Tuyuku
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 3,292
- 1,923
Salamu kwenu.
Kwa muda kidogo nimebahatika kuwa katika recruitment ya staff ndani ya organization yetu. Mara nyingi nimekutana na maombi ya kazi ambayo yanaonesha kabisa mwombaji kutokuwa serious na kitu anachokifanya. Unakuta tangazo la kazi limesema kabisa nini na nini kinatakiwa kuwemo katika maombi hayo, lakini bado utakuta mtu anapuuzia mahitaji hayo.
Unapotuma maombi ya kazi, unapaswa kuzingatia kuwa, maombi hayo yanatakiwa kumshawishi mtangazaji wa nafasi hiyo kuwa unastahili kuwa shortlisted na kuitwa kwenye usaili.
Hilo moja. Kituko kingine nimekiona leo. Miezi miwili nyuma, kuna dada alikuja ofisini kwetu kuomba nafasi ya kazi. Kwa wakati huo, hatukuwa na nafasi wazi. Akatuuliza lini tunaweza kuwa nayo? Nikamjibu kuwa, katika kipindi cha miezi miwili tunategemea kufanya recruitment. Nikamwambia aache namba ya simu ili nafasi ikitokea tuweze kumwarifu. Mara kadhaa aliwahi kunipigia simu kuniuliza kama tayari, nikamjibu mara zote kuwa bado. Kwamba, pindi itakapokuwa tayari nitamwarifu. Nilihitaji kumwarifu kwa sababu; 1. Anavyo vigezo kitaaluma, 2. Alionesha nia hasa ya kufanya kazi nasi.
Leo asubuhi, tumetangaza nafasi ya kazi. Nikamkumbuka. Nikaona uungwana ni kumpigia simu kuwa aombe hiyo nafasi. Nimempigia simu. Kwanza amenijibu kwa nyodo sana (pengine alijua nataka kumtongoza). Nikamsikiliza. Nikamwuliza unaifahamu organization fulani? Akanijibu, "Kama naifahamu wewe unatakaje?"
Nikamwambia, "Unaongea na fulani pengine huna namba yangu."
Akanijibu, "Ndiyo ninajua ninaongea na wewe. Unatakaje kwani?"
Nikaona huyu anaonesha hana staha. Nikamwambia ahsante ninaomba nikutakie siku njema. Akaniuliza nimempigia ili iweje? Nikaona udhia kuendelea kujibizana naye. Nikakata simu.
Baadaye kidogo ananitext, "Samahani nilikuwa na boyfriend wangu nikashindwa kuongea kwa uhuru. Niambie basi."
Nimeamua kumpuuzia.