Ushauri: Nataka niende Dubai kufanya kazi

Caro Lynah

Member
Jul 18, 2016
71
61
Habari waungwana,

Kutokana na maisha kuwa magumu, nimeamua kwenda Dubai kutafuta maisha kivingine. Kwa anaepajua au ataekuwa tayari kuongozana na mimi anakaribishwa kusema lolote la kunijenga sio kukatisha tamaa.
 
Kwa kuwa una experience ya hospitality industry na security, nnakushauri tafuta kupitia mtandao mawakala wa majumba ya kwenye zile rich housing compounds kama vile "The world" na "palm" villages.

Huko kuna majumba ya matajiri kutoka sehemu mbalimbali duniani ambayo wameyanunuwa kwa prestige tu na kuishi kwao ni mara chache sana kwa mwaka.

Ukipata kazi hapo ya ku upkeep nyumba moja ina maana minimal work na fat pay.

Fanya. Kila kitu kinawezekana.
 
Kama una ujuzi na elimu na una nafasi ya kuutumia huko Dubai nenda.

Mabaunsa wengi kutoka mtaani hapa hua wanaenda Dubai kufanya kazi zisizohitaji elimu mfano ulinzi klabu na kuwa walinzi wa swimming pools, wanasema mshahara ni mdogo sana hauzidi 300,000/= ya hapa.
 
aisee mshahara wa laki tatu??? mi jitu ni miongo aisee! i once did manual labor huko but mshahara was no where near laki tatu...

jombaa kule kupo poa... wakenya wengi sana kule wanapiga kazi. kuna franchise moja inaitwa Al shaya wanachukua sana watu wa east africa wacheki kwa site yao unaweza pia kuomba kwa hiyo hiyo site yao.
 
9729f68a458e769edb7922187f1ee109.jpg
 
Kuna mdada namfahamu yupo oman anapiga kazi za ndani,ananyumba tayari ila hajapaua,maisha ni popote tu jamani
 
kuna madada wanafanya za ndani( beki 3) wanakula laki 8 kila mmoja kwa mwezi wanajenga kwao Tanga
1)Marcelo anakula na kila kitu kwenye nyumba husika,anasave mshahara wote.
2)Patrice Evra anaweza kuwa supersub wa make was bosi. Full kuhongwa.
 
Acha uongo hakuna mshahara wa laki 3 dubai. Kama hujui vitu uliza. Nipo dubai huu Mwaka wa tano. Kama una tatizo niulize nikujibu
Wewe ndo ungekuwa msaada kwa huyu mleta Mada hebu mpe ukweli basi
 
1)Marcelo anakula na kila kitu kwenye nyumba husika,anasave mshahara wote.
2)Patrice Evra anaweza kuwa supersub wa make was bosi. Full kuhongwa.
Marcelo. Evra wanasave asee kuhusu kuwa supersub ni ngumu kwa Dubai. sema wanalia na ubaguzi, matusi na Kutoakuwa huru means hawatoki ndani. mmoja wao nilikuwa namsaidia kwenda kupokea kila mwezi anatuma laki 6 za ujenzi kashapau mwingine ndugu zake walimpiga sana sema yake ipo kwenye linta. huwa wananiambia matumizi yao makubwa vocha tuuu
 
Back
Top Bottom