Ushauri tafadhari

Ushauri tafadhari

jescalio

Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
7
Reaction score
3
Nina mdogo wangu alizaa na kaka mmoja na kukataa ujauzito na hata alipojifungua kupelekewa mtoto akawa anajibu mtoto sio wangu,kamtafute baba yake,hana cha huduma walanini, mtoto akiumwa akipigiwa simu anajibu mwache afe, mkimkalisha vikao anahaidi kumhudumia mtoto lakini,akitoka hana habari,kashaitwa ofisi za Ustawi wa jamii hataki.

Basi ndugu yangu tukamwambia pumzika mama tutalea mtoto, sasa ajabu ni kwamba sasa hivi baba wa yule mtoto anakuja na kumdai mtoto tena kinguvu, namtaka mtoto wangu, na vitisho kibao usiponipa mwanangu utaona na mtoto ana miaka minne sasa,sasa hivi anatumia watu waliokaribu na mama wa mtoto wanampiga picha na kumtumia huyo kaka anakazana kuchange profile huko Whatsup.

Kiufupi ameshamtamkia mama wa mtoto kuwa mwanangu nitamchukua kwa vyovyote akiwa mzima au amekufa,akiambiwa suala la kulipa fidia anakujibu sijawahi kulipa fidia kwa mtoto na hakuna nilikozalisha nikalipa fidia na kwa kifupi huwa sizuiwi kuchukua mtoto pale ninapomtaka,kuhudumia sihudumii na fidia sitoi, na mtoto nitamchukua,siwezi lipa fidia maana nitakuwa kama nanunua mtoto wangu,nisaidien wataalamu wa sheria nini kifanyike hapa? Maana kuna muda tunaona kama mwanga vile.
 
Dah......pole kwa huyo ndugu yako kuzaa na kichaa.........hakuna mtu hapo ni wazimu tu huo........
Cha kufanya muhamisheni huyo ndugu yenu akaanze maisha sehemu nyingine aondokane na huyo nsyuka.........
 
Tulishamtoa nyumbani tukampeleka kwa bibi kijijin kimyakimya pasipo huyo nsyuka kujua sijui ni nani aliyemwambia alipo na katoa wapi namba za simu hatujui ana msumbua mbaya tena kwa vitisho kuwa mwanae atampata tu akiwa mzima au amekufa sasa hatuelew tufanyeje
 
Hivi mleta mada hii ndo maada ya kuja kuomba ushauri humu???
hebu jitambue kwanza, yaani jitu zima lililoweza jikunja na kupiga bao
na kupelekea mtoto linawasumbua hivyo leo ndo lije lidai mtoto.......Hell No
 
Mbona raisi tu, Huyo dada aende polisi kwenye dawati la jinsia akatoe malalamiko yake kuwa anatishiwa amani na mzazi mwenzie, na aeleze namna alivyohangaika na mtoto na atoe msimamo wake, wataitwa wote watakutanishwa, hapo huyo mwehu atapewa kile anachostahili. alidhani ni shamba hilo kwamba unapanda unasubiri kuvuna.
 
Duu,upele unakosa mkunaji kweli,yani ningekua mimi alvyokataa mimba ndio angekua kesha chamba U.P.U.PU, nisingetaka kujua hata kama yuko duniani ana hema au laa....
 
Back
Top Bottom