Ushauri: Rais Magufuli mfutie kesi kijana huyu

Ushauri: Rais Magufuli mfutie kesi kijana huyu

Safi sana Lumumba ndiyo napenda hivyo serikali hii siyo ya kuleta masiara watu wanataka wawe juu hatutaki mchezo kwenye utawala huu ukileta fyoko fyoko unashughulikiwa eeh mana amna tumechoka. lakini na wale mafisadi mapapa muwashughulikie jamani isiwe kwa dagaa tu
 
Mkuu, nawashangaa sana hawa vijana wa BAVICHA wanavyishabikia matusi
Malofa na wapumbavu, . CCM wakashangilia pale jangwani . Leo mnasema BAVICHA wanashangilia matusi? Ngugi Wa Thiong'o anasema " The rich man's fart doesn't stink . semen ukweli kuwa akijamba mkubwa mnaita- manukato ila akijamba mdogo-ushuzi. Endeleen na hoja zenu za kibaguz hizo
Wewe ni mjinga na bahati mbaya hujijui kama wewe ni mjinga, mshtakiwa anashtakiwa na Jamhuri na si Magufuli wala Rais. Muwe mnajipa wa kujifunza vitu basic kama hivi, na mpaka mwisho wa kesi Magufuli hatokwenda mahakamani kutoa ushahidi, huyo mtuhumiwa atapambana na DPP na hakimu atapima hoja za upande wa mashtaka na hoja za upande wa utetezi na kutoa maamuzi kama mtuhumiwa ana kesi ya kujibu au Aquito.
 
Malofa na wapumbavu, . ccm wakashangilia pale jangwani . Leo mnasema BAVICHA wanashangilia matusi? Ngugi Wa Thiong'o anasema " The rich man's fart doesn't stink . semen ukweli kuwa akijamba mkubwa mnaita- manukato ila akijamba mdogo-ushuzi. Endeleen na hoja zenu za kibaguz hizo
Sasa umeniquote mimi ili kunipa ujumbe gani labda?
 
Nadhari aliyewaita wapinza watoto wadogo ni Mzee John magu , pia aliongeza kusema mh speaker unakazi ya kulea watoto hawa. Maandiko tuyasome ,Samehe Mara saba sabini
Malofa na wapumbavu, . ccm wakashangilia pale jangwani . Leo mnasema BAVICHA wanashangilia matusi? Ngugi Wa Thiong'o anasema " The rich man's fart doesn't stink . semen ukweli kuwa akijamba mkubwa mnaita- manukato ila akijamba mdogo-ushuzi. Endeleen na hoja zenu za kibaguz hizo
Hawa watu haina hata ya kuwajibu ni wajinga wasio jitambua.
 
Bawacha wewe si ndio huwa unasema Rais anaingilia uhuru wa mahakama? Leo hii ukijua case iko mahakamani kwanini una mshauri Rais avunje sheria na kuingilia uhuru wa Mahakama? Hii ndio demokrasia na utawala bora?

Bawacha mtoto akililia wembe mpe? Mchuma janga hula na wakwao..!
Umesahau nyie ndiyo mlisema kuwa hakuna case na atashinda?
Hebu tuache mahakama zifanye kazi.

Aaah bwana kwanza huyo mtuhumiwa anayedaiwa "kutukana", hakumtaja "Rais" bali "Magufuli" iwapo tu alikuwa anam refer Magufuli huyu ambaye ndiye Rais wa Tz

Kwa sbb hii bado kama mtuhumiwa atasema alimlenga Magufuli huyu, basi Magufuli kwa sbb ndiye mwathirika wa hilo linalodaiwa "tusi", anao uwezo kwenda kuiodolea mbali hiyo kesi!!

Au hutambui kuwa kama kesi itaendelea kuunguruma, basi kuna possibility kubwa kuwa huyu mtu anayeitwa Magufuli na ambaye ndiye anadaiwa kutukanwa akaitwa kwenda kuwa shahidi mahakamani tena akiwa kama witness namba moja?

Nikukumbushe ya Jacob Zuma, president wa SA Republic na kesi yake ya ufisadi.... alisimama mahakamani kujitetea na mwisho wa siku akatiwa hatiani.

Ulivyo wa ajabu utaniambia, SA ni tofauti na TZ na katiba ya huko ni tofauti na yetu. Kwa hili hakuna, si katukanwa yeye bhana!!!??
 
Chezea Magufuli mwenye chembe chembe ya uhaya. Mwendo wa kutengeneza kick na kudeal na vyombo vya habari mpaka mkome mwaka huu. Raisi Hana tofauti na kutafuta kick kwenye magazine kama wema sepetu
 
...inamaana mtu ahukumiwe kunyongwa mpaka kufa kwa alichokihisi/fikiri mtu kuelewa!
Ndio maana kuna circumstantial evidence, alafu pia ndio maana kuna KUUA KWA KUKUSUDIA NA KUUA KWA BAHATI MBAYA na KUKUSUDIA KUUA. Vyote vina adhabu yake.
Wanasheria wanaangaliaga na flow ya matukio na kusudio lako lilikuwa ni nini hata kama haujasema moja kwa moja wewe mtuhumiwa ulikusudia nini.
 
mambo ya kiduwanzi sana kukomaa na kesi kisa umeitwa bwege, kesi za msingi zipo kibao kwenye foleni, mtu anakuja kukomaa na kosa eti la kuitwa bwege??
Rais ana nguvu kisheria kusamehe wafungwa na kupunguza vifungo ila hana nguvu ya kufuta mashitaka, acha sheria ichukue mkondo wake, iwapo jamaa atakutwa na hatia basi rais anaweza kuingilia kati.
 
Tatizo lenu bado mnafikiri tuko kwenye siasa na utawala wa miaka ya 70 na 60 kurudi nyuma.
Unapenda sana favour - acha sheria ifuate mkondo wake, rais hana nguvu kisheria kufuta mashitaka, kama kumbukumbu zako zipo sawa, kuna jamaa mmoja alimpiga kofi mzee Mwinyi (Rais mstaaf) na mzee aliomba yule jamaa asamehewe aachwe lakini jamaa waliendelea na taratibu na jamaa alikula mvua. Hapa suala ni sheria ila si suala la miaka ya 70s or 60s
 
pombe ntamkubali sana akifuta kabisa hii sheria ya mtandao. waliotunga hii sheria kwanza sidhani kama hata huo mtandao wanaweza kuutumia. katika karne hii huwezi kuzuia watu wasitukane facebook.
Hawezi kuifuta kwani hata MCC wamegonga ukuta!
 
MASWALI 10 KUHUSU KESI YA NDUGU ISAAC.!

Leo ndugu Isaac Habakuk wa jijini Arusha amekamatwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuita Rais John Magufuli kuwa ni "Bwege" na anafanya "siasa za maigizo".

Binafsi siungi mkono siasa za kukosoa kwa kutumia matusi au lugha chafu. Kama tunakosoa tukosoe katika namna ya staha itakayolinda utu wa wale tunaowakosoa na pia tukosoe kwa maslahi ya taifa. Siamini kama matusi ni njia sahihi ya kufikisha ujumbe.

Hata hivyo nimesoma hati ya mashtaka ya kijana Isaac nikapata mkanganyiko kidogo, kwa hiyo naomba wanasheria mliomo humu mnisaidie ufafanuzi kidogo.

Maneno anayodaiwa kutumia ndugu Isaac yakamfanya akamatwe ni haya hapa "HIZI SIASA ZA MAIGIZO HALAFU MNAMFANANISHA HUYU BWEGE NA NYERERE WAPI BUANA"

Sasa naomba kaka yangu Msando Alberto, Mawakili wasomi John Mallya, Peter Kibatala, wanasheria wasomi Bob Chacha Wangwe, Ester Safari, Isaya Kitundu na wengine wenye uelewa wa sheria mnisaidie kujibu maswali yafuatayo;

1. Kwanini Polisi wamemshtaki Isaac kwamba amemtukana Mheshimiwa Rais wakati hakuna popote alipomtaja Rais kwa jina wala kwa cheo?

2. Kwanini neno "bwege" limehusishwa na Rais na si mtu mwingine?

3. Je kuna uhusiano wowote wa kinasaba, kishesria, au kimantiki kati ya neno "bwege" na neno "Rais?"

4. Kwa kuwa Ushahidi wa makosa ya jinai unataka uthibitisho usio na shaka (beyond reasonable douts), je Polisi wanaweza kuthibitisha kwamba neno "bwege" linamaanisha "Rais Magufuli?"

5. Isaac amesema "kuna bwege anafanya siasa za maigizo".. Je Polisi wanaweza kuthibitisha kuwa Rais Magufuli anafanya siasa za maigizo?

6. Mbunge wa Kilwa Mhe.Selemani Bungara aliwahi kujiita "bwege" akiwa bungeni na Hansad ikatunza kumbukumbu. Sasa kwanini Polisi hawakuona maneno ya kijana Isaac yanamlenga "bwege official" Mhe.Bungara badala ya mtukufu Rais wetu Magufuli?

7. Kuna watu wengi wanafananishwa na Mwalimu Nyerere kwa mambo mbalimbali. Kwanini Polisi wamehisi "bwege" anayefananishwa na Nyerere kwenye andiko la Isaac ni Rais Magufuli na si mtu mwingine?

8. Kwanini Polisi wanadhani anayefanya "siasa za maigizo" zilizotajwa na ndugu Isaac ni Rais wetu Magufuli?

9. Sheria inatamka wazi kuwa "An individual is never guilty by suspicion." yani mtu hawezi kutiwa hatiani kwa tuhuma tu zisizoweza kuthibitishwa. Je Polisi wanaweza kuthibitisha kuwa "bwege" ni "Mheshimiwa Rais Magufuli?"

10. Sheria pia inasema "burden of proof lies to the one who allege." Yani msalaba wa kuthibitisha tuhuma unabebwa na yule anayetuhumu. Katika kesi hii Polisi ndio wanaomtuhumu kijana Isaac. Je wataweza kuubeba msalalaba wa kuthibitisha tuhuma zilizotajwa? Mbona kama naona msalaba wa kuthibitisha umeanza kuwaelemea Polisi mapema.?

Malisa GJ.!
 
Unapenda sana favour - acha sheria ifuate mkondo wake, rais hana nguvu kisheria kufuta mashitaka, kama kumbukumbu zako zipo sawa, kuna jamaa mmoja alimpiga kofi mzee Mwinyi (Rais mstaaf) na mzee aliomba yule jamaa asamehewe aachwe lakini jamaa waliendelea na taratibu na jamaa alikula mvua. Hapa suala ni sheria ila si suala la miaka ya 70s or 60s
Nchi hii tunaijua.Anaweza kuomba ikafutwa hiyo kesi na kweli ikafutwa.Hata hivyo,ni jambo geni kwa serikali kufuta kesi?
 
Nchi hii tunaijua.Anaweza kuomba ikafutwa hiyo kesi na kweli ikafutwa.Hata hivyo,ni jambo geni kwa serikali kufuta kesi?
Na siku likitokea kubwa kuliko hilo na kesi ikafutwa na rais hali itakuwaje?
 
Watanzania tunashangaza sana sijuwi tuna nini sisi hata kama mtu atafanya ujinga wa waziwazi basi watatokea baadhi ya watu kutetea upuuzi huo hii sijuwi inatoka na nini hivi ni mala ngapi yamekua yakitolewa maonyo mbalimbali juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii iweje leo huyu apate watu wa kumpongeza na kumuona ni shujaa
 
MASWALI 10 KUHUSU KESI YA NDUGU ISAAC.!

Leo ndugu Isaac Habakuk wa jijini Arusha amekamatwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuita Rais John Magufuli kuwa ni "Bwege" na anafanya "siasa za maigizo".

Binafsi siungi mkono siasa za kukosoa kwa kutumia matusi au lugha chafu. Kama tunakosoa tukosoe katika namna ya staha itakayolinda utu wa wale tunaowakosoa na pia tukosoe kwa maslahi ya taifa. Siamini kama matusi ni njia sahihi ya kufikisha ujumbe.

Hata hivyo nimesoma hati ya mashtaka ya kijana Isaac nikapata mkanganyiko kidogo, kwa hiyo naomba wanasheria mliomo humu mnisaidie ufafanuzi kidogo.

Maneno anayodaiwa kutumia ndugu Isaac yakamfanya akamatwe ni haya hapa "HIZI SIASA ZA MAIGIZO HALAFU MNAMFANANISHA HUYU BWEGE NA NYERERE WAPI BUANA"

Sasa naomba kaka yangu Msando Alberto, Mawakili wasomi John Mallya, Peter Kibatala, wanasheria wasomi Bob Chacha Wangwe, Ester Safari, Isaya Kitundu na wengine wenye uelewa wa sheria mnisaidie kujibu maswali yafuatayo;

1. Kwanini Polisi wamemshtaki Isaac kwamba amemtukana Mheshimiwa Rais wakati hakuna popote alipomtaja Rais kwa jina wala kwa cheo?

2. Kwanini neno "bwege" limehusishwa na Rais na si mtu mwingine?

3. Je kuna uhusiano wowote wa kinasaba, kishesria, au kimantiki kati ya neno "bwege" na neno "Rais?"

4. Kwa kuwa Ushahidi wa makosa ya jinai unataka uthibitisho usio na shaka (beyond reasonable douts), je Polisi wanaweza kuthibitisha kwamba neno "bwege" linamaanisha "Rais Magufuli?"

5. Isaac amesema "kuna bwege anafanya siasa za maigizo".. Je Polisi wanaweza kuthibitisha kuwa Rais Magufuli anafanya siasa za maigizo?

6. Mbunge wa Kilwa Mhe.Selemani Bungara aliwahi kujiita "bwege" akiwa bungeni na Hansad ikatunza kumbukumbu. Sasa kwanini Polisi hawakuona maneno ya kijana Isaac yanamlenga "bwege official" Mhe.Bungara badala ya mtukufu Rais wetu Magufuli?

7. Kuna watu wengi wanafananishwa na Mwalimu Nyerere kwa mambo mbalimbali. Kwanini Polisi wamehisi "bwege" anayefananishwa na Nyerere kwenye andiko la Isaac ni Rais Magufuli na si mtu mwingine?

8. Kwanini Polisi wanadhani anayefanya "siasa za maigizo" zilizotajwa na ndugu Isaac ni Rais wetu Magufuli?

9. Sheria inatamka wazi kuwa "An individual is never guilty by suspicion." yani mtu hawezi kutiwa hatiani kwa tuhuma tu zisizoweza kuthibitishwa. Je Polisi wanaweza kuthibitisha kuwa "bwege" ni "Mheshimiwa Rais Magufuli?"

10. Sheria pia inasema "burden of proof lies to the one who allege." Yani msalaba wa kuthibitisha tuhuma unabebwa na yule anayetuhumu. Katika kesi hii Polisi ndio wanaomtuhumu kijana Isaac. Je wataweza kuubeba msalalaba wa kuthibitisha tuhuma zilizotajwa? Mbona kama naona msalaba wa kuthibitisha umeanza kuwaelemea Polisi mapema.?

Malisa GJ.!
nimeipata sehem
 
Raisi Magufuli,wewe ukiwa ni mwanasiasa unapaswa kuwa makini na mambo "madogomadogo" ambayo ukiyapuuza yatakujenga zaidi kuliko ukiyapa uzito.

Kwa ushauri wangu,jambo unalopaswa kutolipa uzito kwa sasa na hii kesi ya kijana Isaack wa mkoani Arusha anaetuhumiwa kukutukana.Kesi ya aina hii kwa mwanasiasa katika dunia ya leo si jambo jema sana hivyo ni bora tu kuachananayo.

Mh,ninaakika kesho ukiagiza Polisi waifute kesi hiyo,utakuwa umejizolea point nyingi sana kisiasa kuliko ukiacha kesi hiyo iendelee.Sifa ya mwanasiasa ni uvumilivu na hata mzee Sitta aliwahi sema Bungeni kuwa mwanasiasa unapaswa kuwa na roho ngumu hivyo mh.jambo hili litazame upya.

Mh.Raisi labda nimalize kwa kukuulize swali hili:

Unakumbuka ni nani aliwaita wapinzani watoto ndani ya Bunge?
Point yako ya kumuomba Rais amsamehe bure huyu kijana mwenye utovu wa nidhamu ninzuri. Lakini umeivuruga kwa kutaka kumshinikiza Rais afanye hivyo na kumuwekea mizengwe! Tukubali kwamba maadili ktk jamii yetu yanahitaji ukarabati mkubwa si kwa vijana tu hata wazee pia hasa katika mambo ya kisiasa.
 
Hawezi kuifuta kwani hata MCC wamegonga ukuta!
naamini uwezo anao ila hana watu wa kumshauri vizuri. hii sheria ndo kati ya sababu zilizotufanya tunyimwe pesa za mcc, hii pekeyake ni sababu tosha ya kitupilia mbali
 
Back
Top Bottom