USHAURI TAFADHALI:mke kagoma kubadili dini yake

Lakunle

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
601
538
Wasalaam wandugu...
Kabla sijamwoa alinijua kuwa Mimi ni muislam,aliniahidi kubadili dini ila nimpe mda.maisha yamesonga miaka imepita tumejaaliwa kuwa na familia
Siku za hivi karibun mwenzangu nikaona amenunua kitabu Cha tenzi za rohoni ...baada ya chakula cha jioni anaanza mapambio ndani...anakemea mapepo juzi Kati kaenda kanisani na kujitambulisha ameokoka.namuuliza mbona unavunja makubaliano anadai yeye uislam hauwez...niko njia panda hapa nawaza watoto ...sijui nifanyaje.wazazi wake hawanipi ushirikiano wowote.nisaidien tafadhal
 
Mkuu.

Hapa usitumie hasira, relax hakikisha unatuliza Akili kudeal na hili Jambo.

Ukweli ni kwamba ulifanya makosa kukubali kuoa Binti asiye wa dini yako, Sasa Kama ni plan, you need to deploy plan B.

Nisipoweza kushauri ni hapa kuhusu watoto, ni wazi watatanga Sana.
 
Kwamba apige chini huu nao ni ushauri kweli? Au bomu,Ungelijua madhara wanayo pata watoto hata usinge sema ndugu.
 
..............Kosa mnalofanya vijana kwa nyie wenye dini zenu ni kuendekeza tamaa za mapenzi bila kuangalia athari za baadae,hakuna mtu atakubali kubadili imani yake kwa jambo la kijinga kama ndoa kwani wa imani yake hawapo/hawaoni?

Owa wa imani yako hata huyu atakaekudanganya leo anabadili anakuwa na target zake mje kugawana mali baadae etc so njia nzuri na bora ya kujenga familia iliyokamilika ni kujenga na mwenzi mnaendana kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wanawake wa siku hizi wamejipanga ukileta haya mambo ya vunja uhusiano anakurudisha zero,nimeona jamaa yangu yalimkuta haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asikudanganye MTU akakwambia atabadili dini kwenye mahusiano,hata akibadili atarudi kwenye imani yake ya awali......mkuu hapo hamna namna mkubaliane tu japo mnawasumbua watoto wenu
 
Achana nae huyo atakusumbua na atawapoteza watoto hayo ndio matatizo ya kua wasio amini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Nini abadili Dini??? Ndoa ndio imfanye abadili alichokuwa anaamini toka amezaliwa?? Ngumu Sana. Kila mmoja abaki na Dini yake. Maisha yaendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…