Ushauri tafadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri tafadhari

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by maumbo, Jun 28, 2012.

 1. m

  maumbo Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wanajamii forum kwanza habari za asubuhi bila shaka mu wazima na kama kuna ambaye anaumwa basi ni mapenzi ya mwenyezi mungu .

  Jamani nina demu ambaye tulisoma naye shule moja ya msingi kuanzia drs la 1-7 baada ya hapo mimi niliendelea na elimu ya sekondari lakini kwa bahati mbaya yeye hakubahatika kuendelea na sekondari kwaiyo baada ya kumaliza tu std 7 akaenda dar kufanya kazi za ndani huku tukibaki kuwasiliana kama kawaida

  baadaye mimi nikajiunga na chuo na nilipomaliza sasa nafanyakazi huklu mkoani morogoro lakini cha kushangaza huyo demu wangu anatabia ya kutoa maamuzi kwa jinsi anavyofikilia yeye mara nyingine akipiga simu kama niko kazini kama sijapokea mara ananiandikia ujumbe sitaki unipigie tena simu yako futa namba yangu na mimi nimeshafuta ,namara nyingi nimekuwa na utaratibu wa kumshauri anaacha kwa muda tabia hiyo lakini baadaye anarudia tena yale yale na ameshawai kunitumia ujumbe wa kusitisha mausiano zaidi ya mara tano

  kila nikimshauri aachane na tabia hizo bado anaendeleza cha kushangaza wakati akitaka tusitishe mausiano na mimi nikiamua kumkaushia kweli angalau kwa mwezi mmoja utaona ananitumia msg ya kuniomba salio ili apate njia ya kurejesha mawasiliano baina yetu,


  jamani wanajamii forum naombeni ushauri wenu kweli kuna mapenzi ya kweli hapo au kuna wengine wanamega lakini ananitumia mimi kama kivuli chake ? Anafaa kweli kuja kuwa mke wa ndoa ? Na ukitazama kwamba yeye yuko dar na mimi niko moro. Ushauri wenu tafadhari na poleni kwa kusoma maelezo marefu hivi
   
 2. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Huyo mpenzi wako anasumbuliwa na tatizo la kukosa uelewa, hana uelewa wa jinsi maisha yalivyo yeye yupo yupo tu,hata kama simu haikupokelewa au msg haikujibiwa kwa mtu mwelewa lazima asubiri maelezo yako kabla ya kujump into conclusion..
   
 3. kiagata

  kiagata Senior Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  1.Sifa za mke wa ndoa ni nyingi na kupata mke hakuna formula ya moja kwa moja.
  2.Cha msingi wewe unatakiwa ujue unataka mke wa aina gani.
  3.Tabia ya mume ndio tabia ya mke na ndio tabia ya watoto.cha msingi wewe ndio unatakiwa ujue kuwa unataka uwe na mji wa aina gani.
  4.Kwa tabia ulizotaja hapo,mimi hanifai.Lakini mke asiyenifaa mimi haimanishi hafai kwa mwanaume mwingine.(i) Kuna wanawake waliachika,wakaolewa pengine na sasa wanafamilia bora za mfano.(ii) Kuna wanawake waliachika wakiwa na familia bora lakini sasa ni familia balaa za mfano.
  Kazi kwako,kusuka au kunyoa.
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Mwanachuo ngoja nisichangie kwanza
   
 5. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mapenzi yana aina nyingi ya kupresent,labda kwa upande wake kachangua hivyo hata hivyo Mapenzi wako akuamini hivyo anajaribu kukutega kuona msimamo wako.
   
 6. N

  Neylu JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Inawezekana hata wewe ndio ukawa tatizo pia.. Sasa usipojibu meseji ya mpenzi wako unataka ujibu ya nani? Kumbuka mko mbali mbali hapo ujue nae ana kawivu flani ukizingatia na kisomo chenyewe basi anakuwa hajiamini amini anahisi unajivinjari na wanachuo wenzio.. Kaa nae chini kwanza umpe msimamo wako na umuonyeshe kweli uko serious.. Halafu na wewe uache tabia ya kumchunia msg na calls zake...
   
 7. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ushauri nitakao kupa ni tembea na wanawake wa class yako kaka....naomba usichukie hii kama vile kumdharau huyo msichana bali kaa ukijua kwamba mitazamo yenu na waisha itatofautiana kutokkana na difference in education....sasa ili kuepesha matatizo huko mbeleni nakushauri uachane na huyo lady alafu utafute mwanamke ambaye angalau kamaliza form six. kwanza upo moro pande zipi kaka?
   
 8. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  hivi nikitaka kushusha pumzi afu niiandike kwa hapa ntaandikaje....uuuuuuuhhhhhhh....mapenzi..!!!!!
   
 9. M

  MKAROLINA Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni elimu kaka, kama una njia mbaal ya kumsaidia atleast apige hatua hata kwa kusoma masomo ya QT atajifunza mengi.
   
 10. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  i hate to say it but you are right.

  she has inferiority complex bcoz you're so much more educated compared to her and she's paranoid that you'll leave for someone better (which you probably will). if you really want to be with her, have her come to Moro to be with you.
   
 11. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni tabia ya baadhi ya wanawake kufanya hivyo ili uhisi kuwa kwa kukosa wewe mambo yake yako safi tu, lakini ukweli wenyewe ni kuwa ana haja nawe sana lakini hiyo ni kedi ili umpapatikie. Binafsi yameshanikuta na mwanzo kama wewe nikijaribu kugombeza. Nilizoea na sasa nawasiliana nae kwa wakati wangu.

  Hilo la labda anaweza kuwa na mwengine sifikiri kama anae wa uhakika kwani angekuwa na wa uhakika kedi yake ingemfanya akueleze kuwa wapo wenzio wanaomtamani ili akutie wivu.
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  blaine n kurt umesema yote
  dada ana wasi wasi na maisha yake na mahusiano yako na wewe
  lwa elimu yako na ya kwako ni vitu viwili tofauti na ana wasi wasi kuwa iko siku ataibiwa na utachukuliwa moja kwa moja
  kama unampenda kwa nini usitafute namna ya kumnyanyua kimasomo hata afikie ngazi za elimu ambapo anaweza kupambanua ulimwengu alio nao na maisha ya baadae
  hivi kwekli unamtegemea kuwa mkeo ilhali mna tofauti kubwa sana ya elimu (though sio muhimu sana kwenye maisha ya ndoa) ila kuondoa ile inferiority complex aliyo nayo better umfanyie mpango wa kunyanyuka kidogo kiellimu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Std + chuo = @#??&*%^
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Tupa kule
   
Loading...