Mimi ni mpenzi wa CHAMA CHA MAPINDUZI lakini kwa hali inavyoonekana Chama kinaelekea shimoni kwa ajili ya mpasuko unaonekana hivi sasa. Lowassa atakapoamua kurudisha kadi kwa kweli atahama na watu wengi sana na usishangae hata Wenyeviti wa Chama chetu wengi watamfuata. Ushauri wangu ni kuwa Lowassa aitwe kiungwana na Chama chetu na kumwomba RADHI kwa yote yaliyotokea kwenye mchujo wa mgombea Urais na kwenye kikao hicho wawepo Wazee kama Mhe. Mzee Mwinyi, Mhe. Mzee Malecela na Mhe. Mzee Mkapa. Ichukuliwe kwamba kuomba radhi siyo kujishusha ila ni jambo la kiungwana.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.