Ushauri: Slaa agombee uenyekiti CHADEMA

Ushauri: Slaa agombee uenyekiti CHADEMA

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,149
Kutokana na umahiri aliouonyesha mh.slaa kiasi cha yeye kuwa ndio kama nembo ya chama kwa sasa na ili kuepusha makundi na kuondoa mpasuko unaokinyemelea chadema nadhani ni wakati muafaka na pia kwa maslahi ya chama Dr. Slaa agombee uenyekiti wa chama na Mh. Mabere Marando agombee ukatibu mkuu wa chama.

Nina imani hawa wawili wakifanya kazi pamoja kutokana na ukaribu wao chadema itafika mbali sana na kuondoa dhana kwamba chadema ni chama cha kabila fulani tu.

Nawasilisha.
 
Hayo ni mawazo mazuri lakini tusubir maamuzi ya vikao vya chama yanayoendelea hivi sasa.
 
Ni mawazo mazuri.. Ila inaonekana ukatibu ndio anaouweza vizuri, hilo tuna uhakika nalo maana tayari ameonesha uwezo wake..naamini chadema ina watu wengi makini kabisa hawa wataamua nani awe mwenyekiti wa chama.. Atakayepatikana nipo tayari kumuunga mkono
 
Ndio maana nyie ccm mliamua kumpa jangili kinana ukatibu mkuu wa chama ili chama chenu kisionekane ni cha majambazi tu? Mkaamua kuchanganya vibaka maharamia mafisadi majambazi na majangili
 
kama ulikuwa ndani ya mawazo yangu, haya mafanikio ya CDM yametokana na kazi yake nzuri (hilo halina ubishi) pamoja na mwenyekiti Freeman, sasa kama Freeman anapumzika na kubakia mshauri wa CDM, basi kwa muda huu basi uwenyekiti apewe Dr.Slaa.

Ingawa hii itakuwa msumari mchungu kwa wana CCM, watafanya kila kiwezekanalo DR. asiwepe wadhifa huu mzito ndani ya chama chake.

Mmeshuhudia makundi, uchafuzi na menginyewe lakini kwa nguvu ya umma na kwa sababu tunaongozwa na nguvu ya mwenyezi mungu basi isharah tutawashinda mafisadi na mapesa yao.

Mungu akisimama hakuna linaloshindikana, hata Daudi aliweza kumsurubu Goriath aliyekuwa na siraha zote za kivita kwa manati tu.

na sisi CDM tutawasurubu CCM kwa manati tu. CDM for people, CDM kwa haki ya kila mtanzania.
 
Freeman Mbowe Tosha Uenyekiti Chadema
Dr Slaa Tosha Urais 2015

Freeman Mbowe & Wilbroad Slaa is the best combination ever in this world!
 
tutilize mpira kwanza. CDM ni system inayojiseti automaticaly na kwa muda muafaka.
 
Mi nasubir hayo maamuzi magumu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Freeman Mbowe Tosha Uenyekiti Chadema
Dr Slaa Tosha Urais 2015

Freeman Mbowe & Wilbroad Slaa is the best combination ever in this world!

Hatutawatenganisha mbowe na slaa, ni kama yesu na roho mtakatifu, watabaki hivo hivo mpaka tuione nuru. Ninyi magamba shugulikieni tembo wetu ndo ajenda mlionayo kwa sasa.
 
Ndio maana nyie ccm mliamua kumpa jangili kinana ukatibu mkuu wa chama ili chama chenu kisionekane ni cha majambazi tu? Mkaamua kuchanganya vibaka maharamia mafisadi majambazi na majangili

Umesahau wazinzi pia kama Mwigulu
 
Hatutawatenganisha mbowe na slaa, ni kama yesu na roho mtakatifu, watabaki hivo hivo mpaka tuione nuru. Ninyi magamba shugulikieni tembo wetu ndo ajenda mlionayo kwa sasa.

na Josephine Mushumbus anakuwa nan? Maria
 
Hatutawatenganisha mbowe na slaa, ni kama yesu na roho mtakatifu, watabaki hivo hivo mpaka tuione nuru. Ninyi magamba shugulikieni tembo wetu ndo ajenda mlionayo kwa sasa.

acha kufuru wapi imeandikwa Yesu na roho mtakatifu wamewah kuwa ma Dj au kwiba wake za watu kiasi umefikia hatua ya kuwafanisha na hivyo vijitu?
 
Ni mawazo mazuri.. Ila inaonekana ukatibu ndio anaouweza vizuri, hilo tuna uhakika nalo maana tayari ameonesha uwezo wake..naamini chadema ina watu wengi makini kabisa hawa wataamua nani awe mwenyekiti wa chama.. Atakayepatikana nipo tayari kumuunga mkono
je huoni kwamba ameshatumia vya kutosha ukatibu mkuu na sasa anatosha kwa uenyekiti?au unataka awe katibu mkuu wa kudumu kama yule seif shariff hamad wa cuf?
 
Ndio maana nyie ccm mliamua kumpa jangili kinana ukatibu mkuu wa chama ili chama chenu kisionekane ni cha majambazi tu? Mkaamua kuchanganya vibaka maharamia mafisadi majambazi na majangili

Dah! hii nimeipenda, ahsante sana.
 
Back
Top Bottom