Ushauri: Nimempa mimba msichana na tayari nina mchumba

Ushauri: Nimempa mimba msichana na tayari nina mchumba

Mtoto wako akienda kulelewa na baba wa kambo, utajisikiaje???? Utajisikiaje akikwambia katoa hiyo mimba, roho yako itakuwa na amani kiasi gani??? Lakini vipi ukisikia huyo Mwanamke amefariki wakati akihangaika kuitoa hiyo mimba, utafurahi au utahuzunika??????

Ili kuwa katika sehemu salama, ni vyema kuikubali na kuilea hiyo mimba mkiwa pamoja (kama wazazi)...

Unaweza kuitelekeza hiyo mimba au kuitoa , kwa lengo tu LA kuendelea kuishi na huyo demu wako wa kisasa (mjini), vipi hapo baadae ukigundua huyo demu wako Wa sasa ANA MATATIZO YA UZAZI????

MWISHO NAKUSHAURI, Mwanaume makini huchukua maamuzi sahihi, kulingana na MAZINGIRA husika ya wakati huo.... sasa tafakari ni yapi maamuzi sahihi kwako kwa mazingira uliyo nayo?
 
Hebu mchukue fasta huyo uliye mpa mimba tayari, unataka nani aje kuwa baba wa kambo!!?
Huyo asiye na mimba tuachie, una ongeza group la ma single mothers bila sababu na mtoto inafaa alelewe na pande zote mbili vzuri.
Haya changamka kabebe ulo mzalisha fasta
Hahahahahahahahaha we jamaa
 
Baada ya kukaa mjini mda mrefu mwezi ulopita niliamua kwenda kijijini kuwasalimia wazazi. Katika mizunguko ya hapa na pale hapo kijijini nilikutana na rafiki angu wa toka kitambo japo sikua na mpango nae tena katika shamrashara za furaha tele moyoni akaamua anizawadie penzi nami sikuona shida kutokana na kulazimisha kwake nikamgegeda japo mara moja.

Chaajabu baada ya kurudi mjini Jana binti ananpigia simu kua anamimba yangu na anahitaji kunifata tuishi wote mjini vinginevyo anasema anaitoa mimba yangu kama kufa afe na kwetu kutoa mimba lazima mtu afe sababu ndo damu ya ukoo wetu ilivyo, nami nashindwa nifanye nini kwani tayari ninamchumba na anatambulika hadi nyumbani na kwao na nampenda sana siwezi msaliti na huku nilipo nipo masomoni japo uhuru wa kuishi na mke upo lakini nahitaji niishi na mke wangu.

Naombeni ushauri kwani binti kanipa mwezi mmoja wa kutoa maamuzi ya kutoa mimba au ni kubali kuishi nae kama mke binti sio mwanafunzi.

Nawasilisha wanaJF, matusi sipendi.
Pia anaweza akawa amekutegeshea tu sababu huwa anakuzimikia tangu kitambo, labda hiyo mimba alidungwa na mwingine kwanini aanze tu eti aseme aje aishi na wewe mjini, labda anataka tu wewe ndio uwe daraja la yeye kuja dar. Think big mkuu
 
Yaani nilitaka nikutukane kaka yangu ila nilivyoanza kutype tu hasira zikayayuka. Yaani hutaki kumsaliti mchumba ako wakati ushamsaliti!
Ni bora umwambie huyo mwanamke yanayoendelea! Huyo uliempa mimba anaonekana anataka sana kuja mjini!!! Hata kuacha kwa amani. Hapo hamna siri.
 
Mwenzio kaitumia fursa vizuri wewe ukadanganyika.
Alikusudia kubeba hiyo mimba mana kwa maelezo yako alikuwa anaforce.
Jiandae mana huyo kajipanga na nia yake umuoe.
Kaa ongea nae vizuri mweleweshe mana atakuharibia hadi kwa mchumba uliyenaye believe me.
 
Huyo aliamua kukutegeshea tuu, hamna namna ingine ni kuoa tuuu
 
Vijana mbona muko hivi.yaani unajua kabisa unamchumba then unaendekeza penzi la fasta fasta....mwenzako amekutega ukamruhusu kuingia kingi subiri akupige tutusa sasa...........ila fanya mamuui ya kiume......
 
Kweli wa kijijini wa kijijini tu
Asa ye aliamua kukuzawadia penzi katika siku zake za hatari

Alipanga kufanya ayo yote ili akuharibie tu. . . Na amefanikiwa

Pole mkuu
.....dah huyu dd alimpenda jamaa ndomaana kazawadia penzi siku za hatari ili ampate!
 
kusaliti ushasaliti lakn kama unampenda mchumba wako kwann hukutumia kinga angalau.? wanaume nashndwa kuwaelewa Jmn...
 
Sasa kama kwenu mtu akitoa mimba anakufa kwa nini unasex ovyoovyo!
Ona sasa una mchumba afu uko nako umevua! Unazani ni lift hiyo kwamba unaweza omba kwa yeyote!
Haya! Sisi kwetu unayefanya nae tendo la ndoa ndio mwanandoa mwenzako; unayezaa nae ndio mkeo
Rudi kijijini ukamchukue mkeo; na siku ingine uache misifa ya mjini
 
Nimesoma headline nikagundua wew ni mtu wa aina gani
 
inaelekea elimu ya kutumia kinga huna kila unaekutana nae kavukavu.hiyo dalili mbaya hata uliye mtia mimba namuinea huruma kwani ataletewa sana watoto wa nje.ajiandae.
 
Baada ya kukaa mjini mda mrefu mwezi ulopita niliamua kwenda kijijini kuwasalimia wazazi. Katika mizunguko ya hapa na pale hapo kijijini nilikutana na rafiki angu wa toka kitambo japo sikua na mpango nae tena katika shamrashara za furaha tele moyoni akaamua anizawadie penzi nami sikuona shida kutokana na kulazimisha kwake nikamgegeda japo mara moja.

Chaajabu baada ya kurudi mjini Jana binti ananpigia simu kua anamimba yangu na anahitaji kunifata tuishi wote mjini vinginevyo anasema anaitoa mimba yangu kama kufa afe na kwetu kutoa mimba lazima mtu afe sababu ndo damu ya ukoo wetu ilivyo, nami nashindwa nifanye nini kwani tayari ninamchumba na anatambulika hadi nyumbani na kwao na nampenda sana siwezi msaliti na huku nilipo nipo masomoni japo uhuru wa kuishi na mke upo lakini nahitaji niishi na mke wangu.

Naombeni ushauri kwani binti kanipa mwezi mmoja wa kutoa maamuzi ya kutoa mimba au ni kubali kuishi nae kama mke binti sio mwanafunzi.

Nawasilisha wanaJF, matusi sipendi.
Dar hatupendagi ujinga
 
Yeye anachoona eti anataka atoe mimba au ajiue
mimba imebambikiwa hiyo ikane halafu m-block simu yake umeingizwa mtegoni halafu unaingia king kichwa kichwa na akitoa mimba afi wala nn achana na mambo ya jadi hapa jukwaani.
 
mimba imebambikiwa hiyo ikane halafu m-block simu yake umeingizwa mtegoni halafu unaingia king kichwa kichwa na akitoa mimba afi wala nn achana na mambo ya jadi hapa jukwaani.
Nashukuru Kwa ushaur wako mzuri
 
Back
Top Bottom