Ushauri: Tuache kukariri katika elimu!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Wasaalamu! Ni kweli na hakuna kipingamizi kuwa Elimu kwa sasa ndio mkombozi wa Maisha kwa Watanzania tulio wengi! Bila kujari ni Level Gani ya Elimu lakini pale mtu atakapo jua kusoma na Kuandika ni dhahiri kuwa elimu itakuwa imemkumboa kwani ataweza kufanya Mambo Mengi!!

Tukubali kuwa kupitia elimu kumekuwa na kudharauliana kwa kiasi kikubwa na hizi Dharau zimegawanyika,tena zimegawanyika katika makundi tofauti,kuna kudharaulina kati ya wale wenye elimu na wasio na elimu,pia wenye elimu wamekuwa wakidharauliana kulingana na level zao za elimu,hata wale wenye Level za elimu sawa wamekuwa wakidharaulina kutokana na kozi za kila mtu anazo soma,hata wanao soma kozi moja ikifika upande wa kuspecialize wamekuwa wakidharaulina!!!

Sioni maana ya kumdharau mtu kupitia elimu wakati wewe hiyo elimu uliyo pata haijawahi kukusaidia!! Watu waliopo chuo kikuu ndio wanao ongoza kwa Dharau kuliko wale walipo kazi na hii kutoka na umri kuwa mdogo unao pelekea ufinyu wa mawazo na kuamini kuwa kufika chuo kikuu ndio kuwin maisha! Unajidanganyaa! Wanafunzi wa vyuo wanamuona alie ishia kidato cha nne au darasa la saba au form six si lolote si chochote na wanasahau kuwa maisha ni duara na maisha ni kama Gwaride! Wanasahau kuwa,kuwa na Elimu isiyo na msaada katika maisha ni kama kupoteza mda!

Tukubali tukate Familia zote 99% wanaamini kuwa Elimu ndio mkombozi wa mtoto wa maskini,wanasahau kuwa bila ya kuwa na Elimu ya maisha ya kujua elimu aliyo ipata itamsaidia vipi katika maisha ni sawa na kazi buree!! Bahati mbaya sana sana katika elimu anayo ipata mwanachuo ambaye anaitumia kumdharau mtu ambaye hajafika chuo haimfundishi kujiandaa na maisha ya mtaani,haimfundishi kujiandaa na maisha bali inamlemaza akili na kumfanya afikirie kusoma,kuajiriwa basi!

Utaona mtu anakuwa akiamini kuwa MD ndo kozi nzuri kuliko kozi nyingine yoyote! Hayo ni mawazo finyu na huko ni kujazwa ujinga!! Siku zoke katika elimu Hakunaga kozi nzuri wala mbaya kozi zote ni sawa inategemea mtu na akili yako!! Jiulize wewe unaye amini kusoma MD ndo kufanikiwa kimaisha hivi unayafahamu maisha ya Madaktari hapa tanzania?,unayaafamu maisha ya maspelicist wakubwa hapa tanzania? Mbona maisha yao hayatofautiani na ya yule alie ishia Darasa la Saba na Akatumia vizuri elimu ya ujasiria mali na kufanikiwa ya nini umdharau?

Hakuna kozi za kimaskini kama MD! Tukubali tukae kuwa MD ni kimbilio la watoto wa kimaskini ambao wanaamini kuwa kusoma MD ni kujiandalia kuwa na maisha mazuri,dear sisters and brothers mnapotea! Watu wa degree acheni kuwadharau watu wa diploma,watu wa diploma acheni kuwadharau watu ambao hawajafika chuo!! Ni wakati wetu sasa kubadirika kifikra na kimawazo na kuacha kuwadharau watu wanao soma Socialogy kwa huezi jua anajiandaa vipi kukabiliana kimaisha! Take my point hakuna Kozi mbaya na Nzuri katika huu ulimwengu wa Elimu kwani Kozi zote ni sawa na kinacho tutofautisha ni mtu na akili ya kimaishaaa!!!

Hii dhana imekuwa mbaya hadi kwa serikali yetu kwani juzi hapa nimesiki waziri akisema kuwa ni lazima kusoma science kwa yule atakae fika kidato cha nne! Ukiangalia sababu anatoa VERY WEAK POINT eti kisa ni kukabiriana na Nchi ya viwanda inayokuja....point haina mashiko hivi yeye naye anataka kuwaaminisha watu kuwa Science ndo inakozo nzuri na ndio inaweza kuwatoa kimaisha watu!! Hiyo ni weak point hivi kiwandi hamna human resource?,hamna mhasibu,hakuna mpishi kiwandani,au hao nao lazima wawe wamesoma science? Hivyo viwanda vitatosha kuajiri watu wote ambao hawata opt masomo yao? Tumefika hatua ya kuanza kuwalazimisha watu wasome vitu ambavyo mwisho wa siku vitawapozea mda na nguvu zao? Mipango mibovu,walimu hamna hili hawalioni!

Tuache kumezeshana sumu,tuache dharau kwa hakuna ajuaye la kesho litakuwaje tukumbuke kwenye Elimu hakuna alie juu ya mwenzie! Ila elimu ya kimaisha ndo itakayo msaidia mtu! Ninawafahamu mdaktari wengi,Maspecialist wengi, ambao wana maisha mabovu hadi unajiuliza hizi ndo kozi ambazo watu wanatudharau nazo kwa kuamini zitawatoa kimaisha?

Niwakati wa kubadirika na kuamini katika maisha! Utakuta mtu anakuja hapa anaomba ushauri kozi ya kusoma? Kweli katika elimu hakuna ushauri, Fanya kile unachokiamini,fanya kile unacho kiweza na kamwe usiige chochote katika elimu wala kamwe usisome kisa baba kasema au mama kasema! SIMAMIA katika unacho kiamini huku ukiacha kuwadharau walio chini yako!!!

HESHIMA NA IMANI NA UVUMILIVU NI NGAO MUHIMU SANA KATIKA KUFANIKIWA! TUACHE KUDHARAULIANA!
 
Mkuu umenena ukweli ila katika negative attitudes nadhani hii makala inhekuwa kama elimu kwa vijana wetu wajue uhalisi wa maisha...

Ulimalizia makala yako vizuri...

Nami napenda kuimalizia kuwa vijana waandaliwe kutokana na changamoto za ulimwengu bila kujali ni wapi kwenye mafanikio sana kwani elimu zote kama zitasomwa kwa ajili ya kuyadhibiti maZingira na kuifanya dunia kuwa sehemu ya amani na utulivu basi kufanya hivyo itakuwa ni bora zaidi ya kuliko kujitamba na kujikweza
 
Well said mkuu...nilienda piga M.A history wadau walinicheka san nataka kuwa nan..nimekomaa imeisha nakula bata mpaka wananiogopa...noted hakun coz nzr wala n
Mbaya ni malengo ya mtu
 
Back
Top Bottom