[USHAURI] Online shopping: Kuna mtu amefanikiwa kwa hapa Tz? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

[USHAURI] Online shopping: Kuna mtu amefanikiwa kwa hapa Tz?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Schrodinger Cat, May 5, 2012.

 1. S

  Schrodinger Cat Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana-JF habarini za weekend,

  Mimi ni mteja wa CRDB Visa na nimeweza kuifungua hii card yangu kutumika online.
  Pia nimejisajili paypal. Cha ajabu ni kwamba karibu mara ya tatu sasa nimenunua vitu
  online, ila baada ya muda muuzaji ananirudia hela kwa kisingizio cha kwamba
  hiyo bidhaa imeisha kwenye stock zao.

  Ningependa kujua kama kuna mtu amewahi kufanikisha manunuzi online na kupokea bidhaa
  yake hapa Bongo. Nataka nijihakikishie kwamba haya ni matukio ya bahati mbaya au
  mpango wa kimakusudi kabisa kuninyima huduma.

  Asante kwa kusoma thread hii.
   
 2. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huwa na nunua online na mara zote nimekuwa nikizipata bila matatizo. Ila tuliamua kupokelea Nairobi. Hii ni kwa sababu ya usumbufu na ipotevu wa vitu vinapofika Dar. Pia posta Tanzania wamekosa uaminifu.
  Kwa hiyo inawezekana.

  Kwanza kabla hujalipa fanya mawasiliano na wenye kuuza hiyo bidhaa na wakuhakikishie wanayo.

  Pili mkubaliane ni kwa njia gani atakutumia huo mzigo.
  Tatu wakupe gharama za kutuma mzigo. Maana mara nyingi wakiona gharama ya kutuma iko juu wanaweza kuamua kukurudishia pesa kupunguza risk. Ila kama kwangu inawezekana na kwqko pia itawezekana.
   
 3. S

  Schrodinger Cat Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa.
  Nairobi ina maana unaenda kuchukua mwenyewe mzigo?
  Labda option ya kuwasiliana na seller labda naona ni nzuri zaidi ili kujua matarajio yake yakoje.
   
 4. i

  iMind JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,908
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi huwa nanunu software ambazo na download mara tu baada ya kulipa. Mara moja tu nimenunua electronic gadget kutoka website ya marekani. Walinijulisha kuwa ili niletewe ni inabidi niongeze au nilipie fedha zaidi kwa ajili ya shipping. Waliship kufika airport Dar wakanilima kodi kubwa nikashindwa kugomboa mara moja. Wakati nasaka pesa nikalipie tax, kibox kikapotea pale airport.

  Toka wakati huo nanunua software movie na miziki tu.
   
 5. Free 4 Life

  Free 4 Life Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila kuwa makini unanunua wapi? Mimi niliwahi kuagiza jersey no.10 ya argentina kwa paypal kama wewe. Ile jersey haikuwahi kufika na $ 35 sikuweza Kurecover walinizungusha mpaka nikasamehe.
   
 6. I

  Incredible JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 937
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 180
  Ushauri wangu ni kwamba kuweni makini sana na online transactions. Ni nzuri, zinaokoa muda lakini uzoefu wangu nikwamba benki inayotoa online options yafaa ikupe huduma zifuatazo

  1. iwe na namba ya simu ambayo ni free na inapatikana masaa 24 ili ukikwama au ukigundua umeingia kwa matapeli basi upige hiyo namba na kufuta hiyo transaction

  2. wakupe credit card. CRDB ina kitu kinaitwa VISA lakini huo ni upuuzi maana VISA yao siyo credit card. Katika nchi zilizo na mabenki yasiyo mchwa, wanapokupa visa card maana yake wewe umepewa uwezo wa kununua vitu japo hauna hela, muuzuji anapata hela toka benki na wewe utakuja lipa hilo deni lako benki siku yoyote mara nyingi a month later.

  Kwahiyo, mpango wa kusema waliona hela haitoshi haupo.

  Isitoshe hapo bongo mabenki yanawaibia sana. Iweje utoe hela yako kwenye ATM ya benki yako alafu utozwe transaction costs? Anayetakiwa kukutoza pesa ni benki ambayo siyo banker wako.

  Kama kwamba hiyo haitoshi, utasikia benki zinajisifu eti mwaka huu wapeingiza faida ml 600. kwanini faida hiyo yote?
   
 7. A

  Ahmada umelewa Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimenunua service Mara nyingi but not products


   
 8. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mi nishanunua products chache amazon, zimefika zote. Vingi vitabu ambavyo havina kindle version. Ukilipia usafiri wa courier inakua uhakika kidogo japo expensive zaidi
  Nilisha-subscribe gazeti fulani, lakini nikapata nakala mbili tu kati ya 12 nyingine ziliibiwa posta. Wenye gazeti walinithibitishia kutuma mpaka na tarehe yaliyofika tz.
   
 9. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
   
 10. m

  mnasaha New Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari. Mimi nimefanikiwa kununua Mara tano na nimefanikiwa Mara tatu. Kwa hiyo inawezekana kabisa


   
 11. Dumelang

  Dumelang JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 2,190
  Likes Received: 1,543
  Trophy Points: 280
  mimi mwenzenu huwa cjui vizuri utaratibu huwa natamani kufanya hizi online shopping ila roho inasita kwanza cjui wanakataje pesa na inatakiwa ujulishe bank au la! na vipi wakichukua pesa zaidi yaani kwa ufupi i know nothing abt online transaction but i like do it one day!

  nielewesheni kidogo taratibu na procedure, na hayo mambo ya paypal
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Aisee kumbe wewe kama mimi, mi nilijaribu kununua vile vi-mp3 vya kuchezea mziki kwa redio ya gari, seller akachukua kisha akadai bidhaa zimeisha, akanirefund kupitia paypal ila hela haijulikani ipo wapi! siku nyingine hivohivo tena seller mwingine akasema hawatumi vitu Tz akanirefund, yaani wameshaniliza kama kilo hivihivi. I am used to credit cards, hizi debit cards ni uchuro mtupu na ni usumbufu sana kwa mteja, I wouldn't recommend kwa kweli.
   
 13. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mkuu,

  Mimi natumia VISA Card toka CRDB na pia nimeiunganisha na PayPal. Nimeitumia kwa muda mrefu sana na kwenye matumizi mbali mbali. Nimeshawahi kununua vitu eBay na Amazon pia na sehemu nyingine nyingi tu bila wasi wasi.

  Ni mara moja tu mambo yalishawahi kwenda mrama.

  Hope that helps!
   
 14. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu tu natumia simu. Ningekugongea bonge la like.
   
Loading...