Ushauri: Ndoa yangu ina miaka 7, nimegundua mume wangu alinificha ana mtoto wa miaka 8

Nothing4good

Senior Member
Feb 19, 2011
180
55
Tumpe ushauri huyu dada.

Ndoa yangu ina miaka 7 ila uhusiano wetu una miaka11. Nina watoto 2 na sasa ni mama kijacho. Mwaka Jana mwishoni nilipata kuwashwa ukeni nikaenda kupima nikaambiwa nina ugonjwa wa zinaa, nikatibiwa na nikaambiwa na mume wangu akatibiwe, nikamwambia hali halisi, akakataa akidai hajisikii chochote hivyo hawezi kupima, nikamlazimisha sana akakubali kupima akapatiwa dawa. Tangia nikutane na mume wangu sijawahi kuchepuka.

Nikamuuliza mwenzangu ananisaliti? Akakataa katakata hajawahi kunisaliti akadai labda maji wanayoogea huko kazini kwao (yeye yupo mkoa mwingine ni kweli wanatumia maji ya visima) mimi kwa kweli sikurizika na majibu yake nikaanza kufanya uchunguzi wangu nikagundua alikuwa na wanawake 3 ila mmoja wao ameachana naye tena kwa ugomvi mkubwa mpaka amemblock kwani ndiye aliyemuambukiza wale wengine 2 bado alikuwa anaendelea nao.

Nilimuuliza tena akakataa nilipomuonyesha vithibiti vya Picha, SMS, na majina yao akakubali na kuomba msamaha huku akilia na Magoti kapiga, sikumjibu chochote nilikaa tu kimya, aliomba ruhusa kazini wiki mzima akawa tu anaomba msamaha nilimsamehe ila nilipanga kutengana naye kwa mda, na nilikuwa naenda kwetu kulikuwa na sherehe hivyo niliwaza nikienda sitarudi kwake.

Kama alilijua hilo naye akataka tuongozane kwenda harusini hivyo nikawa sina jinsi zaidi ya kwenda na kurudi pamoja. Kipindi chote hicho hatukuwahi kufanya mapenzi mpaka mwaka huu mwanzoni aliponiambia kama nimemsamehe kweli tufanye tendo la ndoa kweli nikamkubalia ila kwa kinga cha ajabu mwezi 2 sikuziona siku zangu nikafanya kipimo nikajikuta nina mimba.

Nikamuuliza umenifanyia makusudi hivyo kwanini? Akadai eti alijua tu asiponifanyia hivyo nitamuacha hivyo anaomba nimsamehe sana. Nikawa sina jinsi ndio hivyo. Sasa hivi juzi nikakagua simu yake nikagundua anamtoto wa miaka 8 anamsomesha na wazazi wake wanajua kwani nimeona kuna mpango wa kumpeleka boarding au aje kwa baba yake kwani mazingira ya kwa mama yake, mtoto hayataki.

Sasa kama nimefichwa hata na hili wananitakia mema kweli?
 
Tumpe ushauri huyu dada.

Ndoa yangu ina miaka 7 ila uhusiano wetu una miaka11. Nina Watoto 2 na sasa ni mama kijacho. Mwaka Jana mwishoni nilipata kuwashwa ukeni nikaenda kupima nikaambiwa nina ugonjwa wa zinaa, nikatibiwa na nikaambiwa na mume wangu akatibiwe, nikamwambia hali halisi, akakataa akidai hajisikii chochote hivyo hawezi kupima, nikamlazimisha sana akakubali kupima akapatiwa dawa. Tangia nikutane na mume wangu cjawahi kuchepuka.

Nikamuuliza mwenzangu ananisaliti? akakataa katakata hajawahi kunisaliti akadai labda maji wanayoogea huko kazini kwao (yeye yupo Mkoa mwingine ni kweli wanatumia maji ya visima) Mimi kwa kweli sikurizika na majibu yake nikaanza kufanya uchunguzi wangu nikagundua alikuwa na wanawake 3 ila mmoja wao ameachana naye tena kwa ugomvi mkubwa mpaka amembock kwan ndiye aliye muambukiza.wale wengine 2 bado alikuwa anaendelea nao.

Nilimuuliza tena akakataa nilipomuonyesha vithibiti vya Picha, SMS, na majina yao akakubali na kuomba msamaha huku akilia na Magoti kapiga, sikumjibu chochote nilikaa tu kimya, aliomba ruhusa kazini wiki mzima akawa tu anaomba msamaha nilimsamehe ila nilipanga kutengana naye kwa mda, na nilikuwa naenda kwetu kulikuwa na sherehe hivyo niliwaza nikienda sitarudi kwake, kama alilijua hilo naye akataka tuongozane kwenda harusini hivyo nikawa cna jinsi zaidi ya kwenda na kurudi pamoja. Kipindi chote hicho hatukuwahi kufanya mapenzi mpaka mwaka huu mwanzoni aliponiambia kama nimemsamehe kweli tufanye tendo la ndoa kweli nikamkubalia ila kwa kinga cha ajabu mwezi 2 sikuziona siku zangu nikafanya kipimo nikajikuta nina mimba.

Nikamuuliza umenifanyia makusudi hivyo kwa nini? Akadai eti alijua tu asiponifanyia hivyo nitamuacha hivyo anaomba nimsamehe sana. Nikawa sina jinsi ndio hivyo. Sasa hivi juzi nikakagua simu yake nikagundua anamtoto wa miaka 8 anamsomesha na wazazi wake wanajua kwani nimeona kuna mpango wa kumpeleka boarding au aje kwa baba yake kwani mazingira ya kwa mama yake, mtoto hayataki.

Sasa kama nimefichwa hata na hili wananitakia mema kweli?

Ulishakanywa juu yake sio? Ref Mmmm! Mamdogo jamani!!!!
 
Pole sana Kawaida ya Mwanaume kamili lazima awe msiri sana hasa kwenye mambo aliyofanya kabla ya ndoa.

Huyo mtoto Mwenye miaka 8 ina maana alikuwepo kabla ya mahusiano yenu ya miaka 7 hivyo kama hakuwa tayari kukushirikisha hilo toka zamani sio jambo la kuvunja mahusiano yenu ila kama anatembeza Rungu hadi kwenye visima vya mafuta mwambie apunguze asije kulipukiwa akakupatia madhara.

"Mimi siku mwenzi wangu akigundua siri zangu sijui nitaweka wapi sura yangu"
 
Duuhhhh ila mi huwa niko makini sana!sitaki mke apate machale yoyote na mi!niko very decent and innocent.
Hata simu yangu anakagua anapekua lakini hajawahi kukuta sintofaham yoyote!
Lakini behind the scene angejua shetani ni mdogo wangu wa mwisho
 
kaa chini uyakabili..
~akupe sabaabu pia za kukuficha.?
~na ikiwezekana mnyime tena cha usiku

*tulia utunze wanao...na dumu katika ibada
 
pole sana, huyo jamaa anashindwa kuwa muwazi wakati anajua kabisa mnafamilia na watoto, sina cha kukushauri ila cha msingi mkalishe chini mwambie akuambie a to z
 
Duuhhhh ila mi huwa niko makini sana!sitaki mke apate machale yoyote na mi!niko very decent and innocent.
Hata simu yangu anakagua anapekua lakini hajawahi kukuta sintofaham yoyote!
Lakini behind the scene angejua shetani ni mdogo wangu wa mwisho
hahahahahahahaah
 
kaa chini uyakabili..
~akupe sabaabu pia za kukuficha.?
~na ikiwezekana mnyime tena cha usiku

*tulia utunze wanao...na dumu katika ibada
Mkuu, kwa kawaida huwa tunaeleza matatizo na madhaifu ya wenzetu, ni mara chache sana mtu kueleza matatizo ya mwenzake pengine akataja na visababishi vya matatizo hayo.

Najaribu kusema, ndoa za siku hizi WANANDOA wanasisitizwa sana kuwa na siri(privacy) na hasa kwenye simu.....sasa kama wanafundishana kuogopa kujua mwenzio anawasiliana na nani, ANATAKA matokeo ya PRIVACY hiyo ndio aambiwe?

Kumnyima NAMNA GANI si adhabu, kabla hajajua walikuwa wapo watano( Jamaa na Wanawake watatu, na mmoja kati ya wanawake hao kaleta gonjwa la zinaa ikimaanisha na yeye ana angalau mtu mmoja zaidi ya jamaa).
 
jamaa atakuwa nakula malaya sana huyoo dhuu hadi zinaa hatari sana yaniii hao wanawake zake na wao ni vicheche kuliko hata jamaaa
 
Pole zake....

Ingekuwa mimi hata sijui ningewezaje ku handle this situation very well.
Labda ningemfukuza aende tu, hata kama nampenda vipi.

Kama ameweza kuficha madudu yake kwa kipindi chote hicho tena mkiwa kwenye Ndoa, kitu gani kitamfanya abadilike sasa.? Huyo Dada atakuwa ana mshuku mumewe kila siku, na nina Imani Uaminifu na heshima juu yake vimeshakufa kwa sasa, na mahusiano bila Uaminifu ni kupotezeana mda.

Nashindwa kukupa Ushauri wa kukufaa, kaa naye chini Muyaongee kwa kina, umsikie sababu zake labda unaweza ku move on from there. Fanya kile unachoona kitakufaa wewe na wanao.
 
Kuhusu mtoto wake sio inshu maana mtoto hana kosa na NISHARITI AMLEE.

kuhusu michepuko yake, Niwewe kuamua nn ufanye nahasa ukizingatia kosa sio kosa ,kosa nikurudia kosa.....ila hapa nishariti uwe mwenye uhuru kuanzia kichwani.

Kuhusu Mimba yako ,ni mimba ni baraka..kwan ulitaka uitoe wakat km kuzaa unawatoto wawili???.
 
Back
Top Bottom