Kwanzia mwanzo niliespect kuna sehemu una interest na haka kabinti,not bad kwa kuwa wewe ni mwanaume....
Kuna mambo mawili matatu ambayo hayaingii akilini kwa wepesi:-
-Kuoga,kujipulizia perfume,kutupia nguo za disco na vikorombwezo vyake...
-Kuungana na ''boyfriend asiyempenda'' kwenda disco...
-Kunywa alcohol ''kwa espectation za kutolewa''....
-Kupelekwa wherever,kupata mimba!
-Kuja kukaa na ''wewe rafiki usiyekuwa wa kimapenzi'' akakusimulia
-Ukamuonea huruma na unataka tukushauri hapa ...ok!
Sikia...
-Wanaume tunadhani tuna akili sana simply kwa kuwa tunavaa suruali,kuongea sauti nzito,na hutu tuhadidhi twa kichwa cha familia lakini ukweli ni kwamba mabinti wamejaaliwa akili ya pekee na ndiyo maana wao ndiyo wanaoendesha dunia (quote me)
-Sina sababu ya kuamini wala kutokuamini hii ngonjera ya huyu binti lakini nataka niku allert kwamba huenda ameshaona udhaifu wako na kwa kuwa anajua alikopatia mimba yenyewe hakueleweki ndiyo maana akakutunuku wewe!
Faida za kukubali hii zawadi ni kwamba utakuwa umeokoa kiumbe kama Mungu hatapitisha lake na hivyo ''ukarimu wako'' utakuwa umeongeza mdau mmoja wa kuvuta oxygen na kuexost Co2 ili kukuza uoto duniani!
Hasara za hii kitu ni kwamba kwa kuwa anatambua udhaifu wako basi tegemea kulea watoto wa wenzako kwa kuletea soft reason hadi uote mvi!