Ushauri: Nimemwambia mchumba wangu ukweli kuwa nina mtoto, analia toka jana akinilaumu

kakabahati

Member
Oct 28, 2013
62
22
Mimi ni mwanaume mwenye miaka 31,nina mpenzi wangu tumedumu nae kwenye mahusiano takribani miaka miaka 3,sasa umefika wakati mimi na yeye tumeona ni wakati muafaka wa kuishi pamoja,tumeshatambulishana kwa wazazi wote .

Bahati mbaya kuna kitu nilimficha kwa sababu kila nilipokuwaga najaribu kumweleza alikuwa anapanic sana,sasa imefika wakati nimeona nimweleze ukweli tuu,na jana ndio ilikuwa siku yenyewe nilipomwambia mwenzangu kuwa mimi tayari mwenzio na mtoto na ana miaka miaka3.

Sasa ni analia toka jana akinilaumu kwa nini sikumwelezaga siku zote,na mimi nimemwambia ni kwa sababu kila nilipokuwa naanza kukueleza ulikuwa unabadilika sana nikawa nashindwa, lakini naona mwenzangu haelewi,naombeni mnishauri nifanyeje mwenzenu,NOTE: nampenda sanaaaa
 
Hana mapenzi na watoto huyo......hapo ni dosari tayari ila cha muhimu usimuoneshe kujutia kuwa na huyo mtoto.....onesha unampenda mtoto na uko tayari kumpoteza yeyote anayetishia mahusiano yako na mwanao,atajirudi tu
Ila na wewe mambo ya kwenda kukumbushia na mama mtoto achana nayo hicho ndicho kinampa hofu huyo binti.
 
Mi nakataa sio kuwa hana mapenzi na mtt!
Huwezi jua maisha aliyoishi/pitia mpk aumie kiasi hicho,ipo sbb!

Mi tu nilishakataa hizo habari za mwanaume mwenye mtt sbb ya nilikopitia,sio kuwa siwezi lea au kuwa nina roho mbaya ,no!

Kosa ni kutomwambia mapema tu ili mwanamke ajue km ataweza kuendelea au vp!
 
Ulichelewa sana kumwambia lakini umefanya jambo jema sana kumwambia. Ameumia coz ulitakiwa kuwa wazi mapema sana, kuna mambo ya kuficha lakini sio damu yako.

Now, just hang in there, she will come along. Akishindwa kukubaliana na hali halisi atakuacha, which isn't bad IMHO.
 
Hana mapenzi na watoto huyo......hapo ni dosari tayari ila cha muhimu usimuoneshe kujutia kuwa na huyo mtoto.....onesha unampenda mtoto na uko tayari kumpoteza yeyote anayetishia mahusiano yako na mwanao,atajirudi tu
Ila na wewe mambo ya kwenda kukumbushia na mama mtoto achana nayo hicho ndicho kinampa hofu huyo binti.
Mapenzi na mtoto hapo hakuna tena, jiandae kisaikolojia zaidi ktk ndoa yako kilala heli mzee
 
Ulichelewa sana kumwambia lakini umefanya jambo jema sana kumwambia. Ameumia coz ulitakiwa kuwa wazi mapema sana, kuna mambo ya kuficha lakini sio damu yako.

Now, just hang in there, she will come along. Akishindwa kukubaliana na hali halisi atakuacha, which isn't bad IMHO.
Mpwa,
Wamekuwa kwenye mahusiano kwa miaka mitatu. Ana mtoto wa miaka mitatu.

Sometimes tusiwaonee hawa dada zetu. Huyo binti ana haki ya kulia na hata kumuacha bila kunyoshewa kidole na mtu yeyote.

Aende akamuoe aliyemzalisha.
 
Upo sahihi mpwa, ana haki kulia. Tunaambiwa katika mahusiano tusiwe watu wa siri siri.

Asipokubaliana na ukweli uliokuja late, amuache coz jamaa ana makosa.
 
Umechelewa kumwambia ila pia Wanaume tuna tabia moja kwenye hili suala.

Unapima huyu mwanamke nikimwambia nina mtoto kwa jinsi alivyo si atanikimbia unajipa moyo ngoja nisubiri chance ya kumwambia itakayopunguza chance ya kuachwa au reaction kali mwisho miaka inakata.

Hili lipo hata kwenye ndoa, unakuwa umezaa/ulizaa nje na mke hajui. Na sio kwamba hautaki ajue..ila unahofia nikimwambia aidha ataondoka,suicide, dispoint, n.k.

Unalitunza yakiharibika ndiyo inajulikana...

Kikubwa Mzee ushamweleza acha aamue kusuka au kunyoa. Yeye ndiye mwenye kujua achague lipi.
 
Asipokubaliana na ukweli uliokuja late, amuache coz jamaa ana makosa.

Naam hilo ndilo analopaswa kuambiwa na kila mtu hapa. Kuwa yeye ndo mqenye makosa na anapaswa kuwa mnyenyekevu kwa huyo binti hasa, sio kwa sababu ni mwanamke kiumbe dhaifu, ila kwa sababu yeye ni mkosefu.

Baada ya hapo amuelezee kinagaubaga yaliyotokea, hiyo mimba ilipatikana wakiwa kwenye mahusiano au miezi mingapi kabla. Mtoto yuko wapi anaishije?

Wamekuwa kwenye mahusiano miaka mitatu, naamini walishazungumza juu ya finances. Maana yake alikuwa akidanganya (unless huwa hamtunzi mwanaye). Je, nini kitabadilika.

In short kuanza mazungumzo upya...miaka mitatu yote inafutika mnaanza discussion moja ya kila kitu.

A waste of the lady's time.
 
Back
Top Bottom