Kapyepye Mfyambuzi
JF-Expert Member
- Jun 18, 2020
- 542
- 924
Habari wakuu?
Nina rafiki yangu ambaye ameoa mwaka Jana. Sasa ameniomba ushauri nimeona nije niwashirikishe na nyie ili tuone jinsi ya kumshauri kijana mwenzetu. Wakati anakutana na huyo mchumba wake ambaye Sasa hivi ni mke wake, kabla ya kumuoa alimkuta anaishi yeye pamoja na mdogo wake kwenye chumba kimoja alichokuwa amepanga. Mdogo wake huyo ambaye ni shemeji yake na yeye ni mkubwa tu alishazalishwa watoto watatu wapo kwa bibi yao Kijijini. Sasa baada ya kumuoa ikabidi mke wake kile chumba amwachie mdogo wake.
Mgogoro ulianzia Hapa,,,[emoji675]
Mdogo wake na mke wake ambaye yeye rafiki yangu anamwita shemeji, kazi anayofanya haimkizi mahitaji Kama kulipa kodi ya chumba, kula kuvaa n.k, kibaya zaidi hata yule mwanaume aliyemzalisha hataki hata kumsikia. Sasa rafiki yangu huyu huruma ikamuingia ikabidi amsaidie kumlipia kodi shemeji yake.
Kipindi cha mwanzoni alimlipia kodi ya miezi miwili. Sasa hivi kamlipia kodi ya miezi sita, mkewe amemcharukia, amenuna hamsemeshi, nyumba imekuwa chungu. Sasa rafiki yangu huyo yupo njia panda, hajui afanyeje, amenisimulia na kuniomba ushauri, na mimi nimeona ni bora niwaletee wanabodi ili nijue jinsi ya kumshauri.
Nini mawazo yako au ushauri wako?
Nawasilisha