Ushauri: Ninunue kiwanja au nifanye biashara?

Mkuu nakushauri weka 1mil pembeni na itakayobakia fikiria biashara ya kufanya ambayo itakuwa na returns hatakama ni kidogo kisha ukiimudu utaongezea mtaji. Achana na wanaokushauri kiwanja. Unless kama una shughuli inayokuingizia kipato kwasasa na huna muda wa kuanzisha biashara. Kiwanja kitakaa hapo na mwisho wa siku utaishia kukiuza japo kwa bei ya juu lakini haina tofauti sana na thamani ya hiyo hela kwasasa.. Mfano 2mil kwasasa inawezakuwa na thamani sawa na 5mil miaka mi 5 ijayo. Wanaowekeza kwenye ardhi wengi wana mkwanja wa kutosha au wana biashara nyingine au ajira. Au kama vipi fanya kama ni biashara, ununue hicho kiwanja na ukiendeleze kisha ukiuze fasta na kununua kingine. Iwe ndo biashara yako.
Naona umeongezea nyamatu kwenyempango wa kununua kiwanja,na walasioni kama ni biashara kichaa kamaunavyoiita.
 
Biashara kichaa hiyo mkuu. Inamaana ndani ya miaka mitano atakuwa kapata faida ya 3mil ambayo ni sawa na 50k kwa mwezi. Wakati huo 3mil haitakuwa na thamani sawa na sasa.
Kununua kiwanja unaita ni biasharakichaa?.

Area you serious??.
 
Naona umeongezea nyamatu kwenyempango wa kununua kiwanja,na walasioni kama ni biashara kichaa kamaunavyoiita.
Narudia tena na kusisitiza kuwa kununua kiwanja na kukiacha eti baada ya miaka kadhaa kipande bei ndipo uuze ni kutwanga maji kwenye kinu. kwani hata auze 5mil miaka mi 5 ijayo bado 5mil hiyo ndo atakayohitaji kama anataka kununua tena kiwanja kingine. Hivyo haitakuwa imemwongezea hata idadi ya viwanja. Afanye biashara ya bodaboda yeye mwenyewe au biashara nyingine yoyote au biashara ya viwanja kwa kuviendeleza na kuuza ndani ya muda mfupi ikiwezekana hata miezi kadhaa.
 
Kiwanja kinaukubwa wa 331.24sqmeter kwa hiyo bei unanunua sqmeter moja kwa Tsh 3924.64
 
Hapana sina biashara nyengine mkuu, nipo napiga kazi tu za kuajiriwa pia sina mpango wa kujenga kwa sasa maana sina pesa.
Na nikinunua bodaboda ndani ya mwaka itakua imenirudishia pesa yangu na faida kama ya 1mil tu
Ok kwa wazo langu mm hela inatakiwa uizungushe ili ikuongezee mtajiwako
 
Boda boda siyo biashara. Nunua kiwanja au kama ni biashara tafuta nyingine siyo bodaboda
Boda boda ni pasua kichwa utachanganyikiwa na kuzeeka ubongo.ila kuna nyuzi nyingi naona fursa kibao.hebu pitia thread za jukwaa hili hata page ya pili tuu utaona mambo kibao.
 
Mkuu hili ndilo zingatio langu la kwanza
sasa mbona kuna biashara umeitamka katika maneno yako bila wewe mwenyewe kujua,chukua eneo hilo kama lina mchanga uanze kuwauzia hao uliosema "karibu na eneo wanlochimba mchanga"
 
sasa mbona kuna biashara umeitamka katika maneno yako bila wewe mwenyewe kujua,chukua eneo hilo kama lina mchanga uanze kuwauzia hao uliosema "karibu na eneo wanlochimba mchanga"
Utapata pesa mpaka utakua unacheka huku unaoga bafuni na sabuni inaingia mdomoni kwa furaha
 
nunua kiwanja, kisa baada ya hapo wekea dhamana upate mkopo ufanye biashara
Hati ya kiwanja ataipata kwa gharama pia, lakini Banki wanataka ue na biashara nyingine kusapoti hicho kiwanja other wise atakaa na kusubiri jua lizame
 
Hati ya kiwanja ataipata kwa gharama pia, lakini Banki wanataka ue na biashara nyingine kusapoti hicho kiwanja other wise atakaa na kusubiri jua lizame

chief kukopa sio lazima ukachukue pesa bank, hata watu binafsi pia wanakopesha kama unadhamana ya kitu kisichohamishika. kama anakiwanja, na documents za makabidhiano anazo tunaandikishana tu mkataba na iyo pesa anayotaka ntampa akafungulie biashara.
 
Acha ujinga... zungusha pesa.... kiwanja ndio nini.... yaaani hadi utakua na wajukuu bado ardhi itakuwepo tu...

Tatizo la vijana munapenda saana mjini.... wakati hujui kuwa hata mdaula kutakua mjini tu kabla haujapata pesa....

Wanaowekeza asset ni watu wanaojimudu kimaisha... mwenzangu na mimi kajamba nani pangu pakavu umeokota m2 badala ya kuizungusha ijae unawaza kiwanja.... nunua ule mavi.....

Dadek
Asipo kuelewa hapa basi tena
 
Kama kina ukubwa huo (almost 20m x 20m) kwa bei hiyo kinunue haraka. Probably hakijapimwa na unaweza kufuatilia hati mapema ili kukiongezea thamani. Achana na biashara ya Bodaboda kwa sasa. Itakutia mawazo tu.

Presiely 18.3 M x 18.3 M OR 334.9 SQM !!!
 
Huo ndio ukweli wa hali unapata milioni 5 unakimbilia kiwanja,sijui utakula hicho kiwanja
Waindi na Waarabu hawana viwanja wanazungusha pesa tuuuuuuuu. Sisi masikini tunaangaika na viwanja badala ya kuzungusha pesa yako. Mwisho wa siku sehemu ikiwa mjini mwenye pesa anakuja anakuondoa, kwa sababu huna power ya pesa
Waafrika wanaangamia kwa kukosa Elimu ya Fedha
 
Hapana sina biashara nyengine mkuu, nipo napiga kazi tu za kuajiriwa pia sina mpango wa kujenga kwa sasa maana sina pesa.
Na nikinunua bodaboda ndani ya mwaka itakua imenirudishia pesa yangu na faida kama ya 1mil tu
Nakushauri kijana mwenzangu achana na wanaokushauri nunua kiwanja. Awo ni waoga wa maisha na wengineo wameshafeli kimaisha. Fanya mchakato nunua boxer-150 ya Tsh 1.4 milion
Alafu kama kazini unaingia saa moja, amka asubuhi piga mishe mishe za boda boda na jioni kama unatoka kazini saa 11 piga mda huo mpaka saa 2 usiku. Uwezi kukosa elfu 10. Kwa siku na siku za wikiend unakomaa. Kwa mwaka tayari pesa yako imerudi na mishe zikaendelea
Lakini kama ukimpa mtu, ujue umetoa sadaka hakuna faida yoyote. Biashara yenye faida ni kuwepo mwenyewe na sio kumpa mtu hakuna faida yoyote
 
Nimependa sana ushauri wenu wakuu, mi nina kiwanja changu nilitaka kukiuza, sema nilikuwa nafikilia sana. Sasa nimepata mawazo yenu, na kitu ambacho nimekipata ni kuwa hata ukinunua kiwanja leo hadi kufika mwaka 2020 thamani yake ni ile ile hata kama umekiuza kwa ongezeko la pesa.
 
Nakushauri kijana mwenzangu achana na wanaokushauri nunua kiwanja. Awo ni waoga wa maisha na wengineo wameshafeli kimaisha. Fanya mchakato nunua boxer-150 ya Tsh 1.4 milion
Alafu kama kazini unaingia saa moja, amka asubuhi piga mishe mishe za boda boda na jioni kama unatoka kazini saa 11 piga mda huo mpaka saa 2 usiku. Uwezi kukosa elfu 10. Kwa siku na siku za wikiend unakomaa. Kwa mwaka tayari pesa yako imerudi na mishe zikaendelea
Lakini kama ukimpa mtu, ujue umetoa sadaka hakuna faida yoyote. Biashara yenye faida ni kuwepo mwenyewe na sio kumpa mtu hakuna faida yoyote

Ulicho kisema hapa ni ukweli mtupu wa bila kupepesa macho hata kope kabisa mdau.narudia tena ni ukweli mtupu
 
Una mill 2 mkononi na una option mbili moja ya kununua kiwanja na pili ni bodaboda..source ya option izo ni rafiki ako aliyekushaur ununue kiwanja chao na pili ni ww mwnyew(bodaboda)..ushauri mwing uliopewa apa ni kununua kiwanja na baadh wamesema uzungushe hela iyo.. kwa mtazamo wng: kwnz ww mwnyw binafsi inabid utambue ni aina gani ya uwekezaj unaotaka kufanya je ni wa muda mfupi,wa kati au wa muda mrefu,investment hizo hutegemea na malengo ako na uhitaji wako wa faida(ROI) meaning how soon do u need yo money back je ni baada ya miez6,miaka 3,10 au 20.. aina hizo pia zina aina zake za wawekezaji sasa sitaingia uko.. lakini KIKUBWA kuna principle ya pesa one of my mentors hupenda kuniambia inaitwa RISK TORELANCE AND TIME HORIZON ina maelezo meng lkn kifupi tizama umri wako na uvumilivu wako ktk kitu kinaitwa hasara..kama una miaka above 35 nunua tu hicho kiwanja na usubir kikulipe uzeeni(55) au watoto wako,na kama uko kwa 20's ingia ktk biashara.. kuhusu mawzo ako:kiwanja ni uwekezaji wa muda mrefu na kwa capital ako ya tarakimu 6 UWEKEZAJI HUO HAKUFAI WW..ukweli ni mgumu kumeza ila ndio iko ivo kwa mtaji wa digit 6 utasugua benchi...tuje kwny wazo la bodaboda mara nying watu ninaokutana nao huwa na wazo hilo na sikuzote ushaur wng huwa huwez kuwa na mill2 ukadumbukiza uko au mill7 ukanunua bajaj then wat follows?..zipo fursa nying kwa hela iyo inatosha kabisa na sabab natumia simu sitoandika sana lkn waweza kuizungusha ktk biashara kama ya mifugo hasa ya mbuzi au kondoo au nafaka na uka idouble iyo hela..chochote utakachoamua kufanya hakikisha kinakuwa ni ktk mzunguko wa haraka maana ake kununua na kuuza lakini zingatia sana principle of risk torelance and time horizon ktk uamuz wako..kila la kheri #G.T.O

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom