evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,970
- 9,898
Ushauri unahitajika.
Kuna jamaa yangu aliwahi kuzaa anabinti mwezi wa 9 mwaka huu anafikisha miaka 18 huyo binti alimaliza form 4 mwaka 2024. Hakufaulu yupo nyumbani.
Sasa juzi kuna jamaa walikuja nyumbani kwake wakaleta post kwamba kuna kijana wao anataka kumuoa huyo binti wake wakaeleta posa pamoja na sh laki moja.
Sasa jamaa analalamika kwamba binti yake bado mdogo.
Hako kabinti mi mwenyewe nakafahamu bado kana akili za kitoto kabisa .
Jamaa kamuuliza binti yake kasema huyo mtu hamjui kameambiwa kuhusu kuolewa kenyewe kamaebaki kushangaa hakaelewi.
Sasa jamaa kapokea posa majibu hajawapa .
Sasa jamaa anasema alikuwa na mpango ampeleke huyo binti veta akasomee mambo ya mapambo na urembo ilinawe anasaidia kazi na mke wake (mama wa binti) ambaye ana saluni ya kike.
Wamepata taarifa kwamba huyo kijana anaendesha Balaji .
Sasa anajiuliza akubali hiyo posa au aikatae .
Jamaa yupo ana saluni ya kunyoa wanaume anaishi kwenye nyumba yake anawatoto wengine 3 wa mwisho anamiaka 3