Ushauri: Police na TRA wafanye 'System Integration' kwa malipo ya magari?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,892
16,413
Good morning wana Jf.

Leo nikiwa ninaendesha gari kuelekea maeneo ya VETA chang'ombe ghafla nikasimamishwa na traffic police wakitaka niweke gari pembeni ili wakague kama nimelipia Road Licence.

Wiki moja kabla nikiwa napita barabara ya kilwa nilikutana na kikosi cha traffic police wakiwa wametega camera ndogo yenye uwezo wa kusoma plate numbers za magari kisha wakabaini gari ipi inadaiwa faini ya kosa la barabarani ili mmiliki aweze kulipa pamoja na penalties zote.

Swali: Kwanini Traffic Police na TRA wasifanye system integration kiasi kwamba wakiweka zile kamera za kusoma plate numbers wawe na uwezo wa kuona madeni yote yanayodaiwa kwa gari husika? Kuanzia road licence, insurance, fines za traffic offences, sticker za usalama barabarani na malipo yote inayodaiwa gari?

Tatizo hapa ni nini? Hatuna programmers wa kufanya hivi ama kampuni za auctions zitakosa deals?

Ninawasilisha.
 
nilimsikia rto wa kinondoni akiulizwa swali kama hili majibu yake ni kuwa eti wakiunganisha hizo system mbili itakuwa ni mwisho watu kuazimana magari, itakua ni kosa kukutwa unaendesha gari ambayo sio lako inabidi namba ya gari jina la kwenye kadi na leseni viwe na taarifa zinazofanana!
 
Cheap justification. Hoja yake haina mantiki/logic
 
Mawazo mazuri sana. Hatuna watu makini wakusimamia utekelezaji wa haya mambo. Likipata wajanja wachache wanalipokea na kuliombea fungu, baada ya hapo kitakachofuata ni kama hadithi ya lugumi
 
sawa sawa kiongozi. Mimi nilijuaga na wewe ni mmoja wa hao wazito wa hii nchi ambao wana nafasi za kutekeleza hili
Mimi ni abiria ninayepiga kelele kila muda, lakini naishia kuambulia patupu maana dereva kaweka earphones za mbao hana habari kabisa na sisi
 
nilimsikia rto wa kinondoni akiulizwa swali kama hili majibu yake ni kuwa eti wakiunganisha hizo system mbili itakuwa ni mwisho watu kuazimana magari, itakua ni kosa kukutwa unaendesha gari ambayo sio lako inabidi namba ya gari jina la kwenye kadi na leseni viwe na taarifa zinazofanana!
Mkuu Kazi kubwa nchi hii tunayo kuhusu elimu, anaulizwa RTO kuhusu integration ya system hata ku operate computer hajui what do you expect!
 
Tra kitengo cha load licence wanamipango mibovu inayoikosesha serekali pesa. Nilipita matatizo ya uchumi. Nikapaki gali ndani kwa miaka kalibu 3. Nadaiwa laki 425,000/ ni private car. Nikaenda kulipia tra vingunguti nikiwa na 400,000/ cash. nawaomba nilipe iyo nibakiwe na deni la 25,000/ ili nimalizie nitakapolipia mwisho wa hii. Au mwisho wa mwezi. Majibu yao utafikili sio watendaji wa serekali hii. Wakasema atulipii nusu! NA mfumo wa kielectronic haupokei pesa pungufu!!.kwa iyo atuna njia ya kurisaidia!.nikasema basi niwalipe deni tu. Ego mfumo aukubali,wewe katafute pesa yote. Nikajibu kuwa kaondoka ila wausika inabidi mkaguliwe vyeti. Yank hamna option ya kupokea pesa ya serekari? Alta deni!. USHAULI WANGU.wafanye marekebisho mfumo wa kielectronics uwe na uwezo wa kupokea ela pungufu. Kwani mpaka leo sijalipa naitumia kwa kimtindo. Laki nne ya serekali nimeshazila tena.watu wengi wanaweza lipia kwa kupunguza madeni. Ishakuwa deni pokeeni. Deni linazidi mshahara.
 
Pole sana kwa usumbufu ulioupata mkuu
 
nilimsikia rto wa kinondoni akiulizwa swali kama hili majibu yake ni kuwa eti wakiunganisha hizo system mbili itakuwa ni mwisho watu kuazimana magari, itakua ni kosa kukutwa unaendesha gari ambayo sio lako inabidi namba ya gari jina la kwenye kadi na leseni viwe na taarifa zinazofanana!
Kwa hiyo matajiri waendeshe wenyewe mabai yao? Au sijaelewa vizuri!
 
nilimsikia rto wa kinondoni akiulizwa swali kama hili majibu yake ni kuwa eti wakiunganisha hizo system mbili itakuwa ni mwisho watu kuazimana magari, itakua ni kosa kukutwa unaendesha gari ambayo sio lako inabidi namba ya gari jina la kwenye kadi na leseni viwe na taarifa zinazofanana!
Kwani hata watu wasipoazimana magari kuna hasara gani kwa serikali?
 
Back
Top Bottom