USHAURI: Serikali inunue chakula kwa wakulima

USHAURI: Serikali inunue chakula kwa wakulima

twende wote

Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
50
Reaction score
84
Niende kwenye mada.

Wakulima wameivisha CHAKULA,, lakini cha ajabu chakula kinanunuliwa na wageni wa nchi jirani kiholela, wanapeleka pesa mashine ni wananunua mchele kwa bei za kuruka.

Baada ya mavuno bei zitapanda, mara sugu, na pengine kurudisha tena tz na kutuuzia tena kwa bei mara mbili,

PENDEKEZO

Serikali chukua hatua haraka,lawama kwa wananchi zitazidi kikapu, iongozi mpo kila mahali mnachekelea tu badala ya kusaidia serikali yetu.
 
Kwahili tutamkumbuka sana Magufuli.

Hapa angetoa amri moja tu, hasa kipindi hiki cha kuvuna mpunga bilashaka Jeshi lingenunua na kutunza kwenye maghala yake, kisha wakati wa njaa Jeshi lingewauzia wananchi kwa bei yenye unafuu.

Lakini badala yake kwenye awamu hii sinto shangaa kusikia eti mama amefungua nchi, na soko liwe huria
 
Wacha wakulima wauze mazao yao kwa bei nzuri jamani, nyie wakati wote mnakosea jambo moja na ndilo linalowafanya wakulima wetu kubaki maskini maisha yao yote, nalo ni:

kuwatumia wakulima maskini wa nchi hii kwa ajili ya food security. Halafu mnalalamika mbona kilimo chetu ni duni, kwani kitakuwaje kama hakuna masoko ya uhakika?
 
We nunua chako tunza kwanini serikali ndo ikutunzie. Hao wakulima kwanini wasisubiri wauze bei nzuri?
 
Niende kwenye mada.

Wakulima wameivisha CHAKULA,, lakini cha ajabu chakula kinanunuliwa na wageni wa nchi jirani kiholela, wanapeleka pesa mashine ni wananunua mchele kwa bei za kuruka.

Baada ya mavuno bei zitapanda, mara sugu, na pengine kurudisha tena tz na kutuuzia tena kwa bei mara mbili,

PENDEKEZO

Serikali chukua hatua haraka,lawama kwa wananchi zitazidi kikapu, iongozi mpo kila mahali mnachekelea tu badala ya kusaidia serikali yetu.
Mkuu mbona unaandika kama unakimbizwa?
Elezea wageni toka wapi wananunua, na wananunua chakula gani sehemu gani!
 
Back
Top Bottom