Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,832
- 114,340
Wanabodi,
Mimi ni miongoni mwa watu tuliomuunga mkono kwa dhati, mwamba wa Kaskazini, Edward Ngoyai Lowassa, na tukaahidi humu akiondolewa kwa mizengwe, hatuta kubali, patachimbika. Kilichotokea ni kweli Edward Lowassa aliondolewa kwa mizegwe. Kuna watu humu hawakuuona uzi huu, [h=3]Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC![/h]hivyo Lowassa alipokatwa walishangaa, kama wangeosoma uzi huu kabla, wasinge shangaa!.
Baada ya kuibuka jina John Pombe Magufuli, kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM, kuna watu wanadhani amejiibukia tuu from nowhere!, No!. Na kuna wanadhani ameibuka surprisingly!, no!. Kama wangeusoma uzi huu, [h=3]Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John[/h]angalau wangeelewa ni Magufuli!.
Kwa vile Lowassa ndie kipenzi cha watu, na wengi waliitegemea CCM itimize mapenzi ya watu, lakini CCM wakaamua kutanguliza mbele maslahi mapana zaidi ya taifa, kwa kuwaweke pembeni 'the giants', wengi wa wafuasi wa Lowassa wamekuwa take by surprise na wengine hata kuwa despaired, lakini laiti wangeusoma uzi huu, [h=3]Edward Lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe Rais wetu [/h]wasingekuwa surprized!.
Maadam sasa uchaguzi wa CCM umemalizika, na mgombea wa CCM ni Dr. John Pombe Magufuli, natoa wito na ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa, ayakubali matokeo, avunje kambi yake au ile team yake, ayarudishe nyumba majeshi yake na kujisalimisha rasmi kwenye chama kwa kumsupport mgombea rasmi wa CCM!.
Kama mgombea angekuwa ni Membe, tungependekeza mapambano yaendelee kwa Lowassa kuvuka upande wa pili, nasi tumuingize ikulu!, lakini huyu aliyepitishwa, John Pombe Magufuli, pia ni jembe la ukweli, hivyo Lowassa hata akiamua ku cross, ataishia kupata kipigo kingine, yaani double tragedy !.
Kwa vile Lowassa ni chaguo la watu, na ni sisi watu tulio mchagiza kuwa 2015, ikulu ni yake, kwa ahadi hata asiposimamishwa na CCM, then asimame nje ya CCM tumpeleke ikulu, lakini kwa vile alipita ni Magufuli, ambaye na yeye ni jembe la ukweli, hakuna tena sababu kwa Lowassa kuendeleza mapambano maana huu sasa utakuwa ni mpambano wa mafahali, ziumiazo zitakuwa ni nyika!.
Lowassa tulikupenda, ila CCM imempenda zaidi Magufuli, teremsha silaha chini, kubali kushindwa, rudisha nyuma majeshi, jisalimishe!.
NB: Hii sio mara ya kwanza kwa mimi kutoa ushauri wa bure kwa Lowassa, huko nyuma niliwahi kumshauri, [h=3]Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.[/h]matokeo yake tunayajua, na huu ni ushauri tuu.
Pasco
Maskini Mamvi....wajumbe woooote wanaimba na kucheza mkutanoni....washasahau zile chambichambi......sasa ule msemo wake wa kuhuzunika pamoja na kufurahi pamoja umekuwa kinyume kabisa...... anahuzunika peke yake wajumbe wanafurahi peke yao.....siasa hizi nouma kweli.....
....
....shujaa hupigana mpaka siku ya mwisho hamalolo Nkoi Pasco !!!
hakuna sensa tena magufuli akiwa rais anaweza kutuhesabu wenyewe