Ushauri: UKAWA wasisimamishe mgombea wa Uspika, hawatashinda

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,494
Reaction score
62,000
Spika huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wabunge wote, na ili uwe Spika lazima uwashinde wapinzani wako kwa idadi ya kura.

Kuna misemo ya kizungu inayosema "numbers don't lie", "if you can't fight them join them" na "divide and rule", misemo hii ina maana yake.

November 2010, ulifanyika uchaguzi wa Spika, CCM walimsimamisha Anne Makinda na upande wa upinzani walimsimamisha Mabere Marando kutoka CHADEMA.

Wakati huo kama zikosei CCM ilikuwa na idadi ya wabunge jumla - 252, Chadema - 45, CUF - 43, NCCR - 4 wakati UDP na TLP mmoja kila chama.

Baada ya uchaguzi Makinda alishinda kwa kupata kura 265 na Marando alipata kura 53.

Ukiangalia, Makinda alipata kura zaidi ya idadi ya kura zote za wabunge wa CCM, Marando alipata 53 mchanganuo ulikuwa 43 CHADEMA, 4 NCCR, na baadhi (nafikiri) kutoka CCM. Ukiangalia Makinda alipata kura 13 kutoka ama CUF au TLP au UDP.

Ni wazi Marando asingepata kura kutoka CUF kwa vile kama utakumbuka ilikuwa ni wakati wa vita vya kambi rasmi ya upinzani.

Mwaka huu 2015, idadi ya wabunge wote ni 396 yaani 264 wa majimbo ni, 113 viti maalumu, 10 wa rais, 5 kutoka baraza la wawakilishi na 1 AG.

CCM INA jumla ya wabunge 246 huku UKAWA wakiwa na 117 tu. Kama CCM wakiweka mgombea wao na UKAWA wakiweka mgombea wao bado CCM wana uhakika wa mgombea wao kushinda.

Nashauri UKAWA wasipoteze muda na mali kusimamisha mgombea kwa vile HAWATASHINDA, badala yake wamuunge mkono mmoja wa wagombea wa CCM watakayeona anaweza kulinda maslahi ya taifa na ya umoja wao.

UHALISIA:

Najua wabunge wote 396 hawatakuwepo siku hiyo, ondoa wawakilishi 5 toka Zanzibar, 8 majimbo ambayo hayakufanya uchaguzi, na sidhani kama rais atakuwa tayari ameshateua wabunge wake 10. Kwa hiyo bila kujali watakaokuwa na udhuru mbalimbali, wapiga kura (wabunge) hawatozidi 396 - 5 - 8 - 10 = 373.

Kwa hiyo kama wabunge 373 watapiga kura, ili mtu awe Spika kundi lake lazima lipate siyo pungufu ya kura 187.

UKAWA wana kura 117 jumla wanahitaji lobbying ya kura 70 toka CCM.

Watazipata?
 
CCM ndo wanaamua nani awe spika hao UKAWA ni wasindikizaji tu.
 
Spika huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wabunge wote, na ili uwe Spika lazima uwashinde wapinzania wako kwa idadi ya kura.

Kuna misemo ya kizungu inayosema "numbers don't lie", "if you can't fight them join them" na "divide and rule", misemo hii ina maana yake.

November 2010, ulifanyika uchaguzi wa Spika, CCM walimsimamisha Anne Makinda na upande wa upinzani walimsimamisha Mabere Marando kutoka Chadema.

Wakati huo kama zikosei CCM ilikuwa na idadi ya wabunge jumla - 252, Chadema - 45, CUF - 43, NCCR - 4 wakati UDP na TLP mmoja kila chama.

Baada ya uchaguzi Makinda alishinda kwa kupata kura 265 na Marando alipata kura 53.

Ukiangalia, Makinda alipata kura zai

Hesabu zako zipo sahihi lakini kuna kitu hujakigundua na hujakiweka.Nimekuwa tempted kukiweka na nikikiweka utabadilisha title yako hapo juu.Ila nao watashtuka sana
 
Kwenye demokrasia yeyote hata kama unajua unashindwa sio vibaya ukajaribu.

ACT walijua hawezi kushinda urais ila walisimamisha mgombea.
 
UKAWA watashirikiana na wabunge wa CCM waliokuwa wanamuunga mkono Ngoyai wakati yupo CCM kumuweka mtu wao awe mgombea uspika.
 
Hesabu zako zipo sahihi lakini kuna kitu hujakigundua na hujakiweka.Nimekuwa tempted kukiweka na nikikiweka utabadilisha title yako hapo juu.Ila nao watashtuka sana

Weka tufanye tallying
 
Hesabu zako zipo sahihi lakini kuna kitu hujakigundua na hujakiweka.Nimekuwa tempted kukiweka na nikikiweka utabadilisha title yako hapo juu.Ila nao watashtuka sana
Mkuu angalia nimeweka vizuri mahesabu, kuna watu waliingilia akaunti yangu nilikuwa nashindwa ku-edit.
 
ukawa washirikiane na wabunge ccm kupata spila atakayekuwa mtaifa zaid kuliko mchama
 
UKAWA watamsimamisha Goodluck Ole Medeye,miongoni mwa kura zake za uhakika ni za Chenge,Kangi Lugora,Ngereja,Tibaijuka,Bashe,Martha Umbulla,David Mathayo,Chegeni,Ndassa na wapambe wao.Sitashangaa kuona wakishinda uspika.
 
Spika huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wabunge wote, na ili uwe Spika lazima uwashinde wapinzania wako kwa idadi ya kura.

Kuna misemo ya kizungu inayosema "numbers don't lie", "if you can't fight them join them" na "divide and rule", misemo hii ina maana yake.

November 2010, ulifanyika uchaguzi wa Spika, CCM walimsimamisha Anne Makinda na upande wa upinzani walimsimamisha Mabere Marando kutoka Chadema.

Wakati huo kama zikosei CCM ilikuwa na idadi ya wabunge jumla - 252, Chadema - 45, CUF - 43, NCCR - 4 wakati UDP na TLP mmoja kila chama.

Baada ya uchaguzi Makinda alishinda kwa kupata kura 265 na Marando alipata kura 53.

Ukiangalia, Makinda alipata kura zaidi ya idadi ya kura zote za wabunge wa CCM, Marando alipata 53 mchanganuo ulikuwa 43 Chadema, 4 NCCR, na baadhi (nafikiri) kutoka CCM. Ukiangalia Makinda alipata kura 13 kutoka ama CUF au TLP au UDP.

Ni wazi Marando asingepata kura kutoka CUF kwa vile kama utakumbuka ilikuwa ni wakati wa vita vya kambi rasmi ya upinzani.

Mwaka huu 2015, idadi ya wabunge wote ni 396 yaani 264 wa majimbo ni, 113 viti maalumu, 10 wa rais, 5 kutoka baraza la wawakilishi na 1 AG.

CCM INA jumla ya wabunge 246 huku UKAWA wakiwa na 117 tu. Kama CCM wakiweka mgombea wao na UKAWA wakiweka mgombea wao bado CCM wana uhakika wa mgombea wao kushinda.

Nashauri UKAWA wasipoteze muda na mali kusimamisha mgombea kwa vile HAWATASHINDA, badala yake wamuunge mkono mmoja wa wagombea wa CCM watakayeona anaweza kulinda maslahi ya taifa na ya umoja wao.

UHALISIA:

Najua wabunge wote 396 hawatakuwepo siku hiyo, ondoa wawakilishi 5 toka Zanzibar, 8 majimbo ambayo hayakufanya uchaguzi, na sidhani kama rais atakuwa tayari ameshateua wabunge wake 10. Kwa hiyo bila kujali watakaokuwa na udhuru mbalimbali, wapiga kura (wabunge) hawatozidi 396 - 5 - 8 - 10 = 373.

Kwa hiyo kama wabunge 373 watapiga kura, ili mtu awe Spika kundi lake lazima lipate siyo pungufu ya kura 187.

UKAWA wana kura 117 jumla wanahitaji lobbying ya kura 70 toka CCM.

Watazipata?
CCM wanasimamisha mgombea mmoja tu aliyepitishwa na chama kama hawatasimamisha atapita bila kupingwa,labda ACT(Zito)asimame,au taratibu ni tofauti na 2010?
 
CCM ndo wanaamua nani awe spika hao UKAWA ni wasindikizaji tu.

acha kukurupukia jukwaa la siasa kama huwezi kuchangia.

Ni haki ya kila mtu kuchagua na kuchaguliwa hivyo uache hoja za kipumbavu.
 
ccm wammpe chenge,who cares!! hata wema sepetu anawafaa mkikosa ambaye atalinda masilah yenu
 
Back
Top Bottom