Wana umri gani? Huenda puberty inawasumbua lakini angalia isiwachukue moja kwa moja... Cha zaidi wakabidhi mikononi mwa Mungu awaepushe na ya dunia...
Karucee ushauri plz!! siyo unacheka tu na kusepa bana
nimejaribu kusoma maandishi yako matamko yako hayaendani na ulicho kipost, nikama unachezea watu akili
Jifunze kuwaelewa, usitake wafuate 100% unayoyataka/kuyapenda kwa sababu dunia yako inazeeka kama ulivyo mzee, hawawezi kuvaa bugaloo ulilovaa enzi zako kwa madai ni maadili mema, usiwatenge wanao kutoka dunia yao, shukuru hawavai mbele yako (ina maana wanakuelewa na kukuheshimu) huko kwenye mawasapu umewafuata mwenyewe uwe mpole.
Sio kwamba nawaunga mkono la hasha, nimesimulia kaukweli kanakotukabili, nyinyi mmezoea kuziita changamoto.
Halafu peleleza kupiti mama yao ujue wanao wanakuita jina gani.
1. Mshua
2. Mdingi/dingi
Ikiwa wanakuita kwa namba moja basi ujue wanakukubali jinsi unavyoitikia maombi yao.
Na ikiwa wanakuita kwa jina la namba mbili ujue wanachukia baadhi ya taratibu zako ambazo wanaziita za kikoloni.
Mie kwa maoni yangu mshirikishe mkeo kuhusu hili na mkae chini kuongea kwa kina. Watoto wenu watakaporudi likizo mkae kama familia mkae tena kuongea kwa kina na kuonyesha kutoridhika kwenu na mambo mliyoyaona na kuomba wayaache mara moja. Kama ni wasikivu basi haitakuwa shida kwao kuachana na yale msiyoyaafiki ila ufuatiliaji wa kila mara ni muhimu sana. Kulea watoto hasa wa rika hilo katika hii dunia ya leo na huu utandawazi ni mtihani mkubwa. Kila la heri.