Ushauri: Nimempa ujauzito mchumba wa binamu yangu

sasa dada yangu atunzaje mimba wakati anajua kabisa ni mchumba wa binamu yake? unajua kuna vitu tunafanya hata shetani mwenyewe anashangaa!!
Si unajua ule usemi kitanda hakizai haramu.

Wanaweza kutoa je wataweza kuishi na maumivu ya moyo especially huyo mdada ? Na asipo Pata tena mtoto baadaye ?

Ushauri wangu watunze mimba yao . Amwambie binamu yake ukweli . Mambo Mengine mbele ya safari .
 
Huyo ni mchumba sio mke.
Hakuna tatizo badili mwelekeo wa upepo.
Tangaza ndoa, watakushangaa kwa muda mwisho utakuwa ushapata mke na mtoto.
Wote tunatenda dhambi ILA wenzio huwa tunajitahidi kuficha maovu yetu.
Hawa wadada nao usikute Alikuja kwako kwa mission maalum na wewe kwa kupenda Wanawake weupe wenye mizigo ukaingia bila kinga.
Pole sana
 
ha ha dhambi ya uzinzi hukuona.. any way amua moja kutoa hicho kiumbe au uoe kabisa
Jamani miss chagga,nilivyokuwa ninakuheshimu!!!,yaani siamini macho yangu km kweli wewe mwanamke unayejua uchungu na kiumbe unayesifika kwa kuwa na Huruma unaweza kumshauri huyu jmaa kutoa mimba,jamani tuwe na huruma;Hivi wazazi wetu wangetutoa mimba leo hii tungekuwa tunachat hapa JF??,Chonde jamani mawazo ya hivyo yasipate nafasi ktk akili zetu.
 
Si unajua ule usemi kitanda hakizai haramu.

Wanaweza kutoa je wataweza kuishi na maumivu ya moyo especially huyo mdada ? Na asipo Pata tena mtoto baadaye ?

Ushauri wangu watunze mimba yao . Amwambie binamu yake ukweli . Mambo Mengine mbele ya safari .
na hapo ndipo kazi ilipo!!
 
Weka kila kitu wazi. mtoto hafichiki. atakayenuna anune, atakayechukia achukie. limekwishatokea na halirekebishiki. mlee mtoto kwa 100%. maneno yatasemwa na undugu utabaki kuwa pale pale. uwanaume ni kuwajibila kwa matendo yako.
 
Back
Top Bottom