Ushauri: Serikali pelekeni wataalamu wa biashara na ujasiriamali katika Balozi zetu kuweza kutafuta fursa za uwekezaji

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Kwako Mhe.Rais, kwako waziri wa mambo ya nje kama muhusika mkuu wa wizara ya mambo ya nje na mshauri mkuu wa rais katika mambo yahusiyo diplomasia na uhusiano wa kimataifa. Awali ya yote ninapenda kuchukua nafasi kuwapongeza na kuwatakia kazi njema za kuendelea kuimarisha vema uhusiano wa nchi yetu na nyingine.

Jukumu la kumsaidia Rais wetu ni jukumu zito kwa kipindi hiki cha kupambana na mabeberu, lakini naamni jukumu hilo linakwenda vizuri na kutunufaisha sote. Napenda kutoa mapendekezo kwenu ili kusaidia balozi zetu katika ufanisi wa kuongeza uwekezaji wenye tija nchini. Mhe. Rais katika moja ya mambo ambayo anahitaji mabalozi wafanye ni kuhahakisha wanaleta wawekezaji kuwekeza Tanzania.

Nia ya Mhe.Rais ni nzuri sana ila kuna kikwazo au changamoto ambayo ninaiona katika kutimiza nia hiyo nayo ni ukosefu wa wataalamu wa biashara na ujasiriamali katika balozi zetu. Changamoto hii inafanya nia hii iwe ngumu kufanikiwa. Kwa kuliona hilo, kama mtanzania nimeona nitoe ushauri wenye lengo la kuinua nchi yetu kiuwekezaji.

Kwa nini wataalamu wa biashara na ujasiriamali?
Biashara na uwekezaji ni fani nzuri katika uwekezaji. Wataalamu hawa watakuwa na jukumu la kuisaidia nchi yetu kutafuta fursa na kutuhabarisha. Pia, wataweza kutumia ujuzi wao wa ujasiriamali kuzitanga vema fursa za Tanzania huko wanapotuwakilisha kibiashara Zaidi. Kujua kutangaza na kutumia fursa kutafanya wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza ughaibuni, vivyo hivyo wawekezaji wa ughaibuni kuja kuwekeza Tanzania hivyo uwekezaji kuongezeka.

Wawekezaji wengi wanashindwa kupata taarifa za hali halisi ya soko huko wanapokwenda. Wawekezaji wa Tanzania wanashindwa kujua hali halisi ya soko huko ughaibuni. Uwepo wa wataalamu wa biashara na ujasiriamali katika balozi zetu kutasaidia kutupa taarifa sahihi ya soko na hivyo kuzitumia kujitathimini. Pia, wakiwepo wataalamu wa ujasiriamli na biashara itakuwa rahisi kuongea na wawekezaji wa kigeni kuhusu hali ya biashara Tanzania kibiashara.

Ni cha kufanya?

Serikali kupitia wizara unayoongeza ndiyo yenye nafasi kubwa kukuza uwekezaji na biashari ya nje. Biashara ya nje na uwekezaji utakua kama serikali itawekeza katika watu wenye kuleta matokeo sahihi. Watu hao ni wataalamu wa uwekezaji na biashara. Ninaomba, moja ya ajira zinazopaswa kuwepo ubalozi ni kwa ajili ya wataalamu wa biashara na ujasiriamali.

Pia, ili tuweze kupata taarifa kwa wakati juu ya uwekezaji , ni vema balozi zetu zingekuwa zina taarifa za kutosha katika tovuti zake. Hii itarahisha upatikanaji wa taarifa ambazo hao wataalamu watazikusanya na kuziweka.

Faida za kupeleka wataalamu wa biashara na ujasiriamali
  • Upatikanaji rahisi wa taarifa za hali ya soko na biashara moja kwa moja kutoka kwa wataalamu hao waliopo ubalozini kupitia tovuti za ubalozi
  • Ajira kwa vijana waliomaliza masomo ya biashara na uwekezaji
  • Mapato kuongezeka kutokana kwa kukua kwa biashara na uwekezaji
  • Kutangazwa kwa fursa mpya
 
Yaani hakuna haja ya serikali kutumia pesa. Balozi zote zingetakiwa kuwa na team ya washauri kutoka kwa Watanzania wanaoishi hizo nchi wataalamu wapo huko huko tena free badala ya kutumia pesa kulipa mtu
 
Back
Top Bottom