Ushauri: Suzuki swift na Toyota vitz

omoghaka

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
293
166
Wakuu naomba ushauri wenu kwa mwenye uzoefu wa haya Magari ya SUZUKI SWIFT na TOYOTA VITZ. Ni gari gani zuri kwa utumiaji wa mafuta na kuhimili changamoto za barabara mbovu za vijijini. Nina bajeti ya Milioni nane nahitaji kununua kati ya hayo mawili lakini sina uzoefu.

Tafadhali sana naomba ushauri wenu.
 
suzuki swift engine yake ni cc 1300 lakini vitz ipo ya cc 1000, hapo inaonekana kwenye mafuta vitz itakua inakula mafuta kidogo kuliko swift. sema kwa jinsi ulivyojieleza inaonekana kwa mahitaji yako swift itakufaa zaidi.
 
Sikushauri ununue swift au vitz hiyo pesa ni bora uendelee kuumiza kichwa utaiwekeza katika nn ili iendelee kuzalisha.. N.B Kama ww n mwanamke nunua vitz
 
Sikushauri ununue swift au vitz hiyo pesa ni bora uendelee kuumiza kichwa utaiwekeza katika nn ili iendelee kuzalisha.. N.B Kama ww n mwanamke nunua vitz
Hoja ya kipuuuzi kabisa kuwahi kutokea. Kuna gar yenye jinsia? Utakuta wewe hata baiskeli huna then unatoa hoja nyepesi kama hii.

Duc in Altum
 
8 M kwa Dar ukitulia lazima upate Swift hasa kwa dar

Duc in Altum
Nikitulia vipi mkuu,Nahitaji kuagiza toka Japani moja kwa moja kwa kutumia beforward.Yard za Dar naogopa uchakachuzi mwingi.
 
Nikitulia vipi mkuu,Nahitaji kuagiza toka Japani moja kwa moja kwa kutumia beforward.Yard za Dar naogopa uchakachuzi mwingi.
Kuagiza ni vizur kama huna haraka ila sidhan kama Dar kuna uchakachuz kama watu wengu wanavyodhani. Zipo yard kubwa na wafanyabiashara ambao wapo serious na biashara zao.

Duc in Altum
 
Wadau samahanini kwa kuingilia mada ya mtu mwingine...

Nilipenda kufahamu kati ya Swift na IST ipo ni nzuri kwa mishe za hapa mjini na kutoka kidogo nje ya mji
 
Wadau samahanini kwa kuingilia mada ya mtu mwingine...

Nilipenda kufahamu kati ya Swift na IST ipo ni nzuri kwa mishe za hapa mjini na kutoka kidogo nje ya mji
Still mi nakushauri ununue swift.

Duc in Altum
 
Chukua swift ipo juu juu kidogo kushinda vits
Kuhusu mafuta hazitofautiani sana ila spea za swift zipo juu kidogo kushinda vits
 
Back
Top Bottom