kuhusu mimba waende wote hospitali.madaktari ndio watoe ushauri sahihi..
kuhusu simu,asirudie tena kupekua simu ya mwenzie...
kabla sijakushauri naomba kujua huyo dada ana kazi au bihashara kwa ujumla anakitu anafanya kinachomuingizia income then nimshauri nini cha kufanya hapaswi kupelekwa pelekwa
Waende tuu kwa daktari waangalie suala la hiyo mimba maana atapata ushauri zaidi wa nini cha kufanya
kama mtoto wa kwanza alizaliwa kwa complications kibao utegemee na kutoa mimba kutakuwa na madhara zaidi kwa huyo dada maana inawezekana asipate tena mtoto maishani wakati ndo huyo ametoa mimba
Ni suala la kujipanga tuu kwa huyo jamaa maana mimba ndo hiyo na mtoto bado ni mdogo
Ila aji/pange tuu maana akija kuzaliwa atamkuta wa kwanza tayari ana mwaka na nusu hivi
naamini maamuzi ya kulea au kutokulea liko kwa wahusika wenyewe sasa daktari ni kwenda kusikia nyie wahusika mnatakaje lakini si kutegemea dr awaamulie
Yaani mkuu wanavyoenda kwa Dr tayari wana maamuzi yao maana Dr hata siku moja hawezi kuingilia au kuwaamulia wattoe mimba maana in case wakija kukosa mtoto watamlaumu yule Dr maisha yao yote
La muhimu analoenda kuwashauri Dr ni namna ya kuhandle the situation now ya kuwa na mimba na mtoto mdogo na athari zake na je akizaliwa mtoto hatakuwa na madhara kwa hiyo familia
mkuu hapo uko sahihi maana kama ujauzito wa kwanza ulikuwa na matatizo japo mleta mada hajasema matatizo ni yapi lakini kama yanahusiana na ujauzito kwa nini wafikirie kutoa badili ya kutafuta jinsi ya kulea???? na hili la simu nadhani ni nyongeza tu ya kukuza tatizo ila naamini kuna tatizo zaidi ya hili lililopo
mkuu hapo uko sahihi maana kama ujauzito wa kwanza ulikuwa na matatizo japo mleta mada hajasema matatizo ni yapi lakini kama yanahusiana na ujauzito kwa nini wafikirie kutoa badili ya kutafuta jinsi ya kulea???? na hili la simu nadhani ni nyongeza tu ya kukuza tatizo ila naamini kuna tatizo zaidi ya hili lililopo
Nimekuelewa mkuu. Tatizo lilikuwa ni la ujauzito, ilipelekea hata mtoto kuzaliwa Njiti wa miezi 8, ila mtoto alitoka salama na mpaka sasa ana afya nzuri kabisa. Huyu dada ni ndugu yangu wa karibu aliniomba tukutane akanieleza hayo ambayo yapo moyoni mwake, Inawezekana kuwepo mengine lakini yeye aliniomba ushauri kwa hayo. kwa wakati ule nilishindwa kumshauri, nilijikuta najikanyaga kanyaga hata mi mwenyewe maana niliogopa nisije nikatoa ushauri ambao ungeweza kuhatarisha ndoa yake, nilimuomba akae chini kwanza atulie amuombe na Mungu amuongoze kwenye hilo, maana hata mi sihafiki kabisa suala la kutoa mimba. nimemuomba anipe muda na mimi niendelee kufikiri
kabisa mkuu na nahisi wanaficha mambo mengine kuliko hili la mimba
Mkuu mambo ya ndani ya ndoa mengine ni pasua kichwa
Nimekuelewa mkuu. Tatizo lilikuwa ni la ujauzito, ilipelekea hata mtoto kuzaliwa Njiti wa miezi 8, ila mtoto alitoka salama na mpaka sasa ana afya nzuri kabisa. Huyu dada ni ndugu yangu wa karibu aliniomba tukutane akanieleza hayo ambayo yapo moyoni mwake, Inawezekana kuwepo mengine lakini yeye aliniomba ushauri kwa hayo. kwa wakati ule nilishindwa kumshauri, nilijikuta najikanyaga kanyaga hata mi mwenyewe maana niliogopa nisije nikatoa ushauri ambao ungeweza kuhatarisha ndoa yake, nilimuomba akae chini kwanza atulie amuombe na Mungu amuongoze kwenye hilo, maana hata mi sihafiki kabisa suala la kutoa mimba. nimemuomba anipe muda na mimi niendelee kufikiria.
maana litokalo njia na kusikika kwa watu mara nyingi si tatizo ila lipo ambalo linakaa uvunguni wanaona aibu kulisema kwani lazima liwadharirishe wahusika
hilo alilolifikisha kwako ni sehemu ya tatizo kwani naamini halijaanza ghafla lina mwendelezo wa muda mrefu, na wanaume wengine wanafanya kama kukomoa wakiona hakuna maelewano ndani anaweza akapiga hesabu za mimba kumfunga mke , lakini kwa huyu kulia lia kuitoa ina maana kuna tatizo zaidi isije ikawa wanataka kuachana