Uko sahihi kabisa, nimewahi kusema huko nyuma kwenye post mbalimbali. Ubovu wote wa mifumo na udhaifu ndani ya nchi hii unaletwa na katiba ya rais Mungu mtu. Ukifuatilia vizuri bunge na mahakama inayosemwa ni mihimili inayojitegemea, yote udhaifu ni kwa sababu ya madaraka ya urais.Misingi ya kutegemea kudra na hisani za kiongozi ili kupata suluhu ya matatizo yetu ndo chanzo mpaka Sasa tupo hapa tulipo pasi kuzingatia sheria na kanuni zinataka nini au zina toa muongozo gani kuhusu jambo hilo.kama taifa ni muda Sasa kuunda misingi bora ya kuzingatia sheria na kanuni kwa kuweka mifumo imara yenye uwajibikaji na kila mtu anapaswa kuwajibika kulingana na sheria na kanuni.
Tabia za kuona viongozi Kama miungu watu ndo imeleta shida mbalimbali mfano leo hii shida ya kukatika kwa umeme hovyo hovyo lawama zote kwa rais ,ufisadi katika miradi mbalimbali ya umma lawama zote kwa rais wakati Kuna TAKUKURU na muda huo huo ana wasaidizi kibao chini yake hili ni zao la katiba yetu ambapo rais anapewa nguvu katika kila kitu hivyo jambo lolote ili lifanyiwe kazi lazima pawepo msukumo wa kauli ya rais.
mfumo wa check and balance haupo katika nchi yetu hivyo dhana ya uwajibikaji wa kila mihimiri ya serikali kuwa hovyo.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Nami nikaona Gari kubwa likiteremka Kutoka mlimani limefunikwa bendera ya Taifa , naliona watu wengi wenye nyuso za furaha wanapunga matawi ya miti na kuimba nyimbo za furaha wakilisindikiza gari Hilo.Mimi imefikia mahali kabisa nasema wazi kuwa bila machafuko au mapinduzi ya kijeshi/kiraia, tusitegemee mabadiliko ya kweli ya mifumo hapa nchini. Kwa sababu wanaofanya mabadiliko ya mifumo ni hawa hawa wanaofaidika na mifumo hii mibovu.
Shinikizo la mabadiliko linapokuwa kubwa wanafanya mabadiliko, lakini sio kuendana na mahitaji ya hayo mabadiliko, bali wanafanya mabadiliko bandia ili kuhadaa umma kuwa mlitaka mabadiliko, na sasa tumefanya, huku wakija na lugha za kuwa mabadiliko sio lazima yawe kama mnavyotaka nyie, bali kuendana na mazingira yetu! Kiufupi wanafanya mabadiliko ili kupunguza pressure kwenye jamii, huku wakihakikisha maslahi yao yanabaki, na sio mabadiliko stahiki.
Tusikubali tena kuongozwa na mtu asiye na ndoa rasmiKwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.
Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.
Ila shida yake ipo kwenye kuchukua hatua juu ya watu wanaomzunguka na kufanya mambo ya hovyo katika utawala wake.
Naunga mkono michakato yote ya kodi inayoanzishwa kufanyika Ila shida ipo kwenye matumizi yake ni jinsi gani tunaitumia hiyo pesa inayopatikana kwenye kodi, mfano serikali kwa ujinga imetumia bilioni 629 kwenye zoezi la sensa pekee huu ni ufisadi.
Zoezi lenyewe watu wengi bado hawajahesabiwa mpaka sasa. Leo ni siku ya 6 ndani ya zile siku saba zilizopangwa maana yake kesho ni siku ya mwisho. Zoezi limegubikwa na wizi na ufisadi wakati zoezi lingewatumia mabalozi wa nyumba kumi tu na mwenyekiti wa kijiji lingekuwa limeshakamilika kwa 100%.
wangetumia karatasi za kawaida kujaza taarifa za watu, then kwenye kata ndio wangeweka mfumo wa TEHAMA wa kuingiza zile taarifa kwa kutumia tablet tungefanikiwa kwa 100%
Kukwama kwa zoezi la katiba na tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025, ili nalo ni donda ndugu. Watu wanakushauri kwamba utashindwa uchaguzi 2025 ukileta sasa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Wanakudanganya ungeweka mazingira sawa ya uchaguzi na katiba lazima watu wangukupigia kura 2025 ili kulipa mema uliyowafanyia hata kama wasingekuchagua mema yako yangeandikwa duniani na mbinguni.
Swala ya mfumuko wa bei ndio bomu kuu, watu hawakatai kwamba vitu vinapanda duniani lakini watu wanachokataa ni kwanini vitu muhimu ndio vipande tu kwani vitu vingine ambavyo havipandi vitu havisafirishwi?
Mfano unakuta kiberiti kinauzwa shilingi 100 Tanzania nzima hakipandi bei zaidi ya miaka 10, wakati na chenyewe kinatumia mafuta kuzalishwa. Ila Ngano, mafuta ya kula na sembe inapanda kila muda kila mwaka.
Utasikia usafirishaji, kwanini mafuta ya alizeti yanayozalishwa Rukwa na Singida hapo hapo kiwandani ukiyafuata yana bei ile ile kama unayoinunua Dar es salaam?
Mh. Rais hapa tukubaliane kwamba umeshindwa ku control inflation kwa sasa, mwezi umepita mafuta yanashuka kila siku kwenye soko la dunia kwanini sisi mafuta yanazidi kupanda tu?
Kwanini uwashughulikii wafanyabiashara Ili waache ulafi wa kutaka faida kubwa?
Tofauti yetu na Zanzibar iko wapi, kwanini Zanzibar kila kitu kinachoingizwa kwenye visiwa hivyo bei zake zipo chini, hata bei zao za mafuta zipo chini kuliko sisi au ndio kusema Zanzibar ni taifa tofauti na sisi?
Basi Kama hivyo Rais Mwinyi ana uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei vile, bora tumchukue aje atusaidie huku bara baada ya 2025.
Mambo ni mengi, Ila naomba nikushauri kama unahitaji heshima ya milele basi pumzika 2025 aje mtu mwingine afanye kazi ya Urais. Inawezekana watu wanakushauri vibaya kwa sababu haukuchaguliwa na wananchi ili kukuchonganisha kwa watanzania.
Nakushauri tu kwa kuwa akili unazo ila mapenzi yanakuzidia na nahisi kwa kuwa unafaidika na uongozi kwa namna moja ama nyingine. Ukikaa chini na kutafakari kwa kina yakupasa kuyatambua haya.Tulia dozi ikuingie,kwani Mungu ni WA chadomo na sukuma gang pekee? 😆😆
Ndio ilivyo kote huko hata Duniani ndio maana ya kuwa na manifesto za vyama.
Magufuli hakuwa anafuata sheria yeyote,pili manifesto haziko kisheria ila zinatakiwa kusisitizwa na vyama husika.Manifesto ziko kufuata formalities tu, lakini utekelezaji ni utashi wa rais. Mfano halisi, manifesto ya CCM ya 2015-2020 ilisema mabinti watakaojifungua watarejea shule, lakini Magufuli si aligoma tena akiongea kwa kejeli jukwaani kuwa hasomeshi wazazi, na hakuna mwanaccm alimwambia manifesto imeruhusu? Ni mpaka mashinikizo toka nje ndio ikawa inatafutwa lugha ya zimamoto kuwa watatafutiwa elimu maalum nje ya utaratibu wa kawaida,?
Hebu niambie ni kipi rais atashindwa kufanya akitaka kisa manifesto imesema?
Umeandika ujinga mtupu..Nakushauri tu kwa kuwa akili unazo ila mapenzi yanakuzidia na nahisi kwa kuwa unafaidika na uongozi kwa namna moja ama nyingine. Ukikaa chini na kutafakari kwa kina yakupasa kuyatambua haya.
1. Hali na mwelekeo wa upepo wa kisiasa kwa mama siyo mzuri hivyo mshauri ajipange asiaminishwe na chawa au walamba asali. ( sifaidiki na kupoteza kwake kiti hivyo namuombea mema)
2. Wakati mwingine jitahidi kuuona ukweli kwenye thread za watu hata kama zinakuumiza (ukweli ulio mchungu utakusaidia kutafuta tiba kuliko uongo mtamu utakaokudumaza).
3. Mi siyo muumini wa chama fulani ila mnakosa uadilifu kwa kushindwa kuchukua lililo jema hata kama limetolewa na asiyemuumini wa chama chenu. ( mazuri huigwana mabaya huachwa)
4. Rais siyo Perfect na wanaomzunguka siyo malaika hivyo awapime hata kwa kutumia vyombo vyake vya dola kufuatilia fikra zao juu ya wanayoyaanzisha na kuja kulalamikiwa vikali na wananchi.
5. Fadhira ni nzuri ila siyo kwa wanaokuangusha ama lazima watoke kwenye jamii ya watu fulani, awe na kundi maalumu la wanaofuatilia watu wanaostahili uongozi kama wafanyavyo watu wa mchezo wa mpira miguu / kikapu.
6. Kuvaa tai yenye bendera ya taifa kwa kofia ya uzalendo ni mbinu tu we fuatilia matendo yao ni kama wale waliokuwa wakitembea na katiba ya nchi kila mahali.
7. Wengi wa wanaosifu kwa kuimba na kucheza ni wanaofaidika ( rejea mei mosi 2 zilizopita reactions zake) na response baada ya nyongeza kuwekwa, ama rejea hotuba ya Waziri wa fedha na mipango akisoma bajeti watu walivyodemka.
8. Mwisho nakutafakarisha kuhusu wananchi. ( Waandishi wa habari wanahujumu kwa kutochukua picha vizuri kuonesha nyomi la watu ). Ni ziara ya kuzindua mradi lkn unaletewa kikundi cha hamasa kama vile ni sherehe za kitaifa (kuna tatzo hapo).
Siku yoyote ikimpendeza M/Mungu mwingi wa rehema. Hatukujua namna na wakati ambapo Mwendazake angetoka madarakani.Umeandika ujinga mtupu..
Nataka unile deadline umesema mwisho wa Samia kuwepo madarakani ni lini? Nataka niweke Kumbukumbu sawa.
😁😁😁😁 Umebadiki GIA angani,safi Sana inaweza mpendeza hata 2040Siku yoyote ikimpendeza M/Mungu mwingi wa rehema. Hatukujua namna na wakati ambapo Mwendazake angetoka madarakani.
Yawezekana maana ya Mungu mengi.😁😁😁😁 Umebadiki GIA angani,safi Sana inaweza mpendeza hata 2040
Akina Kabudi na Lukuvi ni maelekezo ambayo yalikuwa hivyo. Mafisadi wenyewe wenyewe kabisa....😁 Hao inakuwa ngumu. Nchi itatikisika.Kuchukua hatua juu ya watu anaowaongoza anaweza, ndio maana aliwaondoa kina Kabudi na Lukuvi.
Tatizo lake kuwachukulia hatua wale vipenzi vyake wa karibu aliowateua yeye ndio anakuwa mgumu kuwachukulia hatua.
Matokeo yake jamaa sasa wanajiamini wanajua hayupo wa kuwafanya chochote kwani ulinzi wanao.
Hii hali ikiendelea, ndio mbele ya safari itaenda kuzalisha mafisadi wa utawala wake, hao "untouchables" wataanza kufanya ujanja na baadhi yao naona wameshaanza.
Hao mafisadi wapya ndio watakuja kuchafua taswira yake siku itakapofika akaondoka madarakani hataacha legacy yoyote, kwa namna alivyoonesha kiu ya kuutaka Urais 2025 sidhani kama ataondoka kabla ya 2030.
Hii ni namna nyingine ya kumdharau Rais. Maana yake yeye hana uwezo so kuna wanaomwendesha.Hili swala la kusema anashauriwa vibaya linanikera balaa,kwamba yeye haoni,hasikii, hatumii akili zake ama vipi?
Jukumu la kuongoza nchi linahitaji mwanaume wa ukweli huo ndo ukweli pasipokupindisha maneno rais kwa sasa kapwaya,naunga hoja Mwinyi wa zanzibar kama Mungu ataendelea kumuweka hai hadi miaka hiyo arudi huku Tanganyika.
Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
Mkuu technically iko hivi;
1. Ni kweli mama ni kiongozi muadilifu sana na mpenda haki. Aidha, ni mara chache sana kusikia kiongozi toka zbar asiye mwadilifu.
2. Kuwa na kiongozi mmoja bora peke yake hakutoshi kufanya mambo yaende sawa. Kutegemea mtu mmoja pekee ili kila kitu kiende sawa, ni sawa na kutegemea injini zuri kwenye gari yenye tairi zenye pancha.
3. Kuhusu kuchukulia watu hatua; unapaswa kuelewa kuwa nchi ina sheria lakini pia kuna actors tofauti tofauti waliopewa majukumu tofauti tofauti na mengine ya kitaalamu. Ni kweli kuna maeneo yenye matatizo ila kufikiri kama Rais anaweza kuingilia kila kitu na kuface mtu mmoja mmoja na kumchukulia hatua sio sahihi. Kiongozi mkubwa kazi yake ni kutoa maelekezo sahihi.
4. Kuhusu mfumuko wa bei; kabla ya kupendekeza solution kwenye jambo lolote, ni muhimu sana kuelewa chanzo sahihi cha tatizo.
Mwisho, ili kila kitu kiwe sawa, ni muhimu kila mtu atekeleze wajibu wake kulingana na uwezo wake na sehemu alipo. Tukiwa na watu wengi wanaofanya hivyo, ndio tutaweza kupiga hatua kwa haraka.
Vinginevyo ni sawa na kuwa na kocha mzuri na wachezaji hawana mbio, tutabakia kulaumu makocha tu kumbe ishu sio kocha bali wachezaji.
Hili swala la kusema anashauriwa vibaya linanikera balaa,kwamba yeye haoni,hasikii, hatumii akili zake ama vipi?
Jukumu la kuongoza nchi linahitaji mwanaume wa ukweli huo ndo ukweli pasipokupindisha maneno rais kwa sasa kapwaya,naunga hoja Mwinyi wa zanzibar kama Mungu ataendelea kumuweka hai hadi miaka hiyo arudi huku Tanganyika.
Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
Hii ni namna nyingine ya kumdharau Rais. Maana yake yeye hana uwezo so kuna wanaomwendesha.
Kwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.