Ushauri wa biashara ya kubeba abiria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa biashara ya kubeba abiria

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Parachichi, May 11, 2010.

 1. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu habari za shughuli!

  Mimi ni mjasiriamali!nilibahatika kuchukua ka mkopo nikanunua gari aina ya Coaster ila kwa sasa inafanya kazi ya kukodisha kama Tours! nilikua nafikiria kuibalisha na kuwa ya kubeba abiria kama vile daladala ila sitaki iwe daladala manake huwa gari inachoka vibaya mno ukijumuisha na foleni za hapa dar ni kuumizana kichwa tuu.

  Najua hapa JF kuna wajasiriamali wenzangu ambao nao pia wapo kwenye hiyo biashara naomba ushauri je nichukue njia ipi yenye abiria?

  Nawasilisha wakuu
   
 2. d

  dullymo Senior Member

  #2
  May 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa kweli kila sehemu kuna msongamanano na abiria ni wengi but njia yenye afadhali kidogo kwa muono wangu ni masaki - posta.
  nadhani daladala zote za njia hiyo sidhani kama zinafika hata 10. sehemu itakayokucheewesha ni foleni ya salenda tu ila ukishaivuka ni mwendo mpeto hadi ukirudi. abiria ni wengi mida ya asubuhi na jioni ila mchana abiria wachache. kazi mwisho ni saa 1 baada ya hapo kama hesabu haijatimia driver atajua mwenyewe kama aibe rout ya masaki - morocco au vipi. nadhani itasaidia kdg
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Bora uiache kwenye tours huko huko ukienda kwenye daladala mzee kichwa kinaweza pasuka utafukuza kila dereva mara akwambie amepigwa bao mara gari iliharibika alafu mwisho wa siku ukitaka kuuza utauza kwa bei ya mbuzi maana gari itakuwa imechoka ukilinganisha na hizo za tours huwa zinadunda safi na bodi halichoki mapema kama daladala.
   
 4. Mrbwire

  Mrbwire Senior Member

  #4
  May 11, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 197
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35

  Sio kwamba hazifiki 10! njia ya masaki posta ina daladala mbili tuu. na moja kati ya hizo yupo kwenye kuihamisha ipige posta-mwenge. Katika njia isiyo na maana bongo hii ni hiyo (Masaki - Posta) Abiria ni wachache sana na wakipanda hakuna kushuka. USITHUBUTU kuipeleka masaki-posta.

  Nashauri uiache kwenye tours mzee.
   
 5. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ndugu yangu mbona naona kama sijakuelewa-angalia nilipo bold. Yote yanawezekana ila kusudi nikutafutie ushauri,hapo TZ inabidi kila bizz uifanyie research na inputs zake ki tz tz na mara nyingi huanzia na 1)umri wako 2)ungetaka mapato kiasi gani/siku 3)wadhifa wako-kijamii 4)una bizz nyingine au?ndio hiyo hiyo 5) je iko mkoa gani hapo TZ 6)mkopo umemaliza 7) Ni lini unatakiwa kutoa uamuzi. Ukinijibu hayo nitakueleza uzoefu wangu na labda kwa hints tu, unaweza kuwa mtu wa heshima huwezi kupigana na madereva na makondakta wa dala 2,kama ni mzee i.e una afya mbaya ni bora ukaiuza tu,maana utakufa na magonjwa ya moyo na stress kama unataka mapato makubwa ili umalizie haraka deni hapo kazi itakuwa ngumu zaidi kama iko nje ya DSM hapo mambo ni magumu zaidi. Nipe inputs nikupe mchango wangu,maana mimi niliziuza kwa 15% ya gharama kunusuru afya yangu!
  :painkiller:
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Kwa ujumla ni heri ununue PUNDA na kufuga kuliko kununua gari la biashara TZ hii.Uza fanya biashara ingine!
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Unataka kuifanya daladala lakini hutaki iwe daladala kipi ni kipi?
   
 8. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2010
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu nimewasoma!nashukuru sana kwa waliosaidia kujibu!yaani namaanisha nataka iwe ya kubeba abiria labda kwa mfano kutoka dar kwenda morogoro,au kutoka dar kwenda Tanga n.k.nilikua namaanisha hivyo wakuu manake kufanya ipige route za hapa dar utakufa na stress kabla ya mda si wako. Kuhusu huyu bwana Katabazi hapo juu ni kuwa kwa sasa naishi Dar Es Salaam na mkopo umebakia kidogo sana ambao naweza kumalizia kuulipa kwa biashara zingine tuu sio lazima nitegemeee hiyo gari.

  Pili kuhusu mapato kwa ujumla wake hata kwa hivi sasa tunavyofanya za kukodisha kama tour ni kuwa at least kwa siku gari inatakiwa ilaze 80,000 ukikosa sana 70,000 baada ya kutoa operating expenses like posho ya dereva na mafuta kama utapata kazi ya kilometa isiozidi 1200 yaani 600 kwenda na 600 kurudi,kama kilometa zitazidi hapo inakuwa ni kati ya 150,000-200,000 per day.

  Sasa nije why nataka kuachana na tours. Huku bongo bizz ni ngumu sana,madalali wameharibu kazi,mtu anakuja anataka kulalia kwa vile anajua kuwa gari haina kazi, kwa hiyo ukitaka hela nzuri ndio hivo unakata miezi hujapata kazi.Kwa mfano kwa ujio huu wa WEF(World Economic Forum) kilikua ni kipindi kizuri sana cha mapato,sasa jamaa waliokamata kazi wanakodisha gari kwa Tshs 150,000,dalali anashika kazi anakupiga na 80,000 per day mafuta ni juu yako. ni biashara kichaa ni bora uwe unajua wazi kuwa gari ina route ya Dar- Tanga kwa mfano mnapakia vichwa vyenu hesabu inaingia.

  Ndio hivo wakuu nilikua naomba ushauri wenu.
   
 9. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani nilivyokusoma hii biashara kwako itakuwa ngumu,nadhani unajua kuwa ukianza routes za kwenda nje ya DSM inabidi uanze utaratibu mpya wa TLB etc,na wenye nguvu wasioogopa pressure hizo kazi wanazifanya bila hivyo vibali i.e wanajua jinsi ya kupambana na wahusika.
  Hapo sasa linakuja tatizo kubwa ambalo hata kama ungetaka vipi kama huna MTU MWAMINIFU basi kila siku gari litafanya kazi za wengine trust me kwa kuambiwa gari liko Morogoro unaweza kukuta liko Rufiji linabeba maiti wewe si utataka hesabu?
  Madalali usiwalaumu ndg yangu,wamewekwa na system and you cant avoid them. Ndio maana kama kiukweli kufanya biashara hii kama huwezi kuhimili stress na kupambana na madalali ni ngumu sana kwa sababu hamna njia ya moja kwa moja.
  Kama una mtu wa kukusaidia kupata shule yenye uwezo wa kulikodi gari kwa ajili ya kuchukua na kuwarudisha nyumbani itakuwa vyema, kwa sababu kama shule haina uroho-shule zinalipisha 45,000/month/student i.e around 24 days na kama unabeba wanafunzi 40 wakikupa 1.6M/month nadhani na hizo siku zingine ukapambana na madali kwa ajili ya harusi na vitu vingine kwenye weekend utarudi kwenye hiyo 70K/month lakini gari yako itakuwa haiumii.Na upane mwing.hizo KM ni nyingi kwenye tours na madereva hujui huwa wanaifanyia nn gari wakipata mwanya.
  K.
   
 10. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  ndugu,
  peleka gari dar tanga,ila weka GPS tracker ikusaidie kujua liko wapi,coaster ukifanya daladala utaharibu gari within a very short time,DAR daladala za uhakika ni DCM,aka GOBOLE ,haya ni magumu,na likigongwa unatoa bati na kupachika bati,kama 109 landrover.

  school bus,itabidi usajili kama school bus,hivyo uwezi kufanyia biashara nyingine after school hrs.
   
Loading...