Viongozi na wapenzi wa Chadema. Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu mwelekeo wa siasa nchini na nimejaribu sana kufanya utafiti usio rasmi. Nilitaka kufahamu watu wanaounga mkono CCM wanafanya hivyo kwa misingi gani na wanaounga mkono Chadema wanasukumwa na nini na pia kutaka kufahamu wanaopinga wanapinga kwa nini.
Nilichogundua ni kwamba wanaoipenda CCM wanafanya hivyo kwa sababu ya mazoea na pia kwa sababu ya kukwamisha Chadema, ni wachache mno wanaounga mkono CCM wanafanya hivyo kwa ajili ya sera ama utendaji.
Kwa upande wa Chadema, watu wengi wanaounga mkono Chadema wanaona chama hiki ni chama cha kumkomboa Mtanzania kutokana na dhuluma na ufisadi wa CCM, ni chama kinachowapa wananchi matumaini. Halikadhalika nimegundua kwamba waislamu wenzangu wengi wanakiona Chadema si tu kama chama cha kikristu bali pia ni cha kibaguzi na ni hatari kubwa sana kwa Waislamu. Mtazamo huu haupo miongoni mwa watanzania wenye elimu ya wastani ama pato la wastani bali hata wasomi wenye title ya udaktari wana mtazamo huohuo na watu wenye uwezo. Kwa kweli mimi nimekipenda sana chama hiki kutokana na sera zake na pia msimamo wake thabiti dhidi ya dhuluma katika jamii na pia nawapenda sana waislamu wenzagu na ningependa kuona Chadema kinakubalika kama chama cha waislamu vilevile.
Huenda watu wakanibeza na kudai naleta hoja za kidini lakini napenda kuwakumbusha Chadema kwamba bila ya Islamic vote Chadema haiwezi kufurukuta katika uchaguzi ujao. Pia ninaona Chadema inafanya makosa mengi kuhalalisha lack of confidence from Muslims, mfano sijawasikia hata mukitoa mkono wa Ramadhan ama Eid lakini uhuru wa South Sudan mulitoa pongezi kwa haraka sana. Mambo kama hayo yananipa mimi na waislamu tunaowaunga mkono shida sana kuwashawishi wenzetu kwamba Chadema ni mkombozi wa wote na Chadema haina ubaguzi.
Ninachoshauri sasa Chadema ijenge mkakati maalumu wenye lengo la kupata support ya Waislamu, ikibidi hata mulete mjadala kati ya Chadema na waislamu ili waislamu wafahamu msimamo wenu juu ya mambo muhimu kwa waislamu. Chadema haiwezi kupata kura za waislamu kutokana na sera tu ama kampeni za uchaguzi, acceptance must begin now. Waumini wenzangu wanaomba mpaka dua musiingie madarakani. Haya yote yanaweza kubadilika na mukawa munaombewa dua muingie madarakani kama mutafanya kazi nzuri ya kukubalika. Hata nchi zilizoendelea swala la dini ni nyeti na ndio maana dini za viongozi huwa zinajadiliwa, tafadhalini sana musi underestimate ushauri wangu.Ninawashauri Chadema kwa kuwa nina imani nacho na pia ningependa kuona ndugu zangu na waumini wenzangu wa Kiislamu wanajiunga na Chadema kwa wingi.
Asanteni
Huenda watu wakanibeza na kudai naleta hoja za kidini lakini napenda kuwakumbusha Chadema kwamba bila ya Islamic vote Chadema haiwezi kufurukuta katika uchaguzi ujao. Pia ninaona Chadema inafanya makosa mengi kuhalalisha lack of confidence from Muslims, mfano sijawasikia hata mukitoa mkono wa Ramadhan ama Eid lakini uhuru wa South Sudan mulitoa pongezi kwa haraka sana. Mambo kama hayo yananipa mimi na waislamu tunaowaunga mkono shida sana kuwashawishi wenzetu kwamba Chadema ni mkombozi wa wote na Chadema haina ubaguzi.
Asanteni
Hapo kwenye red ndipo ulipo boronga. Kwamba CDM haiwezi kukwea hadi madarakani bila kura za Waislamu! Kwa hiyo leo hii CCM ipo madarakani kwa sababu ya kura za Waislamu. Kasome vizuri Statistics za Tanzania ndugu yangu..
Demographics ziko wazi na zinaonesha kwamba chama chochote ambacho kitasusiwa na Waislamu ama Waristu hakiwezi kutwaa dola. Siri moja kubwa ya CCM kushinda ni kuvutia dini zote.
Na mimi nishawahi kuwaza kama mleta mada. Natamani CCM watoke madarakani kwa kushindwa kwa kishindo ili wasipate mwanya wa kuchakachua na ndipo suala la kutegemea kura za waislamu linapojitokeza. Lakini baada ya kuwaza sana hasa katika kufikiria ni mkakati gani chadema wanaweza kuutumia kupenya kwenye ngome za waislamu nikagundua pengine si muhimu sana kwa Chadema kuhofia jambo hili la kufanya jitihada za makusudi kuvutia kura za waislam au kutamani sana kwenda ikulu. Kama watanzania walio wengi (wakiwemo waislamu) hawataipigia kura chadema eti kwa sababu fulani fulani za kidini au kikabila badala ya kuangalia hoja na sera basi huo hautakuwa udhaifu wa Chadema bali wa wapiga kura wenyewe. Na kinachoifanya Tanzania iendelee kuwa na umaskini, ujinga na maradhi, ni kwa sababu wapiga kura wengi ni maskini, wajinga na wagonjwa kiasi cha kushindwa kuchagua chama sahihi. Sasa hapa tusitegemee miujiza. Mpaka pale watu watakapoanza kupambanua kwamba dini zetu hazitusaidii kupambana na ufisadi, ujinga wala maradhi, na makabila yetu hayatusaidii, na kwamba tusitumie vigezo hivi katika kuchagua chama au mgombea.....basi hapo ndipo tutakapokwamuka kama watz, waislam, wakristo, pamoja na makabila yetu.