Ushauri unahitajika kwa huyu Kaka tafadhali

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kuna mkaka alioa mwanamke miaka kadhaa iliyopita,na katika maisha yao ya ndoa walibahatika kuzaa watoto wawili,wa kike na kiume,wakiwa wanaishi Dar kipindi hicho

Bahati mbaya ndoa ikavurugika,mwanamke akakimbia kwenda kusikojulikana ila akawaacha watoto kwa baba yao

Baadae huyo mkaka akahamia Mwanza kikazi na ndo nyumbani kwao

Siku za hivi karibu alipigiwa sim na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ambayo ipo huko ukweni, musoma

Akataka kujua kuna nini,lakini huyo mwalimu alimwambia wewe njoo mara moja hapa shuleni

Basi kaka akaona ngoja afikepo,akaandaa safari akamuaga mke wake ambaye alioa baadae akaenda musoma kwa mwalimu mkuu huyo

Kufika pale mwalimu mkuu wa shule akawaita watoto kama watatu hivi,wa kiume wawili na wa kike mmoja,mwalimu akaanza kumuuliza yule mkaka" Wewe ndo William Dotto? William akajibu" Ndiyo ndo Mimi" Mwalimu akaendelea" Sasa hawa watoto wako,Juma William Dotto,Deborah William Dotto na Jonas William Dotto mbona wana maisha ya ovyo sana,viatu hawana,nguo za shule ni shida,mahudhurio ni mabovu"

William alishangaa kuambiwa watoto hao ni wake,akamuuliza mwalimu " Hawa watoto ni wangu kiaje labda mbona sielewi?

Mwalimu akawambia wale watoto watoke nje maana akawa ameelewa kuwa hapa kuna kitu ,ndipo mwalimu akamwambia,"Mzee nashangaa kuwa na wewe huwafahamu hawa watoto,kwanza walihamia hapa kwa uhamisho kutoka Iringa,mama yao aliwaleta hapa wakiwa na majina hayo ambayo ni ya baba yao ambaye ni wewe,basi tukawapokea,na vyeti vyao vya kuzaliwa jina la baba yao ni William Dotto sasa hatujui nini kinaendelea"

Ndipo William akaamua kumuweka mwalimu wazi,kuwa waliachana na huyo mwanamke ,watoto aliomwachia anaishi nao mwanza,sasa huyo mama alikoenda kutembea akazaa watoto wengine na kuwapachika majina yangu lakini si wanangu hao

Nini cha kumshauri William ? Tangu waachane na mke wake wa kwanza hakumpa talaka kwa kuhofia kupoteza assets zake,pia anaambiwa aajibike kuwatunza watoto ambao si wake ila nyaraka za serikali wanatambuliwa kuwa ni wake

Watoto wa kiume wanasoma Darasa la tano na wa kike la tatu

Majina si sahihi kuficha hadhi ya mtu
 
Dah! Jamaa aangalie uwezo wake Kama ataweza awasaidie akishindwa akae kando asomeshe wanae halali wasijeharibikiwa.. huyo mke wa kwanza atampa stress tu ila Kama anaweza msaidia na amsaidie ila kwa akili.
 
Watoto hawana makosa...kama ana uwezo wa kuwanunulia hata sare basi anunue
 
Dah! Jamaa aangalie uwezo wake Kama ataweza awasaidie akishindwa akae kando asomeshe wanae halali wasijeharibikiwa.. huyo mke wa kwanza atampa stress tu ila Kama anaweza msaidia na amsaidie ila kwa akili.
Je majina ya watoto yaendelee kuwa hivyo au
 
Uwezekano ata kama ana uwezo huwezi kutoa msaada wa moja kwa moja kwa MTU ambaye kwanza hujui uhalisia wao labda aache pesa kidogo atembee zake ata kisheria hakuna cha kumfunga apo

Hakuna haja ya hayo majina kuwa hivyo Kama watoto si wake.

Itakuwa vyema kama ataonana na huyo aliendikisha hayo majina na atete nae ajue namna ya kumsaidia ila awe na tahadhari Sana.
 
Jamaa kama ana uwezo amchukue hata mtoto mmoja, ila hao wengine wawili awasaidie hata kwa kuwanunulia sare za shule na vifaa vingine,Mungu atamlipa.
 
Majina siku zote yanafanana kaka ukilichimba tatizo utajikuta unapata yakukupata
Hakuna haja ya hayo majina kuwa hivyo Kama watoto si wake.

Itakuwa vyema kama ataonana na huyo aliendikisha hayo majina na atete nae ajue namna ya kumsaidia ila awe na tahadhari Sana.
 
Uyo mwanamke ni chizi ye uyo baba si anawatoto wake? Jina sio tatizo kwani ye ndo william dotto peke ake nchini, aende kwa hao watoto wanapokaa aeleze msaada atumie ubinadamu tu,
 
Kuna mkaka alioa mwanamke miaka kadhaa iliyopita,na katika maisha yao ya ndoa walibahatika kuzaa watoto wawili,wa kike na kiume,wakiwa wanaishi Dar kipindi hicho

Bahati mbaya ndoa ikavurugika,mwanamke akakimbia kwenda kusikojulikana ila akawaacha watoto kwa baba yao

Baadae huyo mkaka akahamia Mwanza kikazi na ndo nyumbani kwao

Siku za hivi karibu alipigiwa sim na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ambayo ipo huko ukweni, musoma

Akataka kujua kuna nini,lakini huyo mwalimu alimwambia wewe njoo mara moja hapa shuleni

Basi kaka akaona ngoja afikepo,akaandaa safari akamuaga mke wake ambaye alioa baadae akaenda musoma kwa mwalimu mkuu huyo

Kufika pale mwalimu mkuu wa shule akawaita watoto kama watatu hivi,wa kiume wawili na wa kike mmoja,mwalimu akaanza kumuuliza yule mkaka" Wewe ndo William Dotto? William akajibu" Ndiyo ndo Mimi" Mwalimu akaendelea" Sasa hawa watoto wako,Juma William Dotto,Deborah William Dotto na Jonas William Dotto mbona wana maisha ya ovyo sana,viatu hawana,nguo za shule ni shida,mahudhurio ni mabovu"

William alishangaa kuambiwa watoto hao ni wake,akamuuliza mwalimu " Hawa watoto ni wangu kiaje labda mbona sielewi?

Mwalimu akawambia wale watoto watoke nje maana akawa ameelewa kuwa hapa kuna kitu ,ndipo mwalimu akamwambia,"Mzee nashangaa kuwa na wewe huwafahamu hawa watoto,kwanza walihamia hapa kwa uhamisho kutoka Iringa,mama yao aliwaleta hapa wakiwa na majina hayo ambayo ni ya baba yao ambaye ni wewe,basi tukawapokea,na vyeti vyao vya kuzaliwa jina la baba yao ni William Dotto sasa hatujui nini kinaendelea"

Ndipo William akaamua kumuweka mwalimu wazi,kuwa waliachana na huyo mwanamke ,watoto aliomwachia anaishi nao mwanza,sasa huyo mama alikoenda kutembea akazaa watoto wengine na kuwapachika majina yangu lakini si wanangu hao

Nini cha kumshauri William ? Tangu waachane na mke wake wa kwanza hakumpa talaka kwa kuhofia kupoteza assets zake,pia anaambiwa aajibike kuwatunza watoto ambao si wake ila nyaraka za serikali wanatambuliwa kuwa ni wake

Watoto wa kiume wanasoma Darasa la tano na wa kike la tatu

Majina si sahihi kuficha hadhi ya mtu
wewe na story zako wote hamna mvuto tena .
 
Back
Top Bottom