sangu mnene
Member
- Sep 5, 2012
- 92
- 35
Nimelazimika kuwaza tena suala la katiba pendekezwa baada ya Warioba kudai ataongea mchakato ukianza source Mwanainchi-27/12/2015. Sijui anachowaza Dr Mwakyembe, kama anataka kuandika katiba mpya kwa kuanzia pale ilipoishia kamati ya jaji Warioba ni vema na ni haki,aendelee kwa amani kabisa.Lakini kama anataka aendelee na katiba pendekezwa ya CCM,namshauri aachane nayo kabisa,ni bomu litakalowagawa watanzania.
Akumbuke kuwa katiba pendekezwa;
Nimkumbushe tu Dr Mwakyembe, watanzania hawachelewi kubadilika, Vita alivyovianzisha Dr Magufuli vinahitaji uungwaji mkono wa wananchi wote.Leo kila mtu anampenda rais. Lakini, kazi yote aliyofanya rais Dr Magufuli itaonekana si kitu, kama mchakato wa katiba iliyopitishwa kitapeli utaanza tena.Ukitaka umoja wa taifa hili uendelee kuwepo,na watu waendelee kuiunga mkono CCM basi rudisha rasimu ya Warioba,vinginevyo nakushauri achana kabisa na kufufua mchakato wa katiba.Kujaribu kuitetea katiba pendekezwa ni sawa na kuchezea moto karibu na petroli.ACHA,ACHA KABISA DR MWAKYEMBE KUTETEA KATIBA PENDEKEZWA,ACHA KAMA ULIVYOACHA KUNYONYA, hilo ni bomu kwa utawala mujaarabu wa Dr Magufuli,nakusihi achana na katiba pendekezwa rudi kwenye rasimu ya Warioba.Maneno yangu haya ni hakika,kweli na thabiti, ni suala la muda tu,akipuuzia matokeo tutayaona. Alamski!
Akumbuke kuwa katiba pendekezwa;
- Ilipingwa vikali na uongozi wa dini ya kiislamu, jambo hili liliwaunganisha waislamu wote
- Ilipingwa vikali na viongozi wa dini ya kikristo,jambo hili liliwaunganisha wakristo wote
- Katiba pendekezwa inapingwa na takriban wasomi wote
- Wafanyakazi waliipinga katiba pendekezwa waziwazi bila woga, hasa walimu
- Vyama vya upinzani karibu vyote viliikataa katiba pendekezwa,hata vile vilivyounga mkono baadaye viligeuka
- Wanafunzi wa vyuo na sekondari waliunga mkono rasimu ya Warioba
- Kukataliwa kwa rasimu ya Warioba kumepelekea CCM kuchukiwa sana Zanzibar
- CCM ilichukiwa sana bara, imani kwa CCM ililejea pale Polepole alipotangaza kuwa amehakikishiwa na Magufuli kwamba akiingia madarakani atairudisha rasimu ya Warioba
- NGO ziliipinga katiba pendekezwa waziwazi bila woga wala mawaa
- Waandishi wa habari waliweka tofauti zao kando na kuitetea rasimu ya Warioba kwa nguvu zote n.k