Ushauri: Rais Magufuli mfutie kesi kijana huyu

Ushauri: Rais Magufuli mfutie kesi kijana huyu

Raisi Magufuli,wewe ukiwa ni mwanasiasa unapaswa kuwa makini na mambo "madogomadogo" ambayo ukiyapuuza yatakujenga zaidi kuliko ukiyapa uzito.

Kwa ushauri wangu,jambo unalopaswa kutolipa uzito kwa sasa na hii kesi ya kijana Isaack wa mkoani Arusha anaetuhumiwa kukutukana.Kesi ya aina hii kwa mwanasiasa katika dunia ya leo si jambo jema sana hivyo ni bora tu kuachananayo.

Mh,ninaakika kesho ukiagiza Polisi waifute kesi hiyo,utakuwa umejizolea point nyingi sana kisiasa kuliko ukiacha kesi hiyo iendelee.Sifa ya mwanasiasa ni uvumilivu na hata mzee Sitta aliwahi sema Bungeni kuwa mwanasiasa unapaswa kuwa na roho ngumu hivyo mh.jambo hili litazame upya.

Mh.Raisi labda nimalize kwa kukuulize swali hili:

Unakumbuka ni nani aliwaita wapinzani watoto ndani ya Bunge?
Kwanza wewe mwenyewe maandiko yako inatakiwa wakumulike mara nyingi umekuwa uki post maneno yenye kuwafedhehesha na kuwatusi viongozi wakuu wa nchi.
 
~~>Hata mimi ukiniita Bwege unakula ngumi moja ya Pua...


~~~>Tuacheni haki itendeke Raisi hawezi kuingilia Mahakama.
 
Kwanza wewe mwenyewe maandiko yako inatakiwa wakumulike mara nyingi umekuwa uki post maneno yenye kuwafedhehesha na kuwatusi viongozi wakuu wa nchi.
Acha kujipendekeza!Fanya kazi usiishe kwa kufuta viatu vya wakubwa.
 
Point yako ya kumuomba Rais amsamehe bure huyu kijana mwenye utovu wa nidhamu ninzuri. Lakini umeivuruga kwa kutaka kumshinikiza Rais afanye hivyo na kumuwekea mizengwe! Tukubali kwamba maadili ktk jamii yetu yanahitaji ukarabati mkubwa si kwa vijana tu hata wazee pia hasa katika mambo ya kisiasa.
Mmejiuliza itakuwaje ikitokea kijana huyu anashinda hii kesi?Nini kitafuata?
 
MASWALI 10 KUHUSU KESI YA NDUGU ISAAC.!

Leo ndugu Isaac Habakuk wa jijini Arusha amekamatwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuita Rais John Magufuli kuwa ni "Bwege" na anafanya "siasa za maigizo".

Binafsi siungi mkono siasa za kukosoa kwa kutumia matusi au lugha chafu. Kama tunakosoa tukosoe katika namna ya staha itakayolinda utu wa wale tunaowakosoa na pia tukosoe kwa maslahi ya taifa. Siamini kama matusi ni njia sahihi ya kufikisha ujumbe.

Hata hivyo nimesoma hati ya mashtaka ya kijana Isaac nikapata mkanganyiko kidogo, kwa hiyo naomba wanasheria mliomo humu mnisaidie ufafanuzi kidogo.

Maneno anayodaiwa kutumia ndugu Isaac yakamfanya akamatwe ni haya hapa "HIZI SIASA ZA MAIGIZO HALAFU MNAMFANANISHA HUYU BWEGE NA NYERERE WAPI BUANA"

Sasa naomba kaka yangu Msando Alberto, Mawakili wasomi John Mallya, Peter Kibatala, wanasheria wasomi Bob Chacha Wangwe, Ester Safari, Isaya Kitundu na wengine wenye uelewa wa sheria mnisaidie kujibu maswali yafuatayo;

1. Kwanini Polisi wamemshtaki Isaac kwamba amemtukana Mheshimiwa Rais wakati hakuna popote alipomtaja Rais kwa jina wala kwa cheo?

2. Kwanini neno "bwege" limehusishwa na Rais na si mtu mwingine?

3. Je kuna uhusiano wowote wa kinasaba, kishesria, au kimantiki kati ya neno "bwege" na neno "Rais?"

4. Kwa kuwa Ushahidi wa makosa ya jinai unataka uthibitisho usio na shaka (beyond reasonable douts), je Polisi wanaweza kuthibitisha kwamba neno "bwege" linamaanisha "Rais Magufuli?"

5. Isaac amesema "kuna bwege anafanya siasa za maigizo".. Je Polisi wanaweza kuthibitisha kuwa Rais Magufuli anafanya siasa za maigizo?

6. Mbunge wa Kilwa Mhe.Selemani Bungara aliwahi kujiita "bwege" akiwa bungeni na Hansad ikatunza kumbukumbu. Sasa kwanini Polisi hawakuona maneno ya kijana Isaac yanamlenga "bwege official" Mhe.Bungara badala ya mtukufu Rais wetu Magufuli?

7. Kuna watu wengi wanafananishwa na Mwalimu Nyerere kwa mambo mbalimbali. Kwanini Polisi wamehisi "bwege" anayefananishwa na Nyerere kwenye andiko la Isaac ni Rais Magufuli na si mtu mwingine?

8. Kwanini Polisi wanadhani anayefanya "siasa za maigizo" zilizotajwa na ndugu Isaac ni Rais wetu Magufuli?

9. Sheria inatamka wazi kuwa "An individual is never guilty by suspicion." yani mtu hawezi kutiwa hatiani kwa tuhuma tu zisizoweza kuthibitishwa. Je Polisi wanaweza kuthibitisha kuwa "bwege" ni "Mheshimiwa Rais Magufuli?"

10. Sheria pia inasema "burden of proof lies to the one who allege." Yani msalaba wa kuthibitisha tuhuma unabebwa na yule anayetuhumu. Katika kesi hii Polisi ndio wanaomtuhumu kijana Isaac. Je wataweza kuubeba msalalaba wa kuthibitisha tuhuma zilizotajwa? Mbona kama naona msalaba wa kuthibitisha umeanza kuwaelemea Polisi mapema.?

Malisa GJ.!
Mimi si mwanasheria, lakini vile vile najua kuna kitu kinaitwa circumstancial evidence. Hata kama jina la Rais halikutajwa popote na mtuhumiwa naamini 'comments' za mtuhumiwa yalianzia mahala fulani ambapo jina Rais lilikuwa ni subject of the discussion.
 
Lazima tufike mahali turudi kwenye misingi yenye kufuata maadili. Huwezi endelea na mfumo uleule wa watu kujifanya wao ni machizi.hakuna kinga wala hoja ya kumfanya mtu atukane matusi kisa flani alitukana hakuchuliwa hatua.
Ndo maana hata huyo mshtakiwa hana kinga yyt mahakamani kwamba kosa lako liko sawa na la mtu flani so sio kosa. Kingine ule ni utawala wa JK na huu ni utawala wa JPM mambo hayawez kuwa sawa hata kidogo.
Tufike mahala tujenge kizazi chenye kuheshimu utu wa mtu sio kuendelea na kizazi kibovu miaka na miaka kwa sababu zisizo na mashiko.
 
Lazima tufike mahali turudi kwenye misingi yenye kufuata maadili. Huwezi endelea na mfumo uleule wa watu kujifanya wao ni machizi.hakuna kinga wala hoja ya kumfanya mtu atukane matusi kisa flani alitukana hakuchuliwa hatua.
Ndo maana hata huyo mshtakiwa hana kinga yyt mahakamani kwamba kosa lako liko sawa na la mtu flani so sio kosa. Kingine ule ni utawala wa jk na huu ni utawala wa jpm mambo hayawez kuwa sawa hata kidogo.
Tufike mahala tujenge kizazi chenye kuheshimu utu wa mtu sio kuendelea na kizazi kibovu miaka na miaka kwa sababu zisizo na mashiko.
Kina nani waliingia madarakani kwa kampeni za matusi alafu leo hii ndio waje wakemee matusi?
 
Huwezi kumuita Rais bwege, mwalimu wako tu darasani huwezi kumuita hivyo, sembuse Rais.
Kama lingekuwa tusi wewe ungelirudia hapa kwenye JF? Tusi ni lile ambalo hata mahakamani ukiulizwa kama ni shahidi uliseme, basi unajishauri mara mbili mbili, mpaka wakili akupe msisitizo ulitaje hilo neno! Ni kweli si neno zuri kumwita mtu yoyote wachilia mbali kiongozi wa nchi, suala la kujiuliza ni kwamba kesi hii sisi kama ni taifa inatupa faida gani zaidi ya gharama kwa wanasheria. Hizi ni propaganda za vyombo vya sheria kujirundumbikizia ma allowance kwa njia ya kuwa na kesi nyingi za kushughulikia. Hatima yake, lile lengo la kubana matumizi, linatoweka kwa wajanja wachache kutumia mbinu za kisiasa kujinufaisha.
 
Ombi zuri nadhani Wahusika watalifanyia kazi....nadhani badala ya kujaza Magereza zetu bure...Wajinga kama hawa wapewe kazi ya kuosha vyoo vya mahabusu au kusafisha mitaro ya Jiji la Arusha kwa miaka miwili....kunzia alfajiri mpaka saa nane mchana.
 
Kina nani waliingia madarakani kwa kampeni za matusi alafu leo hii ndio waje wakemee matusi?
Mkuu niko tofauti na wewe, wakati wewe uko katika harakati za kuendelea na mfumo usiojali maadili na wenye kuendekeza upuuzi bila sabb za mashiko mimi niko kwenye harakati za HAPA NI KAZI TU SIASA ZA MATUSI NA MAMBO YASIYONATIJA YALIKUA ENZI ZA JK.
HAMASISHA JAMII IFANYE KAZI SIO KUSHINDANA NA VYOMBO VYA SHERIA KWA NGAO YA KWAMBA MKAPA MARA SIJUI NANI ALITUKANA HAKUSHTAKIWA.
 
Unajua ifike kipindi tutumie akili zetu bara bara....ukiacha uraisi wa nchi pia Magufuli ni mzazi na anafamilia ya watu wanaomuheshimu.....alichokifanya huyo bwana mdogo akikubaliki hata chembe kwani si ustaarabu kutusiana.....mimi nashauri sheria iachwe ichukue mkondo wake....ili wananchi wengine wajifunze kuwaheshimu viongozi wao......
 
Huyo. Lazima awe mfano hasira, zote za MCC zitashushwa kwake
 
Huyo. Lazima awe mfano hasira, zote za mcc zitashushwa kwake
Wala haitasaidi kama mnavyojidanganya bali ndio itazidi kwa watu kutumia lugha ya mafumbo.

Majibu ya haya ninayoyasema utayapata hapa hapa JF.
 
Unamaanisha Rais ndiye anakomaa na kesi? Hii kesi ya jamhuri dhidi ya huyo jamaa. Rais ana mambo mengi ya kufanya zaidi ya haya.
Dah sasa huu muda Jamhuri si ingeutumia kwenye issue ya LuGUMI??
 
Bwege na Lofa si ni maneno yanayofanana, kwa hiyo hapo moja ni tusi lingine sio tusi...
 
By the way, kama kumbukumbu yangu iko sawa kifungu cha 6 cha sheria ya makosa ya mtandaoni adhabu yake ni faini ya Tzs.2m/= au kifungo cha miaka 2 au vyote kwa pamoja. Nina hakika Team Lowassa wanayo hiyo pesa badala ya kumshauri Rais aingilie shughuli za mahakama.
 
Watu bana!! Rais hayupo kufurahisha kundi la watu wachache (Ukawa). Umevunja sheria za nchi wacha haki itendeke.
Naunga mkono uliyoandika, sasa huyu kijana asamehewe akitokea mwingine aliyepewa kiroba akitukana nae asamehewe!!!
 
Back
Top Bottom