Ushauri: Ninunue kiwanja au nifanye biashara?

Zeroth

Member
Jan 26, 2017
25
45
Habari,

Nina kiasi kama sh mil2 hivi, nilikua nina mpango wa kufanya biashara ya bodaboda lakini kuna rafiki yangu wa karibu tu ameniambia kwamba mama yake ana kiwanja anakiuza kipo maeneo ya Mbande Dar es salaam, bei yake ni mil1.3 na kina ukubwa wa futi 60 kwa 60 ndio maelezo yake aliyonipa so imenibidi nije humu jf kwa msaada zaidi.Kwa hiy Kwanza kabisa naomba kujuzwa kama hicho kiwanja na hiyo bei vinalingana? Kama hiyo bei ya kiwanja ni sawa je nifanye nini kati ya hayo?
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
12,779
2,000

Boda boda siyo biashara. Nunua kiwanja au kama ni biashara tafuta nyingine siyo bodaboda
 
Ginner

JF-Expert Member
May 8, 2011
1,189
2,000
Habari,

Nina kiasi kama sh mil2 hivi, nilikua nina mpango wa kufanya biashara ya bodaboda lakini kuna rafiki yangu wa karibu tu ameniambia kwamba mama yake ana kiwanja anakiuza kipo maeneo ya Mbande Dar es salaam, bei yake ni mil1.3 na kina ukubwa wa futi 60 kwa 60 ndio maelezo yake aliyonipa so imenibidi nije humu jf kwa msaada zaidi.Kwa hiy Kwanza kabisa naomba kujuzwa kama hicho kiwanja na hiyo bei vinalingana? Kama hiyo bei ya kiwanja ni sawa je nifanye nini kati ya hayo?

nunua kiwanja, kisa baada ya hapo wekea dhamana upate mkopo ufanye biashara
 
Zeroth

Member
Jan 26, 2017
25
45
nunua kiwanja, kisa baada ya hapo wekea dhamana upate mkopo ufanye biashara
Vipi hiyo bei ya kiwanja ndugu, maana mwenyewe amenambia kua ni rahisi sana ndio yakanijia mawazo hayo ya kucancel malengo ya biashara
 
Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
2,772
2,000
Mkuu nimezipata kwa kufanya kazi lakini malengo yangu yalikua ni kununua bodaboda
vizuri boda boda achana nayo utapoteza muda wako na fedha yako!
nijibu tena maswahil haya
muda wako ukoje? je unao muda wa kutosha wa kusimamia shughuli unayoianzisasha?
kabla ya kufikia uamuzi wa kufanya biashara ya boda boda ulikuwa unawza biashara gani nyingine? unapendelea nini mfano kama unapenda kula kama mimi mgahawa mdogo unaweza kuanzisha na muda kama unao, vinginevyo bado nakushauri nunua kiwanja japo sikushauri ununue hicho nenda ndani zaidi upate hata eneo la laki saba nyingine ujipange kwa biashara. miaka ya nyuma nilinunua eneo laki saba kwa sasa nazungumzia 20m na lingine nilinunua 150,000 kwa sasa nazungumzia 20m.
 
Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
2,772
2,000
Ila mkuu kwa biashara kama ya bodaboda baada ya miaka mitano itakua imenizalishia zaidi ya hiyo 5mil! Au vipi?
baada ya miaka mitano? milioni tano ni nini kwa kiwanja baada ya miaka mitano? kitakuwa kimeenda zaidi ya twenty
 
Zeroth

Member
Jan 26, 2017
25
45
nunua kiwanja, kisa baada ya hapo wekea dhamana upate mkopo ufanye biashara
Mkuu asante kwa ushauri mzuri huu, pia naomba kujua kwa kiwanja kama hiki ukiwekea dhamana unaweza ukapewa mkopo wa Kiasi gani na kwa muda gani?
 
Devon sawa

Senior Member
Apr 30, 2017
164
225
Habari,

Nina kiasi kama sh mil2 hivi, nilikua nina mpango wa kufanya biashara ya bodaboda lakini kuna rafiki yangu wa karibu tu ameniambia kwamba mama yake ana kiwanja anakiuza kipo maeneo ya Mbande Dar es salaam, bei yake ni mil1.3 na kina ukubwa wa futi 60 kwa 60 ndio maelezo yake aliyonipa so imenibidi nije humu jf kwa msaada zaidi.Kwa hiy Kwanza kabisa naomba kujuzwa kama hicho kiwanja na hiyo bei vinalingana? Kama hiyo bei ya kiwanja ni sawa je nifanye nini kati ya hayo?
Usitake kujua uhalali wa bei mkuu,cha msingi ni kujua hilo eneo anayr limiliki analimiliki kihalali au kimagumashi na kama hakuna mgogoro nadhani haliwezi kuuzwa kwa bei hiyo ,kwa maana nyingine unanunua kesi.
 
CHIEF MP

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
1,563
1,500
Umeomba ushauri ila inaonekana mbishi. Usipende kupata ushauri kama akili yako haijajiandaa kusikiliza maoni tofauti na hisia zako.
 
Zeroth

Member
Jan 26, 2017
25
45
vizuri boda boda achana nayo utapoteza muda wako na fedha yako!
nijibu tena maswahil haya
muda wako ukoje? je unao muda wa kutosha wa kusimamia shughuli unayoianzisasha?
kabla ya kufikia uamuzi wa kufanya biashara ya boda boda ulikuwa unawza biashara gani nyingine? unapendelea nini mfano kama unapenda kula kama mimi mgahawa mdogo unaweza kuanzisha na muda kama unao, vinginevyo bado nakushauri nunua kiwanja japo sikushauri ununue hicho nenda ndani zaidi upate hata eneo la laki saba nyingine ujipange kwa biashara. miaka ya nyuma nilinunua eneo laki saba kwa sasa nazungumzia 20m na lingine nilinunua 150,000 kwa sasa nazungumzia 20m.
Okay ndugu nimekuelewa sana asnte, ila kwa hicho kiwanja si kipo mjini kidogo ndiyo maana bei ikafika huko? Au zipo sehem nzuri kidogo yani isiwe kijijini kivile unapopajua ambapo ntapata rahisi zaidi
 
SAW V111

Member
Oct 30, 2016
93
125
Habari,

Nina kiasi kama sh mil2 hivi, nilikua nina mpango wa kufanya biashara ya bodaboda lakini kuna rafiki yangu wa karibu tu ameniambia kwamba mama yake ana kiwanja anakiuza kipo maeneo ya Mbande Dar es salaam, bei yake ni mil1.3 na kina ukubwa wa futi 60 kwa 60 ndio maelezo yake aliyonipa so imenibidi nije humu jf kwa msaada zaidi.Kwa hiy Kwanza kabisa naomba kujuzwa kama hicho kiwanja na hiyo bei vinalingana? Kama hiyo bei ya kiwanja ni sawa je nifanye nini kati ya hayo?
Nunua hicho kiwanja mkuu
 
Man Thom

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
717
1,000
Kiwanja ni asset isiyohamishika tofauti na bodaboda, na kadri siku zinavyokwenda thamani ya ardhi inazidi kupanda, so ni bora kuwekeza kwenye ardhi itakulipa siku za usoni!
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
8,762
2,000
bei yake ni mil1.3 na kina ukubwa wa futi 60 kwa 60 ndio maelezo yake aliyonipa
Kama kina ukubwa huo (almost 20m x 20m) kwa bei hiyo kinunue haraka. Probably hakijapimwa na unaweza kufuatilia hati mapema ili kukiongezea thamani. Achana na biashara ya Bodaboda kwa sasa. Itakutia mawazo tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom