Ushauri wa bure kwa ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAKUNDA, Apr 21, 2012.

 1. M

  MAKUNDA Senior Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna asiyejua kuwa CCM imekuwa ikiingiza mkono wake katika maamuzi ya mahakama hasa katika kesi za kupinga matokeo ya Ubunge. Sasa ushauri ninaotaka kuwapa ni kuwa ni bora mwingilie kwa kuomba kila mlikopinga matokeo mshindwe kesi ili kuhepuka uchaguzi mdogo. Hata kule Arusha muombe rufaa ya CDM ipite na Kamanda G.L aendelee na ubunge wake. Kwanini natoa ushauri huu?
  Ukweli ni kuwa kila uchaguzi mdogo utakaofanyika CCM itashindwa tu na huu ni ukweli usiopingika. Na katika trend ya kushindwa katika chaguzi ndogo mjue ndiyo Chama kitazidi kuporomoka na kujenga mazingira ya kushindwa 2015. Someni alama za nyakati na kutumia busara ndogo. Hii haiitaji shule kutambua. Makamanda wako juu kila mtakapoweka mguu ni mweleka. Mimi siyo mtabiri wa nyota bali busara ya kawaida inanionyesha hivyo.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Broda MAKUNDA,
  Sikio la kufa halisikii dawa!
  Ni mpango wa Mungu kuwa ccm ife kwa mtindo huo wa ubishi, na watafitiniana bila kugundua kitu, hatimaye tutapita kuitazama CCm sura ya mwisho pale Dodoma kaburini, tutatupia udongo wa kwaheri!
  Regime mpya itaanza!
  Hadithi mwisho!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  ungem-mention yule kiongozi aliyepo jf ili apate ujumbe.
   
Loading...