Wakuu nina vijana wangu wawili, wa kike na wa kiume. Wote wako high school sasa. Kimasomo naona kama wanaenda vizuri ila kimaadili napata shaka kidogo hadi nimeamua kuomba muongozo kwa wadau wenzangu hapa.Wako shule tofauti na huwa nawasiliana nao kwa simu, call na texts.
Sasa mimi baba yao nilikuwa nyuma kidogo na hii technology ya whatsApp, simu yangu ilikuwa haisupport hii huduma halafu pia nilikuwa sina munkari nayo kivile. Sasa majuzi hapa nimenunua simu ya kisasa kuliko niliyokuwa nayo mwanzo ni hizi smartphone.
Sasa na mimi ndo sasa nikaamua kujiunga na haya ma-whatsApp. Katika kupekenyua huku na kule si nikaingia kwenye profile zao, daah. Vilivyoko huko sikutegemea kabisa, hayo maneno sasa ya malavidavi kwenye status zao, na yanavyobadilishwa kila siku, khaa nimechoka mwili na roho na hizo picha hivyo vivazi sasa ndo mimeishiwa nguvu kabisa, hata sijawahi waona wakivivaa nyumbani na hata sijui wanavipata wapi.
Kama mzazi najitahidi sana kuongea na wanangu, hadi huwa najipa imani kuwa wananielewa ila haya mambo yao ya kwenye mitandao ndo yamenipa mashaka sasa. Sijawauliza chochote hao watoto na wala hata wife sijamshirikisha. Nimeona nije kwanza kupata ushauri wenu kwa kunijibu mambo yafuatayo.
Je na wewe kama mzazi ulishawahi ona mambo kama hayo kwa vijana wako we uliyachukuliaje.Je haya ni mambo ya kawaida tu katika ulimwengu wa sasa hivyo niyapuuze,je nifanyeje mimi kama mzazi.
NB: Team kuponda tafadhali piteni tu huko pembeni, nitawashukuruni sana.
wapi hujaelewa mkuu? uliza nifafanue
tofauti kabisa mkuu, mi ni wa 47 huko aisee

vivazi gani vya huyo mtoto wako especially wakiume vinavyokukosesha amani??!!!
labda nikuulize wewe ni wa dini gan na shule wanayosoma inafata maadili ya dini? inakuwaje wanamiliki simu shuleni wanaruhusiwa?
mimi wa kwangu mdogo tu nilikuta ameangalia picha za xx kwenye simu yangu halafu akasahau kufuta sijui ndo hajui basi nikazikuta nilitembeza mkongoto ambao hata usahau na hadi leo huwa naacha simu kwa makusudi sijaona akirudia
lakini nmeongeza sana mafundisho ya dini ni lazima kusali sana...haya mashulle ya boarding sometimes hakuna kitu
vile vya kata Kund vile
sasa hio si kawaida tu,vi teenager vyote ndio vivazi vyao hivyo....sasa wewe kama mzazi wafundishe kuvaa suruali kiunoni,waeleze hivyo wanavyovaa sivyo,kupendeza sio lazima wavalie suruali makalioni.
ndio inafuata maadili ya dini za kikristo. Simu hawaruhusiwi kuwa nazo day time, lakini mida ya sas kumi na mbili jioni na kuelea wanakuwa nazo huko wanakolala mabwenini