USHAURI: Rais Samia Suluhu amteue Joseph Magufuli kuwa Mbunge na Waziri

Nikiri kuwa binafsi nilikuwa simfahamu Joseph Magufuli kwa undani hadi nilipomuona juzi akiongea kwenye kongamano la kidini kule Chamwino, Dodoma.

Kijana huyu jasiri alipokaribishwa kutoa shukrani za familia mbele ya Rais na viongozi wa dini, alionesha ukomavu mkubwa sana. Kwa wale mliofuatilia kongamano hili mtakubaliana nami kuwa hata mama Samia alionyesha kumkubali.

Bila kuwachosha na maneno mengi, naomba niingie kwenye hoja moja kwa moja. Umekuwa ni utaratibu wa kawaida kiongozi anapofariki, hasa mbunge, mtoto wake huchukua usukani wa jimbo alilokuwa akiliongoza marehemu baba au mama yake. Mifano ipo mingi sina haja ya kuitaja.

Sasa kwa kuwa Rais Magufuli kipenzi cha wana wa Tanzania, Afrika na dunia nzima ametutoka ghafla pasipo kutarajia, namuomba sana Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu amteue ndugu Joseph John Pombe Magufuli kuwa mbunge na hata kama itampendeza amteue kuwa waziri katika wizara yoyote atakayoona inafaa.

Ninazo sababu zilizonipelekea kutuma ombi langu hili kwa mama Samia na nitazieleza kwa ufupi sana kama ifuatavyo:

Marehemu Rais John Pombe Joseph Magufuli alikuwa kipenzi cha watanzania wote na dunia nzima kwa ujumla. Kitendo cha kumteua Joseph Magufuli kuwa mbunge kitawafuta machozi watanzania, hasa pale watakapokuwa wakisikia jina la Magufuli likitajwa kupitia kwa mtoto wake.

Tukumbuke kuwa Magufuli alikuwa anapendwa na watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kidini, kisiasa, kikabila, kikanda na kijamii.

Hivyo basi, uwepo wa mtoto wa Magufuli ndani ya serikali utawafariji watanzania wote na watu wenye mapenzi na maendeleo ya taifa letu.

Kama ilivyo kawaida kwa watoto wa wabunge waliofariki kufutwa machozi kwa kupewa ubunge kwenye majimbo waliyokuwa wakiyaongoza wazazi wao, kitendo cha Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mbunge na waziri kitasaidia kuifuta machozi familia kwa kuwa nina imani mshahara atakaokuwa anaupata kutokana na uwaziri utasaidia sana kuboresha hali za kiuchumi za wanafamilia.

Ingekuwa baba yake alikuwa mbunge ingekuwa rahisi sana kuteuliwa kugombea ubunge na kukalia kiti cha jimbo la baba yake.

Lakini kwa kuwa baba alikuwa Rais, na kwa mujibu sheria anayepaswa kukalia kiti hicho ni makamu wa Rais, hatuwezi kusema labda mama Samia ampishe akalie usukani kwa kuwa tukifanya hivyo tutakuwa tunavunja katiba ya nchi. Hivyo, njia pekee ya Joseph Magufuli kupenya kwenye siasa ni kupitia ubunge na uwaziri wa kuteuliwa.

Joseph Magufuli ni kijana msomi na mwenye uwezo wa kuongoza wizara yoyote ijapokuwa hajawahi kuingia kwenye siasa. Hivyo, nina imani kuwa anaweza kuwa waziri mzuri kama alivyokuwa baba yake.

Na ningependekeza mama Samia amteue kuwa waziri wa ujenzi ili kumuenzi marehemu baba yake aliyewahi kuongoza wizara hiyo kwa ufanisi mkubwa.

Ikiwa watoto wa wabunge waliowahi kuziba nafasi za baba/mama zao huko nyuma hawakushindwa, iweje Joseph yeye ashindwe?

Kwa sababu hizi nilizozitaja hapo juu, namuomba sana mama yetu na Rais wetu mpendwa H.E Samia Suluhu Hassan amteue Joseph Magufuli kuwa mbunge na kama itampendeza amteue kuwa waziri wa ujenzi.

Nawasilisha.
Hii kusema kafariki ghafla umekupata wapi wewe lofa? Chalamila ameshawahi kataa hii kitu na mkamuunga mkono. So futa mara moja afu pandisha tena uzi mwingine maana huu ni takataka!!!
 
Dahh kuna watu wana mawazo ya kipuudhi sana
Na tabia hii ya kufanya uongozi wa nchi hii kuwa wa kiimla na ikome ni upuudhi tu yaani kabisa unashauri mtu ateuliwe kwenye nafasi ya umma kama kumfuta machozi,
Mawazo ya kipuudhi sana
Aliyeandika hii hoja, akili yake ni kubwa kuzidi yako. Msome vizuri kwa utulivu utamuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi hawatakuelewa hapa. Andishi lako linataka akili kubwa kuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hyo umejipinda mda wote huu kuandika huu upuuzi yaani kiufupi wazo ulilolileta siyo baya ila hoja zako ni "dhaifu mno "
 
Familia ya Nyerere hadi Leo hakuna amepewa hata uwaziri tu ama ubalozi!

Uchaguzi wa Mwaka Jana JPM alitambua nia ya watoto wa Nyerere kugombea nafasi za Ubunge ndani ya chama kura za maoni!

Kura zikapigwa wakapata kura 1 au 2 nadhani
JPM alikuwa na uwezo wa kuwabeba wote ama hata mmoja tu ikibidi kwa nafasi zile walizopewa akina Polepole za viti maalumu!

You know what?
JPM aliwatosa, hakufanya chochote zaidi ya kuwaita akina Makongoro
Musoma siku ile wamuombee kura kwa watu wa Mkoa wa Mara, nao kweli hawakusita ama kukataa.

Kuna muda unaona unafiki wa Taifa Letu, sio ajabu kijana wa Kikwete akawa hata Naibu waziri,
Yaani sijui familia ya Nyerere ilikosea wapi masikini dah!

“acha wote tu wakinywee kikombe”
Watu wanasema JF home of Great Thinkers. Nimesoma comments nyingi sioni great thinkers. Yaani jamaa kaandika kwa akili kubwa, watu mmeshindwa kumuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kijana amtafutie permanent job kwenye taasisi moja safi inatosha (like BOT, TRA & TCRA)

Apate uwezo/uhakika wa kumtunza Mama yake na Bibi yake
Yaani wewe unadhani mama Janet anategemea watoto wake wamtunze financially?? Haupo serious
 
Mitanzania mijinga

Tukiachana na Joseph kuwa mtoto wa Magufuli ana kingine kipi kinachompa sifa ya kuteuliwa? Aliwahi kukwambia ana utashi wa siasa?

CV yake unaijua tukiachana na hizi porojo hapa?
 
Dahh kuna watu wana mawazo ya kipuudhi sana
Na tabia hii ya kufanya uongozi wa nchi hii kuwa wa kiimla na ikome ni upuudhi tu yaani kabisa unashauri mtu ateuliwe kwenye nafasi ya umma kama kumfuta machozi,
Mawazo ya kipuudhi sana
 
Nikiri kuwa binafsi nilikuwa simfahamu Joseph Magufuli kwa undani hadi nilipomuona juzi akiongea kwenye kongamano la kidini kule Chamwino, Dodoma.

Kijana huyu jasiri alipokaribishwa kutoa shukrani za familia mbele ya Rais na viongozi wa dini, alionesha ukomavu mkubwa sana. Kwa wale mliofuatilia kongamano hili mtakubaliana nami kuwa hata mama Samia alionyesha kumkubali.

Bila kuwachosha na maneno mengi, naomba niingie kwenye hoja moja kwa moja. Umekuwa ni utaratibu wa kawaida kiongozi anapofariki, hasa mbunge, mtoto wake huchukua usukani wa jimbo alilokuwa akiliongoza marehemu baba au mama yake. Mifano ipo mingi sina haja ya kuitaja.

Sasa kwa kuwa Rais Magufuli kipenzi cha wana wa Tanzania, Afrika na dunia nzima ametutoka ghafla pasipo kutarajia, namuomba sana Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu amteue ndugu Joseph John Pombe Magufuli kuwa mbunge na hata kama itampendeza amteue kuwa waziri katika wizara yoyote atakayoona inafaa.

Ninazo sababu zilizonipelekea kutuma ombi langu hili kwa mama Samia na nitazieleza kwa ufupi sana kama ifuatavyo:

Marehemu Rais John Pombe Joseph Magufuli alikuwa kipenzi cha watanzania wote na dunia nzima kwa ujumla. Kitendo cha kumteua Joseph Magufuli kuwa mbunge kitawafuta machozi watanzania, hasa pale watakapokuwa wakisikia jina la Magufuli likitajwa kupitia kwa mtoto wake.

Tukumbuke kuwa Magufuli alikuwa anapendwa na watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kidini, kisiasa, kikabila, kikanda na kijamii.

Hivyo basi, uwepo wa mtoto wa Magufuli ndani ya serikali utawafariji watanzania wote na watu wenye mapenzi na maendeleo ya taifa letu.

Kama ilivyo kawaida kwa watoto wa wabunge waliofariki kufutwa machozi kwa kupewa ubunge kwenye majimbo waliyokuwa wakiyaongoza wazazi wao, kitendo cha Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mbunge na waziri kitasaidia kuifuta machozi familia kwa kuwa nina imani mshahara atakaokuwa anaupata kutokana na uwaziri utasaidia sana kuboresha hali za kiuchumi za wanafamilia.

Ingekuwa baba yake alikuwa mbunge ingekuwa rahisi sana kuteuliwa kugombea ubunge na kukalia kiti cha jimbo la baba yake.

Lakini kwa kuwa baba alikuwa Rais, na kwa mujibu sheria anayepaswa kukalia kiti hicho ni makamu wa Rais, hatuwezi kusema labda mama Samia ampishe akalie usukani kwa kuwa tukifanya hivyo tutakuwa tunavunja katiba ya nchi. Hivyo, njia pekee ya Joseph Magufuli kupenya kwenye siasa ni kupitia ubunge na uwaziri wa kuteuliwa.

Joseph Magufuli ni kijana msomi na mwenye uwezo wa kuongoza wizara yoyote ijapokuwa hajawahi kuingia kwenye siasa. Hivyo, nina imani kuwa anaweza kuwa waziri mzuri kama alivyokuwa baba yake.

Na ningependekeza mama Samia amteue kuwa waziri wa ujenzi ili kumuenzi marehemu baba yake aliyewahi kuongoza wizara hiyo kwa ufanisi mkubwa.

Ikiwa watoto wa wabunge waliowahi kuziba nafasi za baba/mama zao huko nyuma hawakushindwa, iweje Joseph yeye ashindwe?

Kwa sababu hizi nilizozitaja hapo juu, namuomba sana mama yetu na Rais wetu mpendwa H.E Samia Suluhu Hassan amteue Joseph Magufuli kuwa mbunge na kama itampendeza amteue kuwa waziri wa ujenzi.

Nawasilisha.

Urais ulikua wa baba yao sio wa familia, hatitaji vyeo vya fadhila ,Kama ndo hivyo wapo watoto wa mwl Nyerere nao wateuliwe pia, mbona mwendazake hakuwai mteua mtoto wa kikwete kuwa waziri, hizi Tabia za upendeleo kisa mtoto wa kiongozi inatakiwa kukoma ,watulie waendeshe miradi aliowaachia, hata hivyo mwanaume hutakiwi kupenda vya bure, Kama wanapenda siasa waanze wenyewe sio kupitia mgongo wa mtu mwingine
 
Back
Top Bottom