Ushauri unahitajika hapa

Ushauri unahitajika hapa

Kwa msisi yetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
811
Reaction score
1,387
Habari Wanabodi,

Naomba ushauri, kuna mdogo wangu yeye ni Mwalimu wa Sekondari alimaliza Chuo Kikuu SAUT mwaka 2014 na kuajiriwa Serikalini mwaka uliofuata 2015, alichukua Education Masomo ni Economics & Geography.

Mwaka kesho amepanga kwenda kusoma Shahada ya Pili, akanifata kuniomba ushauri akasomee nini ikizingawa kuwa yeye tayari ni mwajiriwa-mwalimu.

Kwa kweli imeniwia vigumu sana kumshauri huyu dogo nini akasome,kuna wakati nilifikiri aachane kabisa na ualimu kwa maana ya atose kabisa kuchukua kozi ya Education tena nikajihisi nitamshauri vibaya. Kwa kuwa JF ina wataalamu mbalimbali ni matarajio yangu kuwa mawazo mazuri yatapatikana.

Kwa vile alivyojichanga anatamani kwenda nje ya nchi angalau ndani ya EA Community ,University of Nairobi au Makerere University.

Karibuni kwa mawazo.
 
Niliwahi sikia Nacte hawaruhusu watu wa afya na elimu kubadili kozi, sina uhakika kwa hili wacha tusubiri wataalam
 
Yaani mtu msomi mwenye shahada ya kwanza na ajira juu tayari bado hajui anataka kufanya nini maishani mwake mpaka uje kumuombea ushauri humu?
Dah mawazo ya wabongo ni shida,unachopaswa kuelewa ni kwamba hakuna mkamilifu hapa duniani,kuomba ushauri kwa watu siyo ujinga ujue, ni mara ngapi tunashuhudia maprof na ma dr wakifanya mambao ya kipuuzi kabisa, hao siyo wasomi? Kuwa msomi haikuondolei sifa ya binadamu dhaifu ukaanza kudharau watu,tombana onyanda 😂😂😂
 
Naomba ushauri, kuna mdogo wangu yeye ni Mwalimu wa Sekondari alimaliza Chuo Kikuu SAUT mwaka 2014 na kuajiriwa Serikalini mwaka uliofuata 2015, alichukua Education Masomo ni Economics & Geography.

Mwaka kesho amepanga kwenda kusoma Shahada ya Pili, akanifata kuniomba ushauri akasomee nini ikizingawa kuwa yeye tayari ni mwajiriwa-mwalimu.
Sioni shida iko wapi. Geography na Economics ni teaching subjects zake. Tayari ana degree ya ualimu, sasa kama anataka kulala mbele na Economics au Geography bado atakuwa kwenye line yake na hapo ndipo kwa kutokea. Hivyo anaweza akafanya Master of Arts or Science in Economics au Geography (sioni kwa nini wizara ilete shida). Akifanikiwa anarudi kufundisha na nafasi ikipatikana nje ya teaching ikibidi afanye maamuzi magumu anafanya.
 
Aje Makerere mkuu nimpokee, shida ni kwamba as long as ameajiriwa kama mwalimu, akienda soma kitu nje ya ualimu watamsumbua kazini mana mara nyingi hawaruhusu, inaweza pelekea akisitishiwa mshahara! Ila kama hilo c ttzo, agonge masters ya uchumi tu mkuu

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Makerere kukoje? Accommodation vipi kuna hostel palepale chuoni? Vipi suala la application si hadi afike chuoni? Au kuna application online? Atalipiaje fomu?
 
Kwani Kozi za Education zikoje wakuu? Au ni kozi gani nzuri ya Education?
 
Mkuu Makerere kukoje? Accommodation vipi kuna hostel palepale chuoni? Vipi suala la application si hadi afike chuoni? Au kuna application online? Atalipiaje fomu?
Hapana mkuu, application unaingia web ya chuo...rooms ndani na out of campus zakumwaga, mkaribishe mkuu hatajutia

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom