu, zimeambulia patupu, vitu vya kuvumiliana tu hivi vimekuchafua. magufuli alikuwa kama wewe, akaharibu, ndio maana ulivyoingia tu ukashauriwa na wanaokupenda uzunguke kurekebisha mahusiano na nchi zile, mahusiano yakarudi, nchi ikatengamaa, mzunguko wa pesa ukarudi, watanzania wakaanza kupata furaha waliyopoteza kwa miaka 5 ya jiwe. kwa kifupi, uchaguzi huu ungeshida bila yote haya.
3. Rais wa bunge la ulaya atakuja na ujumbe kwako, tafadhali, jifanya mjinga siku ipite, kubali kumwachia Lisu ili nchi itengamae na tusielekee kulee kwa magufuli ambako wananchi waliishi kwa shida sana, pesa mtaani ilifutika, hatutaki uturudishe kule.
4. Bado uharibifu haujafika mbali sana, bado unaweza kuelekeza vijana wako wawaachie vijana wanaotafutwa kama kina mdude na soka etc, LISU aachiwe huru aendelee na kampeni, atakutukana, ataongea wee lakini nakuhakikishia kwenye uchaguzi ataambulia tu wabunge, hawezi kuwa Rais, wewe utashinda urais. ukifanya hivyo, jina lako litapona, nchi yetu itapona.
5. Umegombana na viongozi wa dini hasa wakatoliki, na wakristo wote, ni muhimu uwasikilize, wewe umewekwa hapo na wananchi, haujawekwa hapo na makaratasi, ulipigiwa kura pamoja na jiwe ndio ukapata icho kiti, ni wananchi wamekuweka hapo, duniani kote watawala huwa hawashindani na wananchi, kwenye mambo ya msingi, huwa wanawasikiliza wananchi. hivi kweli mapadre na maaskofu wooote hao wawe hawana akili kwa wananchosema? kweli kanisa katoliki lote na makanisa mengine ambayo hayasemi ila chini kwa chini yananung'unika, wawe hawana akili na kwamba kila wananchosema sio cha kusikiliza?]
6. J.Kikwete akung'ate sikio, ukitaka kumshinda mpinzani, mwache abwekeee, wewe fanya matendo ya maendeleo, mdomo ameumbiwa mwanadamu, anao ndio maana anaongea, waache wapinzani waongee, wee tekeleza ilani, nakuhakikishia yote wasemayo wapinzani yatakuwa makapi tu. hakuna haja ya kuumizana.
7. Mimi ni mfanyabiashara na mwanasheria, kipindi cha jiwe, pesa zilivyoisha mtaani, wafanyabiashara wenzangu wengi sana walikufa. why? walikopa benki, mzunguko wa pesa ulivyokata kwa sababu jiwe alijifanya kuleta kibesi kwa wazungu, nyumba walizoweka rehani ziliuzwa, biashara zilikata, watu walikufa kwa pressure, PLEASE, bajeti ya nchi yetu haiwezi kutimia bila kutembeza bakuli, walinde hao wanaotuletea pesa, wafanyakazi wataumia na wafanyabiashara pia. tafadhali.
8. Mwisho, mimi sio mwanasisiemu, siwezi kuipigia kura sisiemu, though najua hata nisipokupigia utashinda, kwa sababu ukweli ni kwamba pamoja na kwamba kuna wapinzani lakini sio wengi kama wanaccm, hakuna haja kuumizana mama, wewe umejitangaza mtu wa dini, tunza jina lako na legacy yako ikumbukwe kwa mema.
Mungu akusaidie.