Ushauri unahitajika

TihZ

Senior Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
158
Reaction score
26
Kuna baba fulani hapa mtaani kwetu ana tabia ya kumtaka kila binti atakayemtamani na kibaya zaidi kuna tetesi za chinichini kuwa ni muathirika.Tabia yake imezidi sasa kwani nimegundua ana mahusiano na ndugu yangu ambaye ni mgeni na huu mtaa,baada ya kugundua hilo nikamfuata ndugu yangu na kumshauri aachane naye kwani kuna habari za chini chini kuwa sio mzima kiafya na akanijibu nisijali atajua cha kufanya ila cha ajabu licha ya kumtahadharisha na kumshauri hivyo lakini nimegundua kuwa bado wana mahusiano na jamaa baada ya kuona message za huyu jamaa katika simu ya huyu mdada.Huyo jamaa anatumia fedha kuwahadaa mabinti za watu cha ajabu alishawahi kusemwa na mdada fulani baada ya mdogo wake kutongozwa.Je hivi ni kipi hasa kinawafanya watu wa namna hii kufanya uchafu kama juu?
 
Muandalieni msuto wa gea habib

Ameoa? Mshirikisheni mkewe

Ni tabia mbaya ya mtu tu...
 
Mrudishe nduguyo alikotoka unless itakuwa majuto ni mjukuu!
 

Hapa unataka ushauri au maoni? BTW sikio la kufa halisikii dawa ndo maana unaona tuna serikali mbovu na chama change kichovu lakini bado tumo tuu!!! 'Manabii' wanakuwa na maskendo ya kutisha lakini lakini bado watu hawasikii la muadhini wala mnadi swala
 
Mrudishe nduguyo alikotoka unless itakuwa majuto ni mjukuu!

unadhan kumrudisha ndo suluhu? mtu akipania jambo na hizi simu,mbna anamfata had huko ulipomrudisha
 
Ndugu yako labda nae kaathirika..Huwezi jua
 
Anawahadaa mabinti.....hiyo kazi waachie mabinti wenyewe wataamua. Kwani anawabaka?
 
wote waathirika wawache wale raha zao
 
ushauri ulisha mpa so wa kutoka kwetu wa nn tena?
 
Kwakuwa umemtaadharisha ndugu yako, yakimkuta atajua mwenyewe.

Acha dunia imuoneshe, akiukwaa mrudishe kijijini akafie huko.
 
Huyo nduguyo naye kimeo ana test moto kwa ulimi kwanini usimuunguze!
 
tatizo ni pesa
hatufikirii mbele mawazo yetu yanaishia leo na si kesho.
wadada wengi wa mjini wanapenda pesa so ni vigumu kuamin mpaka hajisikie anaumwa
"nitajua nimeshiba kama tumbo limejaa"
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…